Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hio we unaona elf 70 ni nyingi.kumbuka mahindi hubunguliwa kirahisi sana.Sehemu nitakayoweka stock kila mwaka ikifika Mwezi wa 12 gunia hufika 70
Nafanya kazi sekta binafsi kwa miaka mitano sasa.
Nimejitahidi kadiri ya uwezo wangu kwani kwa miaka hiyo nimeweza kujikamua na kujenga nyumbani(finishing bado) kijijini kwetu si mnajua life tuliokulia maisha ya kuunga unga? (Maisha ya home yalikua mabaya kupindukia,hadi namaliza chuo,njaa ilikua inachakaza nyumbani hadi inatishia kutoa uhai)
Pia kwa miaka mitano hii nimeoa na kujiunga na Msc degree na chuo flani hivi kikongwe hapa nchini,nimenunua ka plot ka kuanzia maisha na kusomba materials
Sasa kwa muda huu nimejikuta mambo yanakua mengi halafu na kipato hakitoshi japo kwa mwezi na take home ni M na kitu hivi.
Nimeona isiwe shida,nimeenda bank kukopa ili nijenge na kununua mahindi ya stock ili badae niuze kuanzia mwezi wa 11 hadi 3 hivi najua bei itakua imepanda kidogo
Sasa hapa nina wasiwasi na hii hela km itamaliza ujenzi,site nilileta material almost 98% (yaani tofari,mawe,mchanga na kokoto).Hela niliyoomba ni 9M nakata 2M ziingie kununua nafaka niweke stock, 1M iingie matumizi ya kawaida (msishangae serikali yetu matumizi ya kawaida ni zaidi ya nusu ya bajeti) halafu 6M zipige ujenzi je zitatosha?
Hapa nasali na kuomba angalau hii hela itoshe