Tuendeleee.......
So baada ya lile tukio zilipita kama siku 3 nilisafiri kidogo niliporudi nikakuta lile tangazo lipo lakini wimbo wamebadilisha wameweka mwingine nafikiri ni wa diamond ule, sikuwaongelesha chochote kuhusu tangazo na kwanini wamebadilisha wimbo nikakaa kimya nikajiambia tu kwamba tayari wamegundua walipokosea.
Baada ya kama siku mbili jamaa akanifata akanambia kwamba aligundua kuwa wimbo haukuwa sawa ndomana kabadilisha, nikamwambia usiwaze tunajifunza kupitia makosa. Stors zikaishia hapo.
Baadae katika stors na utani jamaa wakaanza kuongea kwamba muda mwingi ushauri wangu huwa ni wamaana sana wakawa wanarefer matukio yalopita hasa haya mawili kuhusu kutongoza wateja hovyo na lile tangazo. (Sijisifii wadau lakini tunatofautiana katika kufikiria)
UNAFIKI WA JAMAAA YANGU.
Jamaa akaniuliza nimefikia wapi juu ya lile swala la kufungua frem huku ananicheka "aaaah pesa huna wewe unatokea wapi pesa ya frem unadhani ni kama nyanya"
Sasa nikawa simuelewi jamaa kwanini hasa ananikatisha tamaa kivile na madharau juu, of course kwa mtaji alonao jamaa ni mkubwa kwasasa kunizidi mimi kwasababu hata mafingasho yake ni heavyweight. Lakini nachoamini kwenye biashara ukiwa makini mauzo yako ukawa unayarudisha dukani chapu wewe kujaza mzigo ni fasta tofauti na mtu anayejiuliza sjui hii niweke huku na hii ndo nifungashe.
Jamaa wakawa wananicheka pesa huna kufungua frem huwez wewe endelea kutuuzia sisi tu jichange baadae ndo ufungue.
Nikawa najisemea mwenyewe tu kwamba hakuna kinachoshindikana na hawawezi kujua namiliki tupesa twa kiasi gani hata kama ni tudogo ukilinganiaha na wao japo boss ni mmoja wengine wa2 ni wadogo zake tu.
Huwa nina mentality moja na naomba hata wewe msomoja nikupe "say gud and huge wishes about/to yourself". Huwa nina imani kwamba mimi sijawahi kushindwa kitu tangu nimezaliwa na siyo kwamba sijawahi kushindwa kweli hapana ila sijawahi kushindwa kwasababu huwa sichoki kuanza upya kitu ambacho mwanzo nilishindwa na mwisho wa siku najikuta nakuwa mshindi.
Kwahiyo maneno na vituko vya jamaa zangu havikuwa vinaniteteresha hata kidogo ila huwa nikiwaangalia nawaona kabisa ni swala la muda tutaheshimiana kwasababu kiakili bado niwachanga tu.
Nilivoona wananikatisha tamaa nikaona niache kuwashirikisha mambo yangu nyeti hii ndo hatua ya kwanza niloichukua.
Then nikaanza mdogo mdogo kutafuta frem kimya kimya.
Sasa siku moja nilishangaa sana, huyu jamaa yangu aliniuliza tena kuhusu frem, then akaongezea na kusema "kwahyo unataka ufungue ili utukimbize sio?"
Hii kauli ndo nilikuwa naisubiri kwasababu ilinithibitishia kwamba mimi ni mshindi ndomana wanaogopa na kunikatisha tamaa nisifungue frem. Baada ya hapo nikaongeza umakini nilipokuwa nao karibu, sikuruhusu washike cm yangu nilibadilisha passwords.
Nitawambia kwanini nilibadilisha passwords na kwanini sikutaka washike simu yangu.
Seee you..........