Nimeamka saa 10 alfajiri na kusonga Ugali

Nimeamka saa 10 alfajiri na kusonga Ugali

Watakuona ukisonga na baadae ukila uku wao wakitoa miayo kwa ubao kutokana na aibu yao ya kulirusha asubuhi
 
Mbona kawaida tu. Tunaoendaga mnadani tunajua uzuri wa kula ugali asubuhi.
 
Majirani zako wala hawana muda na wewe punguza kujishtukia
 
Mbona safi tu

Kwa wenzetu wazambia ugali mapema tu mezani huo ndiyo utamaduni wao

Ova
 
Kawaida sana hiyo Mkuu.

Mimi ilikuwa ni kila siku naamka saa 11 asubuhi napika ugali na dagaa nahakikisha mpaka 12 asubuhi nimeshakula na saa 1 naingia kwenye mishe mishe.
 
Chipsi, wali, mikate, tambi ni vyakula vya kike (laini), Me rijali ambaye hana matatizo ya akili hula chipsi dume (mihogo) au ugali dona.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
Inatagemea unakula na nini. Kama ni ule ulaji wa kiswahili, mboga inawekwa kwenye kifuniko cha soda ule na mkate basi ni lazima utasikia njaa.
 
Mbona safi tu

Kwa wenzetu wazambia ugali mapema tu mezani huo ndiyo utamaduni wao

Ova
Kuna kipindi tulitembelewa na mama mmoja mjazito. Alikuwa anaamka saa 10 usiku kusonga ugali na matembele eti mimba ilikuwa inapenda hiki chakula.
 
Back
Top Bottom