Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Alipata kusema Rais Mstaafu wa Tanzania wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi kuwa 'kila zama ina kitabu chake'. Nami sasa nimeamini baada ya 'kuweka' tafsiri yangu binafsi kwenye msemo huo uliojaa hekima na busara kubwa. Binafsi nimetafsiri kuwa 'kila awamu ina wake wa 'kutrend''. Yaani, kila awamu ya urais wa nchi hii yupo kiongozi wa kiserikali au kichama au mwananchi wa kawaida tu anayesikika na kusomeka sana.
Nitatoa mifano minne. Ulipoanza uongozi wa Hayati Magufuli, alikuwepo Dada Mange Kimambi. Alisikika na kusomeka sana akiukosoa utawala wa Hayati Magufuli-tena kwa maneno makali makali. Alikuwepo pia mwanamtandao aitwaye Kigogo2014. Hawa waliikosoa Serikali ya hayati Magufuli na kujiweka kama wenye kujua 'siri' mbalimbali za viongozi na uongozi kwa ujumla wake. Wakapita na sasa wamepoa.
Katika wakati huohuo, alijitokeza Cyprian Musiba. Huyu alijipambanua kama mwanaharakati huru. Lakini, kimsingi, alikuwa mwanaharakati mtetezi wa kufa na kupona wa uongozi wa Hayati Magufuli. Yeye alitumia maneno makali, vitisho na kashfa kwa wale alioamini kuwa walikuwa wakimpinga Hayati Magufuli. Akasikika na kusomeka sana kupitia runinga, mitandao ya kijamii na magazeti. Akapita na kupoa.
Sasa, mara tu baada ya kuanza kwa uongozi wa Rais na Mama yetu Samia Suluhu Hassan, amejitokeza Humphrey Polepole. Yeye hakosoi wala hatetei moja kwa moja uongozi uliopo madarakani. Kuona kukosoa au kuunga kwake mkono ni hadi msikiaji au msomaji atafakari kwa kina. Wapo wanaomuona kuwa ni mkosoaji wa serikali hii. Wapo wanamuona kuwa ni muungaji mkono wa serikali hii.
Polepole-akitokea kuwa mjasiriamali na mwanaharakati, Mjumbe wa Tume ya Katiba, Kiongozi wa serikali (Mkuu wa Wilaya) na chama (Katibu Mwenezi wa CCM) na sasa ni Mbunge wa kuteuliwa na Rais. Polepole amejibanza kwenye kutoa 'darasa' na elimu ya uongozi. Huchombeza pia kwa kukemea matendo na maneno ya viongozi katika utekelezaji wa majukumu yao. Ndiyo hapo anapoonekana kuwa mkosoaji.
Polepole sasa ni Musiba mpya-lakini yeye amechangamka kwa kuficha lengo lake la moja kwa moja la maneno na matendo yake. Polepole ni kitabu cha zama hii. Ni anaye-trend kuliko wengine. Hawa wote-Kimambi, Kigogo2014, Musiba na Polepole hutumiwa na nani na maslahi gani? Tuendelee kufanya tafakuri za kisiasa.