Nimeamua kujishusha na kufungua biashara ya mkaa

Nimeamua kujishusha na kufungua biashara ya mkaa

Gien Banks

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
336
Reaction score
887
Poleni na mapambano ndugu wana JF

Husika na kichwa cha habari

Katika pita pita zangu za hapa na pale wakuu nimeona nifanye biashara ya mkaa (ni wazo ila niko finishing stages ni execute idea)

Yani ninunue kwa wanaoleta mkaa mjini kwa jumla. Magunia kadhaa niyachane na kuuza reja na jumla maeneo ya makazi ya watu.

Sababu zangu ni hizi:

1. Mkaa hauozi utachelewa kutoka ila utaisha

2. Unahesabika yani hesabu zake za biashara kdgo ni rahisi sio pasua kichwa

3. Kwa mtazamo wangu bado soko lipo japo changamoto za majiko ya gas.

4. Eneo la biashara ni kijitonyama / karibu na sinza

Nimewekeza sehem nyingi sana biashara ambazo ni classy and so called za kisomi ila hamna maajabu yeyote zaidi ya hasara na mtaji kukata. Unatoa mfuko wa kushoto ili kujazilizia mfuko wa kulia ilhali mfuko wa kulia una tundu umetoboka. So ndio hivyo wandugu.

Nakaribisha ushauri / maoni / kukosolewa / kuboreshwa wazo na mtazamo wa hyo biashara husika.

Ahsanteni na mbarikiwe 🤝
 
Mali Asili wanasemaje? Una vibali? Binafsi Sielewi ila kuna muuza mkaa mmoja nilikuwa namuona anauza kwa kujificha ficha sijui tatizo lilikuwa nini (Huenda ukilipa tozo zote kama inavyotakiwa unaweza kujikuta unafanya kazi ya Kanisa) Hio ni assumption sina uhakika as well as kuna kuuziwa mkaa mbaya.
 
Mali Asili wanasemaje ?, Una Vibali ? Binafsi Sielewi ila kuna muuza mkaa mmoja nilikuwa namuona anauza kwa kujificha ficha sijui tatizo lilikuwa nini (Huenda ukilipa tozo zote kama inavyotakiwa unaweza kujikuta unafanya kazi ya Kanisa) Hio ni assumption sina uhakika, as well as kuna kuuziwa mkaa mbaya.
Sihitaji vibali cz nanunua kwa wanaoleta mjini, mimi ni kuuza jumla na reja kwenye goli nilio plan kuuzia. Vibali hao wanaoleta ndio watakata. (If I’m Being Right Tho)
 
Ni biashara nzuri. ILA imejaa sana Rushwa.wakati mwingine ukienda kihalali ndiyo unazidi kuwekewa mazingira magumu zaidi

Iko hiv.katika kila wilaya kuna ofisi za misitu za Wilaya na TFS,nenda ukapate maelekezo na ujue aina ya vibari pamoja na leseni yake pamoja ushuru wa wake.

Kumbuka sheria zake ni kali sana ukikiuka na ukaingia kwenye 18 zao unaweza ukapoteza mtaji pamoja na kufungwa.

Wale jamaa kule kwenye yale mageti yao unaona wamekaa wanafanana na mkaa pamoja na viofis vyao vichafuchafu hivi ila wako very powerful na wengine na mamilionea kwa fedha za rushwa
 
Ni biashara nzuri.ILA imejaa sana Rushwa.wakati mwingine ukienda kihalali ndiyo unazidi kuwekewa mazingira magumu zaidi

Iko hiv.katika kila wilaya kuna ofisi za misitu za Wilaya na TFS,nenda ukapate maelekezo na ujue aina ya vibari pamoja na leseni yake pamoja ushuru wa wake.
Kumbuka sheria zake ni kali sana ukikiuka na ukaingia kwenye 18 zao unaweza ukapoteza mtaji pamoja na kufungwa.

Wale jamaa kule kwenye yale mageti yao unaona wamekaa wanafanana na mkaa pamoja na viofis vyao vichafuchafu hivi ila wako very powerful na wengine na mamilionea kwa fedha za rushwa

Noma Sanaaa aisee. Nimelipokea kwa mikono miwili. Ubarikiwe Sana.
 
Acha tu ndugu yangu. Nisamehe lakini. Hilo neno kujishusha acha niseme hivyo maana nimepitia mengi. Daah
Ndo maana wengine unaonekana kila sehemu umegusa lol all the best karibu duniani thou😀😀!

Ila sio biashara endelevu. Supplier wako akipigwa pin ndo ntolee! (nahisi tu )
 
Sihitaji vibali cz nanunua kwa wanaoleta mjini....mimi ni kuuza jumla na reja kwenye goli nilio plan kuuzia. Vibali hao wanaoleta ndio watakata. (If I’m Being Right Tho)
Kubali lazima hata kama unauza rejereja, fuata taratibu utalia siku si nyingi. Utashusha mzigo alafu jamaa nao wanafika unabebwa wewe na mkaa wako, kubali cha rejjareja nadhani ni laki na nusu ofisi za maliasili wilaya husika
 
Ukiwa na gunia zako zisizozidi 5 wala maliasili hawahangaiki na wewe,siku hizi watu wanachofanya wanaweka mkaa mwingi kwenye stoo (chimbo) wewe unakuwa na gunia zako chache za kuuza ukiisha unasogeza,hapo unakuwa umejiepusha na kuombwa rushwa na kutoa laki 2 na 61 ya vibali vya maliasili.KUWEKA GUNIA 100 KIJIWENI HIYO ILISHAPITWA NA WAKATI SIKU HIZI
 
Sihitaji vibali cz nanunua kwa wanaoleta mjini....mimi ni kuuza jumla na reja kwenye goli nilio plan kuuzia. Vibali hao wanaoleta ndio watakata. (If I’m Being Right Tho)
Labda ununue gunia moja then ukimaliza ununue tena lakini tofauti na hivyo utakamatwa na kutakiwa uoneshe kibali Cha store ya kuhifadhi mkaa
 
Ukiwa na gunia zako zisizozidi 5 wala maliasili hawahangaiki na wewe,siku hizi watu wanachofanya wanaweka mkaa mwingi kwenye stoo (chimbo) wewe unakuwa na gunia zako chache za kuuza ukiisha unasogeza,hapo unakuwa umejiepusha na kuombwa rushwa na kutoa laki 2 na 61 ya vibali vya maliasili.KUWEKA GUNIA 100 KIJIWENI HIYO ILISHAPITWA NA WAKATI SIKU HIZI
Labda kwa huko DAR lakini SI kwa Dodoma mkuu
 
Last time ulisema unafikiria kufanya mishe za gari used...je iliishiaje
Ile haikuwezekana eneo halijakaa fresh alaf its risky (kupata magari sahihi yaliyo legit) well it needs capital ku set mazingira fresh na ujenzi. So its kind of a pending business.
 
Labda kwa huko DAR lakini SI kwa Dodoma mkuu
Ndio kwa Dar huwa wanasumbuliwa na kutakiwa wawe na vibali wale wenye kuleta mzigo mkubwa, Ila kwa wale wenye store za uswahilin wenye kuuza rejaraja na kwa jumla huwa hawasumbuliwi.
 
Back
Top Bottom