Nimeambiwa wanaoingia sekondari shule za serikali mtaala ni wa Kiswahili kwa masomo yote

Mambo ya kipumbavu kabisa kuwahi kutokea unawaigaje wajapan,wachina na mataifa mengine yaliyoendelea kutumia lugha zao kufundishia na huu ukapuku wetu si ndio tunazidi kuzama gizani, kiswahili kinakupeleka wapi
 
Walimu sasa wa hizo lugha nyinginezo kuacha kiingereza ndiyo hakuna kwa idadi kubwa.

Serikali ianzishe course ya ualimu yenye lugha nyingine kama kispain, kiItaly, kichina, kifaransa n.k ili sasa Walimu hao wakafundishe sekondari kuanzia kidato cha kwanza, na waweke ULAZIMA kwa mwanafunzi kuchukua somo mojawapo atakalofanyia NECTA ya form 4.

Na ili wanafunzi wawe siriazi na hizo lugha, warudishe PENALTI ya lazima endapo atafeli kama ilivyokua awali kwa Mathematics.
 
Luggage ndio nini, wachina bila kujua kiingereza wala wasingefika hapo walipo, tuulize sisi tunaofanya nao biashara, na mchina kama hajui kiingereza aajiriki na wana kiingereza safi sio hicho chenu cha prof.Ndalichako.
Uwenakiasi basi katika kuwelezea hao wachina wanoongea kiingereza safi maana sio wewe peke yako unayefanya kazi na wachina hapa Tanzania.
 
Hakika ni kurudi nyuma.
Kwa mantiki hii kwa upande wa ajira za kuajiriwa tunakuwa tunalenga soko la ndani tu ambalo nalo litabase kwenye ajira za Serikali kwa kiasi kikubwa.

Wakenya na Wanyarwanda wataendelea kutake over.
Na wanaopanga hiyo mipango watoto wao hawasomi hizo shule.
 
Kung'ang'ania Kiswahili Kwa nchi masikini kama Tanzania ilihali haina technolojia wala viwanda kiasi cha watu kusimama na miguu yao ni UPUMBAVU NA KUENDELEA KUFANYA WATU MASIKINI.

Soko la ajira la ndani ni kichefuchefu, vijana wanamaliza shule hawana ajira na hatuwezi kuwaaccomodate kwenye soko la ndani, kijana inabiti avuke mipaka akajitafutie - huko aendako lugha ni kiingereza - NI KUUANA NJAA TU.
Soko la ndani la ajira Kwa kiasi kikubwa ni sekta binafsi ambako mahitaji ni lugha ya kiingereza, tena inawekwa kabisa kama moja ya kigezo cha kupata kazi na interview inakuwa ni kiiingereza kabisa.

Kiingereza kwasasa hakiepukiki, tumeshachelewa kukikwepa, tuweje nguvu na juhudi watu wetu waongee kiingereza waweze kupata fursa nyingi.

China kwasasa watu wanajifunza kiingereza Kwa nguvu ili waweze kuwasiliana na dunia nyingine, maana Kwasasa watu wao wanatoka sana nje ya mipaka yao.
Kingine wachina wananguvu ya kiuchumi hivyo watu wao na makampuni yao oversees wanakuwa na wakarimani kurahisisha kazi zao.
Mchina anatoa sana scholarship watu kwenda China kusoma na moja ya sharti ni kujifunza kuchina, tafsiri watu wengi watakuwa wanajua kuchina na kuwasiliana nao wanapokuwa oversee.
Mchina kupitia ushawishi wake wa kisiasa na kiuchumi, amelazimisha na kuinfluence watu kuongea kichina.
 
Mtaala ulioboreshwa kwa kidato cha kwanza utaanza kutekelezwa mwakani, yaani 2025. Vitabu vya kiada vya kidato cha kwanza vipo tayari, na madarasa mengine maandalizi yanaendelea.

Mitaala iliyoboreshwa inapatikana kwenye website ya TET hapa TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…