Nimeamua Kukopa Bank

HahahHa, itakua siyo maximum , sisi wengine tumeshindwa kuchukua mkopo kabisa kwa rate hiyo ya salary,
Mtaani kwetu kuna nyumba 5 zimepigwa mnada huku naona ,
Nyumba yangu mdogo mdogo nitamalizia kwa salary hii hii 1+
Kwani ukikopa hela benki kwa udhamini wa muajiri wako Kuna ulazima wa kuweka nyumba rehani?kampuni si ndio inakudhamini,au siku hizi wamebadilisha utaratibu?
 
Mkuu umeshaezeka? 6m ni gharama ya kuezeka tu iyo. Hebu fanya rouph estimation
Hata mimi nilitaka kushangaa maana kuna pagale langu lina miezi kama sita sijafanikiwa kupaua na fundi alinipigia gharama za kupaua ilifika m5.7
 
Boss kukopa halaf ukajenge sikushauri kabisa.. Maana unaenda zika fedha..


Ni bora hiyo fedha 5 M fanya biashara hiyo ya mazao lakini Angalizo kuwa makini na zao lipi unataka kununua, mwaka huu kanda ya ziwa mpunga ni mchache-so hii ni fursa..

Ila mahindi usipoteze fedha yako..

Balance nyingine walau Mil 3 iweke fixed diposit huku ukiisoma biashara yako, na hiyo inakuww kama Back Up yako..

Muhimu, biashara ifanye mwenyewe usitume mtu.
 
Kwani ukikopa hela benki kwa udhamini wa muajiri wako Kuna ulazima wa kuweka nyumba rehani?kampuni si ndio inakudhamini,au siku hizi wamebadilisha utaratibu?
Mimi nipo kampuni binafsi, kwa kampuni yetu hawaruhusu kuchukua mkopo bank mkuu, wao wanataka mkopo uchukue ndani ya kampuni na ndani ya miezi 6 hela yao iwe imerudi yote,
 
Iyo yako ikoje
Kiwanja changu ni tambarare,hakihitaji leveling, material 98% nishamwaga nje ya hii hela.
Maana yake hii hela itakua kulipa fundi na kununua ndondo na cement ambapo cement haizidi mifuko 20.
 
Kiwanja changu ni tambarare,hakihitaji leveling, material 98% nishamwaga nje ya hii hela.
Maana yake hii hela itakua kulipa fundi na kununua ndondo na cement ambapo cement haizidi mifuko 20.
Hebu nieleze iyo nyumba yako ina ukubwa gani. Matofali 60 unatumia mfuko 1. Kama cement hazizidi 20 maana yake 20x60=1200. Matofali 1200 iyo ni chumba, choo na jiko labda ndo vyaweza kutosha tena jiko, chumba na choo viwe vidogo sana. Apo hujafunga beam na mazaga zaga kibao. Inshort iyo hela ni ndogo sana kwenye ujenzi
 
Ninatumi burnt bricks mkuu,tofari 4000
 
Kwetu sisi hawaruhusu , ukitaka kopa hapa hapa lakini mkopo unapaswa kurejesha within 6 months, Mimi bado finishing tuu napambana na salary yangu
Huyu jamaa katupa chai hii...tena ya mchana..Kama ni taasisi Binafsi hawana mdhamana kwa wafanyakazi wao bank?
 
Uko sina utaalamu nako. Lakini nna uzowefu wa kutosha kwenye ujenzi. Na kila siku nafanya makisio. Mil 6 inakua ni kuezeka tu
Ni kweli mkuu, milioni 6 haiwezi kutosha kujenga nyumba. Ujenzi wa hali ya chini inabidi ijengwe kidogo kidogo hatua kwa hatua
 
Msomi achana na assumptions na ramli..

Fuatilia Bei za vitu uje na approximation iliyo sahihi ,Mungu amekupa akili ili usimsumbue kwa vitu vilivyo ndani ya uwezo wako....
 
Msomi achana na assumptions na ramli..

Fuatilia Bei za vitu uje na approximation iliyo sahihi ,Mungu amekupa akili ili usimsumbue kwa vitu vilivyo ndani ya uwezo wako....
Asante,But vitu vyote vy kisomi kuanza na assumption then zinakuja facts za kuprove wrong or right assumption
 
Sikishauri Sikushauri kuweka stock ya mahindi, bei yake haitabiriki bora mpunga au maharage.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…