Nimeamini jamani hakuna kitu kigumu kama wajasiriamali

Pole sana mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu injinia ukwaju my wife wako mgahawa wake uko wapi niwe unaenda kumuungisha kipind hiki kigumu cha biashara
yupo jirani na amu akulete tu Mkuu au akuelekeze
km leo kalaza supu na vyapati
 
Ya kuuza nyapu au?
Maana zingine zote kama zinastruggle kimtindo
nyapu hazitoki kabisa
kwa awamu hii zilishuka bei karibia na bure
sasa Corona vidume vinakimbia unajua hela ndio stimulator
 
Uzuri wa supu anaunga mchana inakuwa mboga.
Shida kwenye chapati sasa
nilimuelekezaga afunge kwenye Rambo halafu asubuhi ashtue kwenye Microwave
wengi hawajagundua ugumu wake
labda @Joowzey akishtuliwa hatakula tena
Corona kiboko dada amu
 
Mimi silipi ada na nina mpango wakifungua shule nikadai ada iliyobaki ya miezi miwili.
Maana nililipa ya miezi 3 akasoma mwezi tu tukasimama corona.
Utalipa Ada huku wanafunzi wako nyumbani?
Wakikaa miezi miwili .. mishahara ya walimu wanatoa wapi?
Huku tumeitiwa Mitihani ya kufanya wakiwa nyumbani wakaambatanisha na Ada pamoja na usafiri eti wakifunga mwezi June 2020 ni km 180 + ada 800 inagonga 1M kwa mtoto mmoja
kuuliza naambiwa mishahara ya walinzi kufyeka majani, wapishi walimu na wakurugenzi, eti mbona Serikalini wanalipwa? tulitakiwa tulipe zote kwa mkupuo walipoanza mwaka 2020 January kwani ni Bajeti
Jamani wawe na huruma watoto tupo nao majumbani wanakula kulala na kujisomea, mbona Muungano na Mei mosi wamefuta?
 
Mambo ni
Mambo ni magumu sana kwa sasa.
 
Kuanziasha biashara zaidi ya mmoja kwa pamoja na kwa mda mmoja ni hatari; waweza ukajikuta umefeli pote.

Ni vizuri kuipa nafasi biashara mmoja ikisimama vizuri then ndo safari ya biashara ya Pili ifuate.

Nafikiri hata wenye biashara zaidi mmoja walifuata misingi hii. Hakuna mtu anayependa kuwa na biashara mmoja tu hiyo hiyo na akaridhika. Ila na kwanini urisk pesa yako ya mtaji kwa biashara tatu tofauti tena ambazo hujawahi zifanya kabla.
 
Easier said than done. Ukiona mtu ana biashara moja usifikiri ndio aliibuka tu hio moja ikakubali. Ni kwamba wengi washadunda kwenye biashara kibao kabla ya hio moja kusimama, sasa mtu kama huyu hadi aanzishe ingine sio kazi ndogo.
Kikwazo kikubwa ni usimamizi. Hizi biashara ndogo ndogo usiposimamia wewe mwenyewe utapiga hatua mbili mbele tatu nyuma. Na biashara ikisimama ukasema ngoja niwaachie watu niende kuanzisha ingine hii ulioiacha ukirudi utalia. Biashara zetu ndogo ndogo ni changamoto sana.
 
Ukiona
Lakini pia biashara ni risk na hata ktk hiyo mpya aliyofungua bado hana uhakika nayo

kwakua umeshaamua kucheza ngoma,basi ingia uwanjani icheze ukisema ufanye kwa

kusikilizia upepo wa biashara 1,utajikuta unapoteza Muda na Pesa Pia maana hamnaga biashra

inakaa stable "kamwe" hata umfate bakhressa umuulize anataka nn atakwambia bado anadhani

taste ya zile ice cream zake sio tamu kama anavyotaka,anahtaji pesa zaidi kuboresha.

Muhimu ukishaamua kuwa mjasiramali jitose experience utaipata humo humo uwanjani maana

hamna chuo cha ujasiriamali DUNIANI ni mtu kuamua kukubali risk na kuzi face jicho kwa jicho.
 
Nakubali wala sikatai kbs,ukawa na 1M au 2M au kiasi chochote ukaambiwa mpe mtu anzishe biashara

wakaja vijana wawili mbele yako mmoja akakupa wazo la biashara 1 ambalo atalisimamia kwa ufasaha

na aka kuahidi atarudisha pesa yako baada ya mwezi,Mwingine akakupa mawazo ya biashara 3 nae

akakuelezea na kuchambua atavyofanyaa kwa ufanisi na akakuahidi atarudisha pesa yako baada ya mwezi.

wewe kama mtoa mkopo,utampa nani huo mkopo wako kati ya vijana hao wawili mbele yako.

NOTE: VIJANA wote ni wapya ktk biashara wote hawana experience
 
Unataka jibu langu. Nitampa mwenye wazo moja kwasababu huyu akili yake yote na juhudi zake zote ataweka sehemu moja, huyu wa tatu simpi, mshika mawili moja humponyoka. Biashara zenyewe anajifunza hizo tatu ataweza vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…