Sirdirashy
JF-Expert Member
- Jan 26, 2014
- 3,243
- 3,047
Pole mkuu ila usifike huko ila fata haya.Sijui kwanini Mungu aliruhusu wachawi wawepo, sisi home watoto wa kiume tunapita nyakati ngumu sana.
Kuna muda mara kadhaa nishajiuliza kama "Mungu yupo kweli" na anaruhusu haya. Watu wa dini mtasema nimetenda dhambi,ila no inabidi kuhoji kwakweli.
Halafu wanaoenda kwa waganga ni kama wanafanikiwa, ukimlilia Mungu unakuta huoni chochote.
1. Kama unaishi kwenye nyumba ya mzee au mnaishi nyumba ya mzee hameni na pangisheni.
2. Kama mna mali za mzee mnadeal nazo moja kwa moja km mashamba mnalima halikadhalika acheni kodisheni.
3. Kama unaishi karibu na hao ndugu jaribu kuwa mbali nao namaanisha mama mkubwa na mwanae.
Kwann nimekwambia hayo sababu ni hizi.
1. Ni rahisi kuja mnapoishi nakuacha athari.
Hakuna athari kubwa km mchawi kujua unapoishi aidha atatuma mtu, au yy kuja nawanaweka vitu chooni, nje au kuviacha anapokuja
2. Kama mna mali mnadeal nazo mojakwamoja achaneni nazo kwa sababu zinamaagano zitumieni indirect km kupangisha mjipatie riziki.
3. Than kaeni mbali nao japo mchawi anapiga popote na kwa umbali wowote lkn ukiwa mbali nae athari zake huwa afifu sana.
La mwisho:
Usikate tamaa wala kumkufuru Mola wako nahangaikeni popote ili mpate nafuu usijikite kwenye kuingia kwenye uchawi kwani huko ndo utaangamiza zaidi ndugu zako kwa mikono yako.