Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Dah Pole sana Folk nakumbuka nilivyokuwa nangojea kifo cha Mama yangu kisa Cancer ya Figo, Bandama na Ini hakika bora usikie kifo cha ghafla ila usikae kusubiri msiba.

Tangu kipindi hicho amefariki Mama najua hataondoka mtu mwingine duniani nishangae.
 
Mungu baba tusamehe wanao tunaopata vijitatzo vdg tunalalamika mpk tunakufuru, naomb tupate cha kujifunza wanandugu, m mtu wa utani sana na nimeingia humu nitanie watu matokeo yake nimeamua nimuombee popote alipo
 
Dah Pole sana Folk nakumbuka nilivyokuwa nangojea kifo cha Mama yangu kisa Cancer ya Figo, Bandama na Ini hakika bora usikie kifo cha ghafla ila usikae kusubiri msiba.

Tangu kipindi hicho amefariki Mama najua hataondoka mtu mwingine duniani nishangae.
Duuh poleni sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliambiwa nikipatiwa good medication naweza kuishi hadi miezi nane. Lakini matibabu ni gharama kubwa na sihitaji msaada niko Kwenye critical stage na napata maumivu makali sana. Nahisi ni vema nife nipumzike.
..............Nimekosa cha kuandika,pole sana ndugu yangu.

Jiandae sasa Roho yako iende ikapokelewe na mikono salama ya Mungu.sina nia kukukatisha tamaa ila ukweli ni huo,mimi nitakufa yule atakufa issue ni jinsi gani tumejiandaa?at least umeambiwa na limit unaijua mtihani upo kwetu tusiojua lolote kuhusu afya zetu pengine tunaweza kukuacha hai sie tukatangulia who knows?!

Sali kwa imani yako unayoiamini Mungu akupunguzie maumivu,atatenda kazi yake akiona muda wako umefika...Mungu ni mwema sana,kwa huruma yake utaiona paradiso maana kuna post yako nimesoma ukisema more than 19yrs upo ktk mateso makubwa,kwa jicho la imani hii miaka duniani inaweza kuwa ndo kuzimu yako ila maisha baada ya haya ya mwili wa nyama yatakuwa mazuri sana kwa nafsi yako.

Mungu Baba akusaidie akipenda kukuponya akuponye akipenda kukuchukua basi ukawe mmoja wa wanaoizunguka meza yake takatifu iliyojaa mazuri yote.....Amina.

Nakuweka ktk sala zangu kukuombea binadam mwenzangu maana sijui kesho nitakukuta wapi na utanisaidiaje kuniombea na mimi.

Haya maneno yanafariji mno, naungana na wewe katika sala kumuombea huyu ndugu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu huwa anatafuta binadamu wakumsimangia shetani na ukiamini basi wewe ni miongoni mwa ambao Mungu huwatumia kama hazina yake.

Kimsingi uwepo ama nguvu za Mwenyezi Mungu huwa zinaonekana pale ukomo wakufikiri wa mwanadamu unapofika mwisho.

Maradhi kama haya ambayo dawa za kila aina zimegonga mwamba,wabobezi wa kitabibu wa kila aina wame declear kukosa suluhu kiasi cha kusema dhahiri kwamba kwa ugonjwa huu lazima afe.

Hakika hicho ni kipindi ambacho shetani anajitahidi sana kutunishiana misuli na Mungu muumba ili tu apate kuuaminisha uma kuwa yeye yupo na atakalo liamua wakulipinga hayupo.

Tafadhari usimpe shetani ushindi badala yake ikaribishe imani kwamba Kristo yupo kwa ajili yako.

Tambua watu kama wewe ni hazina ambayo Mungu huwa inahitaji sana ili apate kumsimangia shetani.

Furaha ya baba ni kuona mwana yuko na afya njema ikibidi hata kwa vita na mapambano.Hakuna baba mwenye uwezo wakumsadia mwanae kumtoa kwenye taabu na kukata tamaa badala yake akamtelekeza.

Mungu wetu ni mwenye huruma na hakika ukiamini katika yeye hakika kupitia wewe Mungu atamsimanga shetani na hakika hilo linalosubiriwa kamwe halitatokea.

Imani ni zaidi ya tiba tunazozifahamu.

Be blessed.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom