Nimeambiwa Wajukuu hawaruhusiwi kurithi nifanyeje?

Nimeambiwa Wajukuu hawaruhusiwi kurithi nifanyeje?

i still kinda lost!
Mana kumbukumbu za kimahakama baso ni tatizo kutrace.

Mashauri yote ya mirathi miwili ni kama no traces.
Hapo inakuwaje wadau?
 
Wewe ni mtu mwema sana.....kwa kua wewe na mdogo wako ndio warithi wa wazazi wenu ,fanya hivi...tengeneza minutes za kikao cha familia(hakikisha huwashirikishi hao ndugu bali tumia majina yao na wasainie kama kikao kimefanyika)tafuta cheti cha kifo cha mzee kafungue mirathi...na fanya unavyoweza mahakamani wa expadite hili zoezi...ukishapewa mamlaka ya msimamizi wa mirathi...nenda kafanye transfer ya hizo nyumba kuja majina yako/wajukuu uliowakusudia....kikubwa fanya kwa usiri hao mafia wasijue.
1. Mleta hoja, usifuate Ushauri huu kwani unapotosha.
Ukifanya hivyo utakuwa unafanya jinai ya kughushi nyaraka (Kughushi Muhtasari wa Mirathi) na hukumu yake ni miaka saba gerezani endapo kama Mahakama ikikutia hatiani kwa kosa hilo.
2. Unachotakiwa kufanya Kwanza ni kushughulikia suala la Mirathi ya wazazi/ wamiliki wa awali wa hizo nyumba. Baada ya kukamilika kwa suala la mirathi ndipo sasa unaweza kuhamisha umiliki wa hizo nyumba kwenda kwa mtu yeyote yule utakayetaka.
Je, eneo/ardhi ambapo nyumba ilipo tayari imepimwa? Mmiliki wa hiyo nyumba aliyesajiliwa/anayetambulika kisheria ni nani?
Tafuta Mwanasheria Mzuri mwenye uelewa mpana katika Sheria za Mirathi na Sheria za Ardhi ili akuongoze katika hili.
 
Huwezi andika urithi kwa wanao Kwa nyumba uliyorithishwa na babako.

Mimi NI mrithi by default.
Mzee hakurithisha wajukuu zake.


yani mi narithi kwa babangu bila hata wosia unless wosia wake umenikana( Napo labda niwe nimefanya BAADHI YA makosa yaliyoainishwa kisheria mojawapo kulala na MKE WA Baba au kutomuuguza Baba mpk mauti)
Vinginevyo NI mrithi WA asili.

Kimbembe kwenda Kwa wajukuu!!

Watoto wangu wanarithi kwangu, kwa.mali nilizochuma Mimi!!

za babangu/ mamangu kama Hawakutamka kabla hawajafariki Mimi siwezi wajumuisha kwenye urithi WA kile nilichorithi kutoka kwao wether Kwa tamko au Kwa asili.

Sasa basi!!

Iwapo Mimi niliye mnufaika pekee wa Mali ya Wazazi wangu.
nikifariki!!
Mali Ile unarudi kwenye familia ya wahusika.
(Hapo sasa ndo Baba zangu wadogo wanapoingia kwenye hii issue)
Kabla ya kuandika wosia lazima abadilishe umiliki kutoka kwa Marehemu Baba yake kwenda kwenye jina lake, hapo Sasa atakua anaandika wosia Kama mwenye Mali baada ya zowezi la umiliki kukamilika!!
 
Kabla ya kuandika wosia lazima abadilishe umiliki kutoka kwa Marehemu Baba yake kwenda kwenye jina lake, hapo Sasa atakua anaandika wosia Kama mwenye Mali baada ya zowezi la umiliki kukamilika!!
Shukrani sana!
 
Back
Top Bottom