ERoni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 48,052
- 104,677
I do love you too sis darling!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
I do love you too sis darling!
Nipo mjini sasa zile offer ulizokuwa unanipa sijui bado ziko au majanga yamekukumba na wewe?
Mrembo ni biashara gan japo nikuungishe rafiki yangu
Mimi nimekimbia ofisi juz kat wamepiga mnada furniture za ofis yangu wateja wangu wengi ni mashule na makampuni ya utalii
Pia niliagiza mizigo china imekwama uko tangu february ndugu mteja anataka refund alaf mkulungwa niko juu ya mawe balaa
Yaan kua CEO wa vikampuni uchwara ni stress balaa kuitwa tapeli nje nje yaan
Ya vinywaji bestie. Karibu Mwananyamala siku moja uniungishe hata maji tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Yani siamin kama hii corona umefka hapa
Nlikua nalaza laki kwa 4dys lakin now
Hata 10k ya kula inakosekana
god is good
Hongera sana kwa kufungua dream business yako mama.
nyapu hazitoki kabisaYa kuuza nyapu au?
Maana zingine zote kama zinastruggle kimtindo
Mimi silipi ada na nina mpango wakifungua shule nikadai ada iliyobaki ya miezi miwili.
Maana nililipa ya miezi 3 akasoma mwezi tu tukasimama corona.
Huku tumeitiwa Mitihani ya kufanya wakiwa nyumbani wakaambatanisha na Ada pamoja na usafiri eti wakifunga mwezi June 2020 ni km 180 + ada 800 inagonga 1M kwa mtoto mmojaUtalipa Ada huku wanafunzi wako nyumbani?
Wakikaa miezi miwili .. mishahara ya walimu wanatoa wapi?
Mambo ni magumu sana kwa sasa.Well hii thread ni kwa ajili ya wote tuliaoathiriwa kiuchumi directly na corona. Najua kila mmoja atakuwa ameathirika kwa level yake lakini nawaongelea wale waliopigwa pigo takatifu. Mfano anayefuga kuku wa kizungu atapeleka wapi na alikuwa anategemea watu wa catering kwenye mashughuli, watu wa catering na mapambo jamani eeee ndo hivo tena tupige goti tu naimani Jehovah adinai atatusikia.
Kuna wale wanaofanya biashara za importation na exportation jamani poleni sana wenzangu hiki kilio chetu sote.
Hotels, wafanyakazi na wajasi wnaotegemea watalii.
Wamiliki wa mashule jamani mbaya zaidi kipato hakuna lakini lazima ulipe mikopo ya bank na ulipie fixed costs.
Wauza uji mihogo n. K mashuleni poleni sana.
Sasa usiombe corona ikuathiri kwa kiasi kikubwa na huku una mkopo sijui bank sijui microfinance haloo hao watu wanajifanya kama vile hakuna kinachoendelea wao wanataka rejesho tu ilihali mikopo wamesitisha na pengine hata wao mishahara wamepunguziwa kwa kiasi fulani ila sasa kwa kupiga simu na kudai hao balaaa.
Kama mimi mkurugenzi na muanzilishi wa kampuni ninalia lia njaa fikiria wale wa chini yangu hali ikoje?
Shughuli za uzalishaji hakuna lakini fixed costs kama hela ya pango na ulinzi lazima nilipie natoa wapi mimi hizo ilhali sizalishi?
Binafsi nimefunga ofisi nimefunga na nyumba nimerudi kwa bi mkubwa vijana wa sasa wanasema kurudisha jezi eee ndo nisharudisha jezi hivo.
Na hii ni biashara yangu changa sana niliyoipambania usiku na mchana isimame. Ninmeipambania haswa wanaojua nini nachofanya humu na tuna mawasiliano ya karibu wanaelewa.
Lakini corona imeipenda zaidi.
Ooo kuna watu watakuja na sera zao hapa huna saving sijui akiba uncertainties bla bla nyie ndugu kama ninavyosema kujiajiri ni kugumu sana hasa kukuza biashara jamani ukisema utoe laki uweke akiba unawaza hii laki si nikinunua kitendea kazi fulani kitasaidia mauzo yaongezeke? Basi unachukua ile hela unaongeza vitendeo kazi.
Wajasiriamali na wafanyabiashara mliokuwa kwenye game mda mrefu hongereni sana na SHIKAMOOOOONI maana najua mmevuka vizingiti vingi.
Wale jirani zangu jamani nishatoka kijijini nimerudi mjini kwenye ugali wa bure mnaweza kuja tu kunisalimia.
Kuanziasha biashara zaidi ya mmoja kwa pamoja na kwa mda mmoja ni hatari; waweza ukajikuta umefeli pote.Ujasiriamali mgumu mumie,ndio mana tunashauriana kila siku
usiwe na biashara moja,maana ukija upepo kama huu kilio chake
sio cha kawaida,mtu unakuta ana 1M anataka kufungua biashara
anamaliza 1M yote kwenye biashara 1 huyu mtu lazima ipo siku atalia tu.
wakati alikua anauwezo akaigawa 1M akatoa biashara za 300k kama 3 hivi
ikiyumba hii ile inaenda na haziwezi kuyumba zote otherwise uwe ulikurupuka
wakati wa kuzifungua,Ujasiriamali maana yake ni ufanye biashara zaidi ya mbili.
Ila kwa hali ya sasa hamna mfanya Legal business mwenye amani,Hakuna Hali ni ngumu.
Easier said than done. Ukiona mtu ana biashara moja usifikiri ndio aliibuka tu hio moja ikakubali. Ni kwamba wengi washadunda kwenye biashara kibao kabla ya hio moja kusimama, sasa mtu kama huyu hadi aanzishe ingine sio kazi ndogo.Ujasiriamali mgumu mumie,ndio mana tunashauriana kila siku
usiwe na biashara moja,maana ukija upepo kama huu kilio chake
sio cha kawaida,mtu unakuta ana 1M anataka kufungua biashara
anamaliza 1M yote kwenye biashara 1 huyu mtu lazima ipo siku atalia tu.
wakati alikua anauwezo akaigawa 1M akatoa biashara za 300k kama 3 hivi
ikiyumba hii ile inaenda na haziwezi kuyumba zote otherwise uwe ulikurupuka
wakati wa kuzifungua,Ujasiriamali maana yake ni ufanye biashara zaidi ya mbili.
Ila kwa hali ya sasa hamna mfanya Legal business mwenye amani,Hakuna Hali ni ngumu.
Lakini pia biashara ni risk na hata ktk hiyo mpya aliyofungua bado hana uhakika nayoKuanziasha biashara zaidi ya mmoja kwa pamoja na kwa mda mmoja ni hatari; waweza ukajikuta umefeli pote.
Ni vizuri kuipa nafasi biashara mmoja ikisimama vizuri then ndo safari ya biashara ya Pili ifuate.
Nafikiri hata wenye biashara zaidi mmoja walifuata misingi hii. Hakuna mtu anayependa kuwa na biashara mmoja tu hiyo hiyo na akaridhika. Ila na kwanini urisk pesa yako ya mtaji kwa biashara tatu tofauti tena ambazo hujawahi zifanya kabla.
Nakubali wala sikatai kbs,ukawa na 1M au 2M au kiasi chochote ukaambiwa mpe mtu anzishe biasharaEasier said than done. Ukiona mtu ana biashara moja usifikiri ndio aliibuka tu hio moja ikakubali. Ni kwamba wengi washadunda kwenye biashara kibao kabla ya hio moja kusimama, sasa mtu kama huyu hadi aanzishe ingine sio kazi ndogo.
Kikwazo kikubwa ni usimamizi. Hizi biashara ndogo ndogo usiposimamia wewe mwenyewe utapiga hatua mbili mbele tatu nyuma. Na biashara ikisimama ukasema ngoja niwaachie watu niende kuanzisha ingine hii ulioiacha ukirudi utalia. Biashara zetu ndogo ndogo ni changamoto sana.
Unataka jibu langu. Nitampa mwenye wazo moja kwasababu huyu akili yake yote na juhudi zake zote ataweka sehemu moja, huyu wa tatu simpi, mshika mawili moja humponyoka. Biashara zenyewe anajifunza hizo tatu ataweza vipi?Nakubali wala sikatai kbs,ukawa na 1M au 2M au kiasi chochote ukaambiwa mpe mtu anzishe biashara
wakaja vijana wawili mbele yako mmoja akakupa wazo la biashara 1 ambalo atalisimamia kwa ufasaha
na aka kuahidi atarudisha pesa yako baada ya mwezi,Mwingine akakupa mawazo ya biashara 3 nae
akakuelezea na kuchambua atavyofanyaa kwa ufanisi na akakuahidi atarudisha pesa yako baada ya mwezi.
wewe kama mtoa mkopo,utampa nani huo mkopo wako kati ya vijana hao wawili mbele yako.
NOTE: VIJANA wote ni wapya ktk biashara wote hawana experience