kwa-muda
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 2,097
- 5,348
Wana JF mimi si mwandishi mzuri kwa sababu niliishia na 5B, lakini ningependa tujadili suala fulani kuhusu elimu.
Toka serikali ijipange kwamba inabadilisha mtaala watoto primary watasoma kwa miaka sita, kuna mambo mengi ambayo bado hayajaeleweka. Hivyo nilielezwa na mwalimu jana haya yafuatayo:
Kwamba, wanafunzi ambao mwaka huu wako la tatu, hao ndiyo ambao wataishia la sita.
Hapa sasa nikawaza, kama kwenye shule za serikali kila mwaka madarasa na madawati hayatoshi, ina maana mwaka hao wanafunzi wa la 3 watakapokuwa wamehitimu la sita ili waendelee na sekondari, ndiyo huo huo mwaka ambao wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la nne mwaka huu watakapokuwa wanahitimu la saba ili nao waende sekondari. Ina maana kutakuwa na maelfu ya wanafunzi wanaoingia sekondari.
Sasa, sijui shule zetu zitaweza kuwapokea wote au maandalizi yatakuwa tayari au tutaanza kujiandaa baada ya kufika huo mwaka.
Nikaambiwa pia kuwa, mtaala umebadilika masomo ya sekondari yanafundishwa kwa kiswahili tena kuanzia wanaoingia sekondari mwaka kesho kwa shule za serikali. Hili sina hakika kama ni kweli, ila kama ni kweli je, tumejiandaa kwa vitabu.
Kama kuna jambo gumu ni kufundisha sayansi kwa kiingereza maana terms nyingi mwisho wa siku huwa tunarudia kuzitamka kwa kiingereza. Na kama vitabu tu vya kiingereza primary hivi vipya vina makosa mengi, itakuwaje pale vitabu vya chemistry, physics, biology vitakapotafsiriwa kwa kiswahili. Sijui serikali imejipanga vipi hapo.
Mtazamo wangu:
Najua watu watatoa mifano ya Ufaransa, China, Urusi na nchi kibao kuwa wanafundisha kwa lugha zao husia na wana maendeleo makubwa. Ila sidhani kama walifanya hivyo kwa kukurupuka. Nawaza kama hao watoto wakimaliza form 4, je, 5 na 6 nako wataenda kusoma kwa kiswahili?
Na kama lengo ni elimu iwe kwa kiswahili, mbona kwa sasa kuna shule nyingi za serikali zimejengwa ambazo zinafundisha kwa kutumia kiingereza? Mfano bunju nafahamu mbili baada ya moja kufungwa kwa sababu ilijengwa kwenye mkondo wa maji.
Vipi chuo? Wataenda kusoma kwa Kiswahili. Je, wataweza kucompete kwenye soko la ajira la kimataifa Isije kuwa wanaofanya na kuandaa haya, watoto wao wanasoma shule za mitaala ya Kiingereza tu mwanzo mwisho kwa sababu wanajua hii mitaala it won't work.
Sema, ifike wakati masuala ya elimu serikali iwe nayo serious. Hapa kuna uwezekano awamu nyingine akaja mwingine akabadilisha haya yote.