Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

habari
zenu wapendwa,nimekuwa na shauku ya kulima mahindi kama robo heka kwa njia ya umwagiliji wa kutumia maji ya bomba lakini sifahamu namna ya
umwagiliaji wa mahindi unavo kuwa naomba kujuzwa huu utalaamu kwa yeyote anayefahamu, kilimo hiki nataka kufanyia Dodoma.
 
All da best mkuu wanahitajika vijana wengi kama wew kwani huu msingi tungekuwa nao kipindi tangu tunasoma juu ya kujiajili leo hii wasingekuwepo watu wakihangaika mtaani kutafuta ajira big up sanaaa bro
 
Kaka tupo pamoja, mimi nimeanza mwaka huu na ekari 20 kwanza, mwakan napanda na 50, pia nimejaribu na mpunga kidogo ndo twasubili mavuno sasa 2kitegemea mshahara utatuumbua mwisho wa siku kama wasemavyo waswahili

FAINALI UZEENI!
 
 
Ehh Kaka hebu tupe ripoti ndugu yetu mambo yalikuwaje? pia kwa sasa huko shambani kwako mambo yakoje yaani bei za kununua shamba zikoje kwa hekta maana hata mm najisikia sana kuingia katika kilimo.

Hope all is well with you.
 
Huu ni ukweli na cha kushangaza mtu akiwa na kimasters chake ukimtajia hela (kilimo) anaona hawezi.

Anapenda akae ofisini alipwe 3.5 Gross halafu awe ana mkopo wa kigari kama LAV4. Baada ya hapo majungu tu fulani ni fisadi fulani ni mwizi. Basi.

Huku watu wenye akilili wakipiga hela. Hongera sana bro.

This is great idea
 
Hongera maskn jeur utafka 2 mkuu mungu abariki kazi ya mikono yako
 
Umenifurahisha sana sana asubuhi hii, vijana kama nyie ndio wanatakiwa katika maisha ya sasa,nakutakia mafanikio mema in every step ya biashara yako nzuri. brilliant vision
 
Nimeanza na biashara ya kununua mazao mwaka huu huko mkoani Njombe yaani maharage ,mahindi na alizeti, mfano kwa sasa mahindi debe ni elfu tano, nimeweza kutumia muda finyu nilionao kufanya organization nzima ya ununuzi, nina mpango wakusafirisha na kufungua store yangu mwenyewe dar na kuuza mwenyewe.

Pia nimelima kidogo mwaka huu huko mkoani lkn 2014 nitaingia rasmi kwenye kilimo cha mahindi, alizeti na maharage. Siku hizi wadau unaweza ukapulizia dawa za kuua magugu mara baada ya kupanda ili magugu yasiote hivyo kupunguza tatizo la kusumbuana na vibarua.

Pi hapo hapo nitaendelea kununua hayo mazao pia
 

harverster tunashukuru kwa taarifa. hope utaendelea kutupa update kadri mambo yanavyoendelea. mimi ni mmoja ya watu ninaoamini kwenye kushare taarifa sahihi kwa wengine zenye nia ya kuwafungua macho na kuwachallenge.

Kuna wadau humu tulikubaliana mpaka kutembelea kwenye maeneo yao ya kilimo bahati mbaya wamepotea, soko la bidhaa ni kubwa sana sidhani kama ukishare na mwingine then atakupiku kwenye biashara yako kwani riziki anatoa maanani.
 
ELNINO
hongera sana kwa kuamua kujiendeleza kupitia kilimo ni uamuzi wa busara sana...BIG UP

Mi pia ninalima sana nipo wilayani babati mkoa wa manyara napia ninaendesha blog inayojihushana maswala ya kilimo tu (Agribusines) kwa msingi huu ningependa nipate mawasiliano na wewe ili tuweze kushirikiane ktk mambo mbalimbali ya kilimo lkn pia naana magazine ya kilimo hivyo nataka nikufanyie inteview ili juhudi zako zifahamike kwa vijana walio wengi na ikibidi wafuate njia unayoitumia wewe.

Tuwasiliane tafadhali mengi tuapeana huko, simu ni 0714020714 email ni drabainc@yahoo.com pia kwa kutumia hiyo email unaweza kunitafuta ktk facebook...

Nakutakia mafanikio mema
johnson
 

nimependa hii, sasa mkuu nielekeze, hiyo runnig cost ni kwa production tu au na kukodia mashamba?
 
Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50.

Hivi hii average ya hekari 1 kwa gunia 30 mmmmh naona mahesabu yako yalikwua too optimistic hapa.

Lakini umesaidia sana kutufumbua macho na sisi wengine ndio tunasubiri kuvuna mahindi sasa kutokana na post yako hii ila sasa hayo makadirio ni tofauti kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…