Nimeamini Tanzania tuna utawala wa sheria, kule Uganda Rais Museveni amesema ataongea na Jaji Mkuu dhamana kwa waandamanaji ifutwe!

Nimeamini Tanzania tuna utawala wa sheria, kule Uganda Rais Museveni amesema ataongea na Jaji Mkuu dhamana kwa waandamanaji ifutwe!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kiukweli nimeamini na nimekubali kuwa katika ulimwengu wa siasa Tanzania inafuata utawala wa sheria.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema ataongea na Jaji mkuu wa nchi hiyo ili kufuta dhamana kwa washtakiwa wote waliotenda kosa la kuandamana bila kibali.

Museveni amesisitiza kuwa kama Jaji mkuu hatakubaliana naye basi ataitisha kura ya maoni ili kubadili katiba.

Taarifa za kauli za Rais Museveni zimeripotiwa na ITV habari.

My take; Tanzania dhamana kwa wanasiasa ziko wazi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hivi mkuu mfano ukiwa si hata ukiena hospitali wodi ya wagonjwa mahututi lazima utakuta mwenye afadhali kuliko mwenzake? Lakini bado wote watakuwa wagonjwa mahututi wanazidiana tu kiwango cha umahututi.

Nao Uganda wana mazuri yao, mfano vyombo vya habari vingi vinajielewa ndiyo maana viligoma raisi kutumia cheo chake kuvishinikiza vicover kampeni zake eti akijifanya anahutubia taifa.
 
Humuoni jaji mkuu yupo na Jiwe kila siku, hujiulizi mmoja wa covid19 aliachiwaje usiku.

Utawala wa sheria my foot.
 
Kati ya Nchi Afrika zenye Raia Zezeta, basi Uganda ni no1.

Na ujinga wao huo ndo unampa kiburi Mh Dikteta.

Yani imefka hatua Mseveni katangaza ushindi kabla ya uchaguzi!!sasa nini maana ya kuwasumbua Raia kama unajua na unalengo kabsa kuwa huwezi kuachia ngazi?

Nyambafu Waganda!
 
Alichoongea Polepole kuhusu kuongea na Jaji Mkuu ndicho alichoongea Museveni kuhusu kuoongea na Jaji Mkuu, hiyo tofauti unayoiona wewe iko wapi!
 
Kati ya Nchi Afrika zenye Raia Zezeta, basi Uganda ni no1.

Na ujinga wao huo ndo unampa kiburi Mh Dikteta.

Yani imefka hatua Mseveni katangaza ushindi kabla ya uchaguzi!!sasa nini maana ya kuwasumbua Raia kama unajua na unalengo kabsa kuwa huwezi kuachia ngazi?

Nyambafu Waganda!
Mseveni hakupewa uraisi kwa ngonjera bali kwa mtutu wa bunduki.

Na sababu zilizopelekea kutwaa nchi bado ziko varied hadi leo.

Je umeishasikia Marekani au Uingereza inamshutumu au kumwekea Museveni vikwazo?

Kwa sababu wanatambua umuhimu wake kuendelea kuitawala nchi hiyo.
 
Daah kweli 🤔,lakini nini sababu ya mataifa makubwa kutoiwekea vikwazo Uganda? Kama unamaelezo ya kina tafadhali naomba ufafanuzi.
 
Daah kweli 🤔,lakini nini sababu ya mataifa makubwa kutoiwekea vikwazo Uganda??kama unamaelezo ya kina tafadhali naomba ufafanuzi
Mkuu for decades Uganda used to be a killing field, thousands if not millions perished between seventies and early nineties.

Na sababu zinaanzia mbali zaidi ya hapo baada ya uhuru waziri Mkuu Obbote kutunishana misuri na Mfalme Kabaka wa Buganda. Obbote akatumia jeshi kumuangamiza Mfalme Kabaka lakina nae Mfalme Kabaka a Sandhurst trained commodore aliyaangamiza vikosi vya jeshi la Obbote kabla hajasaidiwa na Iddi Amin kukata umeme uliokuwa nyezo kuu ya Electric powered Machine gun.

Lakini commodore Mfalme akaweza kuwatoroka katika mavazi ya utawa yaani sister.

Naye Obbote akaja ondolewa na Idd Amin, na Amin akatawala kwa mkono wa chuma aliangamiza watu malaki kama si mamilioni.
Si hiyo tu Wapinzani wa Amin wakisaidiwa na serikali ya Tanzania wakaja muondoa Idd Amin na baadae kumrudisha Obbote kwenye madaraka.

Obbote safari hii aliingia kulipiza kisasi akauwa waganda kwa maelfu na alipozidiwa akapora pesa zote za hazina na kukumbilia Zambia.

Katika danadana ya kuwania Uongozi ndipo akaja Museveni na NRA akaweza kuituliza na kuiunganisha nchi.

Museveni amepunguza ukabila na kujenga utaifa.

Usione vya elea,Uganda wanamhitaji Museveni labda kuliko anavyowahitaji.
 
Afadhali huyo anayesema ataongea na Jaji mkuu kuliko anayemwamuru jaji mkuu kutoa hukumu pasipo ridhaa yake kwa hiyo wewe unaposema kuna utawala wa sheria unajidanganya kumbuka wahenga walisema NYANI HAONI KUNDULE.
 
Back
Top Bottom