Nimeamua kuharibu mwili Ili nipate pesa

Hiyo title ya uzi wako ina ukakasi sana, ungejaribu kuiweka sawa kabla vijana wa hovyo hawajaanza mijineno yao.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mpo wapi huko pa siko na mashine za kupandisha zege juu
 
Hatari Danger!
 
Kaka nimekuelewa sana kuwa hutaki ushauri ila unapoona mtu anaelekea kuumia lazima uzibe masikio kidogo.

1. Unaposema "afya ni uhai" ni ujinga tuu, hizo hela unazo tengeneza huta enjoy utakuja kutumia kujitibu badae
2. Mzee hizo energy drink tumia kwa kiasi, usifanye sifa utakuja pata magonjwa ya moyo
3. Mzee mwili ukichoka umechoka, mwili ukifika limit unatakiwa kupumzika sasa ww ukitumia hizo pain killer zina addiction mbaya sana, ukitumia sana mwili utadhoofika utakuwa kila siku inabidi utumie ili usisikie uchovu, yatakuua mzee hayo madawa.
4. Ukichanganya pain killer na energy drink ini lako litafeli au utakuja kupata magonjwa ya ini.

Najua maisha ni magumu alaf una madeni ila usije fanya ndo sababu ya kujiua, maana hayo mambo uliyosema ukiyafanya kweli utaishi kwa tabu sana badae, utajuta mzee, hizo hela utatumia kujitibu ukiwa umelazwa.

Ushauri wangu, ukichoka pumzika vizur, usiku pata muda mwingi wa kulala, tumia sana ndizi na parachichi, kunywa maji mengi na muombe sana mungu, nguvu unazohitaji zitakuja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…