Nimeambiwa wanaoingia sekondari shule za serikali mtaala ni wa Kiswahili kwa masomo yote

Nimeambiwa wanaoingia sekondari shule za serikali mtaala ni wa Kiswahili kwa masomo yote

Unawaamini walimu wa shule za msingi. Kwanini usitafute taarifa wizara ya elimu? Walimu wa shule ya msingi sidhani kama watakua na taarifa nyeti kama hizo.
Unachosema ni kweli mkuu maana kila mwalimu ananipa version yake hadi ninashindwa kuelewa.
Lakini unadhani kama walimu wenyewe hawana taarifa na hizi unazirefer kama taarifa nyeti, hudhani kwamba wizara haijafanya kazi yake vizuri?
Maana walimu hao hao wa primary ni kiungo muhimu katika mikakati ya wizara nao ndiyo rahisi kuwafikishia taarifa wazazi.
 
Kwa sekondari haya masomo yangetakiwa kufundishwa kwa kiswahili kwa lazima shule zote
  1. History
  2. Civics
  3. Kiswahili chenyewe
Yaliyobaki hata kama tukiendelea na mombo sio mbaya. Kufundisha historia na uraia kwa kizungu inaweza kuwa moja ya sababu Tanzania ina taifa la wajinga wengi.
 
Kama ni hayo sawa. Ila kwa masomo ya sayansi itakuwa ni balaa kubwa sana.
 
Naona tuzingatie lugha ya malkia kama Kenya na Uganda, tusipokuwa makini katika soko la ajira la kimataifa tutakuwa mbumbumbu. Mf. Amekuja mwekezaji kutoka England, anatoa interview, Kenya na Uganda watachukuwa hizo kazi. Sisi ni mwendo wa yes na no tu.
 
Kosa letu la kwanza primary education kufundisha masomo yote kiswahili.
Kosa litakuzwa maradufu kufundisha masomo yote ya secondary education kwa kiswahili.
Na sijui wanapata ukakasi gani kuamua lugha moja tu, haswa kingereza kufundishia kuanzia elimu ya msingi.
 
hilo la kiswahili kufundishwa sekondari linashawishiwa na taasisi za haki elimu, lakini litaturudisha nyuma sana.
Litarudisha nyuma kivip mkuu sio kwamba itakuwa rahisi kuelewa tofauti na Sasa hivi. Hata leo hii ukiingia vyuoni ili mwalimu uelekeweke vizuri walau uchanganye na kiswahili.
Kinachotafutwa ni ujuzi na sio lughalugha0
 
Naona tuzingatie lugha ya malkia kama Kenya na Uganda, tusipokuwa makini katika soko la ajira la kimataifa tutakuwa mbumbumbu. Mf. Amekuja mwekezaji kutoka England, anatoa interview, Kenya na Uganda watachukuwa hizo kazi. Sisi ni mwendo wa yes na no tu.
Mashart yatawekwa kwa ajili ya kuaccomodate kiswahili, kwani wawekezaji wanatoka nchi zinazoongea kiingereza tu? Vipi kwa China ambako kinaongelewa Kichina ila bado wawekezaji wanakimbilia huko
 
Wana JF mimi si mwandishi mzuri kwa sababu niliishia na 5B, lakini ningependa tujadili suala fulani kuhusu elimu.

Toka serikali ijipange kwamba inabadilisha mtaala watoto primary watasoma kwa miaka sita, kuna mambo mengi ambayo bado hayajaeleweka. Hivyo nilielezwa na mwalimu jana haya yafuatayo:
Kwamba, wanafunzi ambao mwaka huu wako la tatu, hao ndiyo ambao wataishia la sita.

Hapa sasa nikawaza, kama kwenye shule za serikali kila mwaka madarasa na madawati hayatoshi, ina maana mwaka hao wanafunzi wa la 3 watakapokuwa wamehitimu la sita ili waendelee na sekondari, ndiyo huo huo mwaka ambao wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la nne mwaka huu watakapokuwa wanahitimu la saba ili nao waende sekondari. Ina maana kutakuwa na maelfu ya wanafunzi wanaoingia sekondari.

Sasa, sijui shule zetu zitaweza kuwapokea wote au maandalizi yatakuwa tayari au tutaanza kujiandaa baada ya kufika huo mwaka.

Nikaambiwa pia kuwa, mtaala umebadilika masomo ya sekondari yanafundishwa kwa kiswahili tena kuanzia wanaoingia sekondari mwaka kesho kwa shule za serikali. Hili sina hakika kama ni kweli, ila kama ni kweli je, tumejiandaa kwa vitabu.

Kama kuna jambo gumu ni kufundisha sayansi kwa kiingereza maana terms nyingi mwisho wa siku huwa tunarudia kuzitamka kwa kiingereza. Na kama vitabu tu vya kiingereza primary hivi vipya vina makosa mengi, itakuwaje pale vitabu vya chemistry, physics, biology vitakapotafsiriwa kwa kiswahili. Sijui serikali imejipanga vipi hapo.

Mtazamo wangu:
Najua watu watatoa mifano ya Ufaransa, China, Urusi na nchi kibao kuwa wanafundisha kwa lugha zao husia na wana maendeleo makubwa. Ila sidhani kama walifanya hivyo kwa kukurupuka. Nawaza kama hao watoto wakimaliza form 4, je, 5 na 6 nako wataenda kusoma kwa kiswahili?

Na kama lengo ni elimu iwe kwa kiswahili, mbona kwa sasa kuna shule nyingi za serikali zimejengwa ambazo zinafundisha kwa kutumia kiingereza? Mfano bunju nafahamu mbili baada ya moja kufungwa kwa sababu ilijengwa kwenye mkondo wa maji.

Vipi chuo? Wataenda kusoma kwa Kiswahili. Je, wataweza kucompete kwenye soko la ajira la kimataifa Isije kuwa wanaofanya na kuandaa haya, watoto wao wanasoma shule za mitaala ya Kiingereza tu mwanzo mwisho kwa sababu wanajua hii mitaala it won't work.

Sema, ifike wakati masuala ya elimu serikali iwe nayo serious. Hapa kuna uwezekano awamu nyingine akaja mwingine akabadilisha haya yote.
Hii inawahusu watu wa hali duni peke yao, wale wenye uwezo wa kusomesha watoto wao private schools(hii ni pamoja na watunga sera wenyewe) na wale wenye uwezo wa kuwasomesha watoto wao nje ya nchi ndiyo watakuwa wanatengeza kizazi kitakachokuwa na advantages/opportunities nyingi mno. Hii kuwafanya walalahoi kutokuja kuweza kutoka katika chain hiyo ya ulalahoi kwa generations nyingi mbeleni.
 
Mkuu ina maana hizo hizo shule za msingi zitaongezwa madarasa ziwe pia na sekondari? Vipi miundombinu ya majengo maana hili linakuwa tatizo kila mwaka madarasa na madawati? Nimesikia pia lazima kabla mtu hajamaliza form 4 apitie masomo ya ufundi kama veta. Najiuliza kama maabara tu zilikuwa kikwazo, hili litawezekana kweli au ndiyo mafunzo ya vitendo kusomwa kwa nadharia.
Hili la vocational training ni zuri, ila najiuliza kama litaweza kutekelezeka.
Hakika madarasa yataongezwa kwa kila shule ya msingi endapo mpango na muongozo huu wa elimu utafanyiwa kazi kama inavyoelekezwa.

Elimu ya amali (ufundi na makorokoro yote) itafanyika sanjari na masomo ya kawaida katika ngazi ya msingi na sekondari.
 
Mashart yatawekwa kwa ajili ya kuaccomodate kiswahili, kwani wawekezaji wanatoka nchi zinazoongea kiingereza tu? Vipi kwa China ambako kinaongelewa Kichina ila bado wawekezaji wanakimbilia huko
TZ na China ziko sawa ktk Uchumi na Uwekezaji?
 
TZ na China ziko sawa ktk Uchumi na Uwekezaji?
Mpaka China inafika hapo ilipaaa jiulize ? Kabla ya China kupaa kiuchumi ilikuwa inatumia kiingereza kwenye mitaala yake ? Vip kwani japan wanatumia kiingereza kwenye mitaala Yao au kabla ya kuendelea walikuwa wanatumia kiingereza? Tuacheni inferiority complex kiswahili kinaweza kikawa English tu ila bado tunaabudu luggage za wenzetu
 
Mkuu ina maana hizo hizo shule za msingi zitaongezwa madarasa ziwe pia na sekondari? Vipi miundombinu ya majengo maana hili linakuwa tatizo kila mwaka madarasa na madawati? Nimesikia pia lazima kabla mtu hajamaliza form 4 apitie masomo ya ufundi kama veta. Najiuliza kama maabara tu zilikuwa kikwazo, hili litawezekana kweli au ndiyo mafunzo ya vitendo kusomwa kwa nadharia.
Hili la vocational training ni zuri, ila najiuliza kama litaweza kutekelezeka.
Maabara kwa kila sekondari ilishindikana itakuwa hizo shule za ufundi? hayo mawazo yatabaki vitabuni.
 
Mpaka China inafika hapo ilipaaa jiulize ? Kabla ya China kupaa kiuchumi ilikuwa inatumia kiingereza kwenye mitaala yake ? Vip kwani japan wanatumia kiingereza kwenye mitaala Yao au kabla ya kuendelea walikuwa wanatumia kiingereza? Tuacheni inferiority complex kiswahili kinaweza kikawa English tu ila bado tunaabudu luggage za wenzetu
Luggage ndio nini, wachina bila kujua kiingereza wala wasingefika hapo walipo, tuulize sisi tunaofanya nao biashara, na mchina kama hajui kiingereza aajiriki na wana kiingereza safi sio hicho chenu cha prof.Ndalichako
 
Kufundisha kwa kiswahili ni kurudi nyuma hatua 100000000. Siungi mkono kabisa.
Hakika ni kurudi nyuma.
Kwa mantiki hii kwa upande wa ajira za kuajiriwa tunakuwa tunalenga soko la ndani tu ambalo nalo litabase kwenye ajira za Serikali kwa kiasi kikubwa.

Wakenya na Wanyarwanda wataendelea kutake over.
 
Hili suala la lugha ya kufundishia limeturudisha nyuma sana watanzania Kwa kitunyima maarifa ya kusaka fursa nje ya Nchi.Inatakiwa tuachane na kiswahili kabisa tutumie lugha za kimataifa kama kiingereza au kifaransa.Kiswahili hakina tija labda kama tu gekuwa tu ajimudu Kwa Kila kitu kama ilivyo marekani au china ndiyo tungeng'ang'ania na kiswahili chetu tofauti na hapo ni kujichelewesha maendeleo Kwa wtz.
 
Shida Tanzania sio lugha ya kufundishia bali ni ubora wa elimu inayotolewa.
 
Back
Top Bottom