Nimeamini Tanzania tuna vichambuzi uchwara vya michezo

Nimeamini Tanzania tuna vichambuzi uchwara vya michezo

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Tanzania tuna vichambuzi uchwara vya michezo. Eti mtu akishawafahamu wachezaji 10 wa timu za Ulaya eti anatafuta kiredio uchwara nae akachambue habari za michezo. Ni watu wanaokatisha Tamaa wachezaji, makocha, na wadhamini wa timu. Wanagombanisha wachezaji kwa wachezaji, wachezaji na makocha, makocha na viongozi wa club na viongozi wa club na wafadhili.

Vichambuzi vyetu vinachambua mpira kwa kusukumwa na ushabiki wa timu zao.

Kuna kichambuzi uchwara wa kwenye kiredio uchwara eti amekasirika yeye kwanini Cedric na Zahera wamerudi tena Yanga, boo, kama vile ameambiwa atasaidia kuwalipa.

Kuelekea mechi ya ngao ya jamii, vichambuzi uchwara vilitoa nafasi kubwa kwa Simba kuishinda Yanga eti Simba Ina sakho na kanoute na Ina muunganiko kuliko Yanga.

Vichambuzi hivi vinaisifu Simba kucheza na Mazembe eti Simba Iko tayari kwa champions league.

Vikome
 
Hawajui hii ni profession mtu anasomea ...wenyewe wanakaa kwenye vijiwe vya kahawa na kutuletea story ambazo hazina ukwel wowote
 
Punguza jazba ndugu huu ni mpira tu .

Binadam mwenzako utamwitaje vichambuz uchwara? Si ajabu vimekuzid maisha ,vina uhakika wa kula kuliko wewe.

Hata km ni hasira hapo umevuka mipaka ,mbona wapo wakina maurid kitenge ni yanga damu kabisa na wapo upande wa yanga husemi? Kuwa mchambuzi haikufanyi usiwe na upande wa timu fulan ,hata marefa Wana timu moja wapo Kati ya Simba na yanga.

Utu ni Jambo la msingi ,Leo hii umejificha hapa na I'd fake unadharau utu wa watu km kweli wewe umekamilika nenda ig kaongee haya uliyoyamwaga hapa alafu watu wathaminishe maisha yako na ya hivyo vichambuz uchwara.

Chuki ,husda Mara nyingi vinamilikiwa na watu maskin wenye shida ya maisha wasio na uhakika hata wa Dona dagaa ,hasira zao huhamishia kwa waliofanikiwa .

Ile ni kazi km zilivyo zingine?

Vipi na manara tumuweke wap ambae kutwa kawadharirisha yanga Leo hii kawa mfalme hapo yanga na mnamshobokea waz waz ,ifahamike hizo ni kaz za watu so ukiona mtu fulan ameegemea upande fulan jua ndiko kwenye faida kwa mtazamo wake yeye na huenda ndiko anapatia ugali.

Me nadhan ungeanza na manara ambae kawanenea kila aina ya lugha nyie yanga leo kaja kwenu ni mfalme ,yupo zungu mbona ni yanga kabisa na ni mchambuzi wa mpira huwaoni?

Kisa leo mmeshinda ndio unaona mwisho wa dunia ,kulia kupokezana kucheka kupokezana punguza dharau
 
Wako wachambuzi aina ya shafii dauda, Ally Mayai ambao mara nyingi kama sio zote wanapokuwa nyuma ya Mike wanafahamu kuwa wanasikilizwa na watu wenye mapenzi na timu tofautitofauti hata kama wao ni wapenzi wa timu zao.

Wanachambua mpira kwa weledi sio ushabiki kama wa akina Gembe, Job, na wengine.
 
He kwahiyo una uhakika kuwa mimi nakula kwa wazazi? Njoo inbox nikwambie tukutane wapi ili uone ni mtu wa aina gani na Nina nini.

Ninachosema hapa kuwa nyuma ya Mike kwenye chombo Cha habari lazima ujue kuwa unasikikizwa na watu wote.

Kwakuwa hicho chombo Cha habari sio Cha timu yako unayoishabikia basi uwe mwangalifu. Kuna maneno ambayo yanastahili kusikika kwenye chombo Cha blhabari Cha timu husika au kiongozi wa timu husika.
 
Paragraph ya pili kutoka chini hata Kocha Nabi anakiri Yanga hawana muunganiko
 
Wako wachambuzi aina ya shafii dauda, Ally Mayai ambao mara nyingi kama sio zote wanapokuwa nyuma ya Mike wanafahamu kuwa wanasikilizwa na watu wenye mapenzi na timu tofautitofauti hata kama wao ni wapenzi wa timu zao. Wanachambua mpira kwa weledi sio ushabiki kama wa akina Gembe, Job, na wengine.
Shafii Dauda nakukatalia. Jamaa ni mnafiki, muongo na mzushi sana hayuko professional na kazi yake
 
Yule mnafiki wa Efm Mwenye majina ya O-O Sjui Kwa Sasa Ana Hali Gani Huko Aliko [emoji58][emoji58]
 
Kuna yule mchambuzi wa wasafi anaitwa George Job, juzi eti amekaza misuli kabisa eti kwanini Yanga wamewarudisha Kaze na Zahera

Anasahau kwamba Zahera alishika nafasi ya pili kwenye msimamo wakati Yanga inapitisha mabakuli jukwaani kama ombaomba

Shida ya wachambuzi wengi wanaongozwa sana na mihemko yao

Let's take a look at Ally mayai japokuwa anafahamika ni yanga kabisa ila uchambuzi wake upo very clear without doubt, George Ambangile shout out kwake.
 
Kuna wachambuzi wapo EFM
Mmoja anakipara na mwingine anavaa miwani yaani hawa kila jambo Yanga wanalofanya ni baya tu hawajawahi kusifia wao ni kuponda tu.
Akina nani hao mbwiga.
 
Yule mnafiki wa Efm Mwenye majina ya O-O Sjui Kwa Sasa Ana Hali Gani Huko Aliko [emoji58][emoji58]
Shida Yao wanazibeza Zanaco na Rivers kuwa ni timu ndogo kuliko Mazembe ya Sasa, hivyo Yanga haikustahili kufungwa na timu hizi, lakini Simba ilikuwa halali kufungwa na TP Mazembe. Huu ndio upuuzi wao, hawaangalii mchezo uwanjani. Mara zote waliwasifu Kanoute, Sakho, Banda na muunganiko.

Niliwaambiaga kuwa wachezaji wazuri sana wa Nigeria, Mali, Senegal, Ghana, Cameron, Burkina Faso hawaji kucheza Tanzania, woooote wazuri wanaenda timu za Ulaya na Afrika kaskazini. Hivyo, ukimuona mchezaji wa ukanda ule anakuja huku kwetu kiwango chake sio Cha kutisha sana, ni Cha akina ambundo, Bocco, lusajo, mzamiru, na Dickson Job tu.

Congo mpira umeshuka, TP Mazembe inaweza kufungwa na Rivers na Zanaco pia.

Vichambuzi vyetu viliudharau pia mchango wa kukosekana kwa Aucho, Mayele na Fiston djuma kwenye Yanga kufungwa Rivers. Waling'ang'ania timu mbovu timu mbovu haina muunganiko kiasi Cha kuhatarisha kazi ya Nabi Yanga. Ilimbidi Nabi naye ajitetee kwa kusema timu haina muunganiko anahitaji miezi 3.

Vichambuzi vikaipa Simba kichwa kuwa Ina muunganiko, Iko vizuri, inacheza vizuri, Sakho, Sakho Sakho Banda Banda kanoute, wachezaji wamezoeana hadi Gomez na Mwamed wakapata kichwa.

Vichambuzi vyetu na hata Gomez walikuwa hawausemi ubaya wa kukosekana kwa Chama na Miquissone kwenye kikosi Cha Simba kuwa ni tatizo. Wanasema Sakho na Banda na kanoute wameyaficha mapengo ya Chama na miquissone,, thubuuuuutu!!!! Wale jamaa ndio waliokuwa wakiamua Simba ifungwe na kufunga ngapi kwenye mechi.
 
Shida Yao wanazibeza Zanaco na Rivers kuwa ni timu ndogo kuliko Mazembe ya Sasa hivyo Yanga haijustahili kufungwa na timu hizi, lakini Simba ilikuwa halali kufungwa na TP Mazembe. Huu ndio upuuzi wao hawaangalii mchezo uwanjani. Mara zote waliwasifu Kanoute, Sakho, Banda na muunganiko.

Niliwaambiaga kuwa wachezaji wazuri sana wa Nigeria, Mali, Senegal, Ghana, Cameron, Burkina Faso hawaji kucheza Tanzania, woooote wazuri wanaenda timu za Ulaya na Afrika kaskazini. Hivyo, ukimuona mchezaji wa ukanda ule anakuja huku kwetu kiwango chake sio Cha kutisha sana ni Cha akina ambundo, Bocco, lusajo, mzamiru, na Dickson Job tu.

Congo mpira umeshuka, TP Mazembe inaweza kufungwa na Rivers na Zanaco pia.

Vichambuzi vyetu viliudharau pia mchango wa kukosekana kwa Aucho, Mayele na Fiston djuma kwenye Yanga kufungwa Rivers. Waling'ang'ania timu mbovu timu mbovu haina muunganiko kiasi Cha kuhatarisha kazi ya Nabi Yanga. Ilimbidi Nabi naye ajitetee kwa kusema timu haina muunganiko anahitaji miezi 3.

Vichambuzi vikaipa Simba kichwa kuwa Ina muunganiko, Iko vizuri, inacheza vizuri, Sakho, Sakho Sakho Banda Banda kanoute wachezaji wamezoeana hadi Gomez na Mwamed wakapata kichwa.

Vichambuzi vyetu na hata Gomez walikuwa hawausemi ubaya wa kukosekana kwa Chama na Miquissone kwenye kikosi Cha Simba kuwa ni tatizo. Wanasema Sakho na Banda na kanoute wameyaficha mapengo ya Chama na miquissone,, thubuuuuutu!!!! Wale jamaa ndio waliokuwa wakiamua Simba ifungwe na kufunga ngapi kwenye mechi.
Jamaa MJINGA kweli yule
Juzi alkuja na moja eti anamuona MSHAMBULIAJI wa Simba kaondoka na MPIRA sijui kaupata wapi...
 
Kuna Mwingine yuko Yale magazeti ya Udaku ya GLOBAL sijui,nina uhakika leo hatoamka ana kakipindi kake online.

Kosa wanalolifanya kama wao ni wana habari watumie Vyombo na taaluma yao wakiwa NEUTRAL

Kama wanataka kuegemea upande mmoja wajitoe kwenye tasnia ya Habari wawe Mashabiki kama sisi tuchambane.
 
Kuna yule mchambuzi wa wasafi anaitwa George Job, juzi eti amekaza misuli kabisa eti kwanini Yanga wamewarudisha Kaze na zahera

Anasahau kwamba zahera alishika nafasi ya pili kwenye msimamo wakati Yanga inapitisha mabakuli jukwaani kama ombaomba

Shida ya wachambuzi wengi wanaongozwa sana na mihemko yao

Let's take a look at Ally mayai japokuwa anafahamika ni yanga kabisa ila uchambuzi wake upo very clear without doubt, George Ambangile shout out kwake.
Sio kubeza TU kwanini Yanga imewarudisha Cedric na Zahera, bali alikuwa anawabeza pia Cedric na Zahera kurudi Yanga eti hawakuwa na Cha kufanya huko, huyu ni mchambuzi uchwara anayetaka kuingilia hata maisha ya wengine, anasahau kuwa mpira ni pesa na mpira ni ajira na furaha na mipango. Zahera anapenda Yanga, na Zahera anapenda kuishi Tanzania ndio maana alikwenda Gwambina ili aendelee kuishi Tanzania, anaipenda Tanzania. Cedric akiwa Tanzania ni kama vile Yuko Burundi, huwezi kujuwa kwanini amekubali kurudi Yanga na Tanzania tena.

Mkataba ndiyo kete ya mwisho kwenye ajira.
 
Akina nani hao mbwiga.
Wanaharibu mpira wetu, hawana weledi kabisa, yaani ni kama wahuni wanavyobishana kwenye vibanda umiza kuhusu mpira na kusahau kuwa wako nyuma ya mike na vipasa sauti. Unapokuwa unaongea na media lazima uwe neutral as much as possible, SEMA ukweli wote lakini bila kuongeza mahaba yako. Wanaotakiwa kuonyesha mahaba Yao kwenye chombo Cha habari ni viongozi wa timu; kamwaga, bumbuli, Bwire, kifaru kama watakaribishwa kwenye chombo Cha habari.
 
Wapi kuna chuo cha uchambuzi ndugu
Mkuu wachambuzi wa mpira huwa ni walio na elimu ya ukocha na wachezaji wa zamani

Hapa bongo kuna yule Dominick salamba ni kocha kabisa wa kusomea, ally mayai tembele ni mchezaji wa zamani tena wa viwango vikubwa hapa Tanzania, George Ambangile ni kocha wa kusomea
 
Sio kubeza TU kwanini Yanga imewarudisha Cedric na Zahera, bali alikuwa anawabeza pia Cedric na Zahera kurudi Yanga eti hawakuwa na Cha kufanya huko, huyu ni mchambuzi uchwara anayetaka kuingilia hata maisha ya wengine, anasahau kuwa mpira ni pesa na mpira ni ajira na furaha na mipango. Zahera anapenda Yanga, na Zahera anapenda kuishi Tanzania ndio maana alikwenda Gwambina ili aendelee kuishi Tanzania, anaipenda Tanzania. Cedric akiwa Tanzania ni kama vile Yuko Burundi, huwezi kujuwa kwanini amekubali kurudi Yanga na Tanzania tena.

Mkataba ndiyo kete ya mwisho kwenye ajira.
Waandishi Wa Habari Fulani Wako Kwenye Hizi Platform za Radio kutoa Machungu Yao Dhidi Ya Viongozi Wa Team Fulani.

Jemadari Kwa SSa Ana Hasira Na Yanga Kisa Yule Goli Kipa Wake Alitemwa ndio Maana anatema Sana Nyongo
 
Back
Top Bottom