Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Hongera kwa jitihada kaka, lakini hakikisha unatumia mbolea ili kuhakikisha mavuno hayo, pia spacing shambani ni jambo la msingi sana kwani mahindi unapaswa kuwa na mahindi 17000 kwa ekari. Bei ya mahindi msimu huu haijafika 50000 hapa tuliani hiyo pia isikufanye uchanganyikiwe. Tuwasiliane ukitaka ushauri wa kitaalamu zaidi


Dah ndg kama ndio unavyopiga hesabu kwenye kilimo namna hii,lazima ile kwako.......unless you have intensive management kuhakikisha katika kila hatua kila kila kitu kinafanyika ontime na kiwango muafaka.

Kwa uzoefu wangu mdogo niliopata,kama unataka kilimo kikutoe......uwe na maji ya uhakika,mbolea kwa kiwango inachotakiwa,madawa kwa wakati na kiasi kinachotakiwa,palizi kwa wakati vilevile.........kwani ukizemebea katika kimoja wapo basi tija hutoiona na inaweza kula kwako........in short tofauti na wengi tunavyofanya,weka watu,futailia ukiwa na shughuli zako nyingine kama kazi ya kuajiriwa.....kwakweli kilimo is a full time job if you real want to succeed......kwa mfani kilimo cha mboga moga ,huhitaji kila siku uwepo shambani na kukagua kila mmea,asubuhi unapoamka na jioni kabla hujamaliza siku.Kwani hii itakusaidia kujua kama kuna tatizo mapema na kulidhibiti.

Tatizo jingine ni watu wa kusimamia,chondechonde waswahili wanakwambia kazi/mali yako lazima uitolee macho hinhaa mda wote,hat kama mmeingia mkataba na msimamizi vizuri namna gani,kwa uzoefu nilioupata ni Watanzania wachache sana unaweza ukawaachia shughuli ya mtu kuisimamia wakafanya 100%.So being there most of the tym ni muhimu.

Kama unaweza wakati wa msimu hamkia shambani always?
 
Kwa binafsi yangu nimeyapenda mawazo na maamuzi yako ndugu kwani kutegemea ajira tu ni kuukubali utumwa vijana wenzangu ni muda sasa umefika wa kuacha kulalamikia serikali na ukosefu wa ajira tuwekeze katika kilimo endelevu, 'there is a market out there'
 
JF

Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa
mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10
years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.

Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara
wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha
kuwaachia wanangu.

Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza
kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji,
nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja
na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa
na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.

Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale
Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project
up to 1,000 in next 3 - 5 years.

Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata
gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia
average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m
by July this year.

Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.

Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa
miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh

By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na
nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe.
by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. Sasa ole
wenu mseme nimefanya ufisadi.

This is a challenge to you JF - hasa mnaopata less than 5m per month -
think twice and join me.

Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata
shambani
- huu ni wosia.
uko vizur,all ze best
 
Wakuu wa JF nifungueni macho kwa uzoefu mlionao juu ya kilimo cha mahindi ya biashara (kuyauza yakiwa mabichi kwa ajili ya kuchoma) ili kuongeza kipato, maeneo ya Pwani.

Naomba ushauri kwa mwenye uzoefu na hii mambo
 
Nakupongeza sana kwa kulima mahindi kibiashara! Nakupa mchango wangu wa mawazo kiujumla tu maana haijulikani kwa usahihi ni eneo lipi linalokutatiza, je ni shambani au sokoni!

Kilimo cha biashara lazima uanzie kwanza sokoni ili ujue mapema soko likoje. Lijue kwanza soko lako ulilolenga iwapo ni wanunuzi wa jumla au wachomaji wenyewe au utachoma mwenyewe?

Fika hapo sokoni ufanye utafiti kutoka kwa wateja tofauti tofauti ili kutambua masuala yafuatayo
  1. Bei zinavyobadilika ili kujua msimu wenye faida zaidi
  2. Misimu mizuri na mibaya ya biashara ya kuchoma
  3. Aina ya mahindi yanayopendwa na wateja na ubora wake unaotakiwa sokoni
  4. Gharama za kusafirisha mahindi yako na urahisi wa kupata usafiri,
  5. Tambua wasafirishaji kadhaa na wakupe namba ya simu zao kwa kuendelea kuwasiliana
  6. Faida na hasara kuuza kwa kutumia dalali au moja kwa moja kwa wachomaji.
  7. Tambua wanunuzi wako watarajiwa na uanze mawasiliano nao na pengine upate namba zao za simu.
  8. Fika pia kwenye maduka ya pembejeo ulizia bei za mbegu, aina ya mbegu zilizopo, aina na bei ya mbolea na madawa yanayohitajika na gharama za kusafirisha

Taarifa za sokoni zitakufanya uamue jinsi ya kujipanga shambani ili kulima kwa uhakika kulingana na soko linavyotaka kwa faida zaidi na kwa uhakika zaidi. Hata hivyo mambo mengi mengine utayajua kazini kupitia hasara na vikwazo utakavyovipata, mambo ya hasara hayo yapo wala usihofu maana ukianzisha ujasiria mali wowote hatua za mwanzo huwa ni darasa kwako, utapiga mieleka tu kama siyo shambani basi sokoni lakini hatimae utakuwa BINGWA! Kwa hiyo hata kama unamtaji mkubwa anza kidogo kidogo yaani kama robo au theluthi ya mtaji wako upate darasa kwanza, au la ukipenda piga ki-mexico ingia mzima mzima ukitoka umetoka, na ukianguka unapotea kabisa kwenye ramani ya shamba na unajisikia kichefuchefu kabisa ukitajiwa mambo ya kilimo!

Kama unahitaji mambo ya utunzaji mahindi shambani weka wazi! Na wengine wataboresha zaidi!!

Mniwie radhi kwa kuwachosha kwa maelezo marefu maana mimi nami sinaga dogo jamani mweee!! Heshima sana kwenu MALILA na El Nino popote pale mlipo you are my heros!, you inspired me to come here!!
 
JF
Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.
Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.

Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.

Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.

Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m by July this year.

Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.

Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh

By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe. by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. Sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.

This is a challenge to you JF - hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.

Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.
umenena tatzo mtaji ndo unasumbua
 
Hongera mkuu penye nia pana njia, mie mwenyewe ipo siku nitarudi kwenye kilimo kwanza maana niliwahi kujaribu nikala loss kwa kuwa nilikuwa nategemea mvua, kikubwa ni kukomaa hasa palizi ya kwanza na ya pili hakikisha unasimamia palizi maana ukichemsha hapo utavuna mabua. Pia usikate tamaa hata kama hutopata kile ambacho umekusudia jaribu tena msimu mwingine. Mie mwenyewe najipanga mkuu ipo siku nitarudi tena kwenye kilimo kwanza maana kiukweli kilimo ukikichukulia serious kinalipa na uzuri unaweza fanya kazi za kilimo huku unafanya kazi nyingine
Bro umenichekesha sana, kumbe ulienda kwenye kilimo kujaribu??? Next time ukirud, usijaribu bali nenda kalime, yaani uingie kwenye kilimo full fledged. Hakuna investment yoyote ukaifanya kwa kujaribu then ukatoka. Ukienda kwa lengo la kujaribu hutokuwa committed kama ukenda kwa lengo la kujikita.

Na ndio maana kuwa muajiriwa sehemu na huku unafanya business kuna posibility ndogo sana ya kutoka maana ideally wewe unaamini zaid kwenye ajira yako kuliko kwenye business yako. So hata msimamiz wako pia naye anaamin kuwa wewe (boss) hutegemei sana kitega uchumi chako bali unategemea zaid kazi. So atakuhujumu tu na tegemea kuvuna mabua. Ukitaka umpe shares huyo msimamiz na sio umuajiri na kumlipa kila mwisho wa mwezi.


Ila kama mfanyakazi, upo serious na kilimo kama huyu aliyelima heka 50, omba likizo bila malipo just for one year, nenda kakurupushe pori lako huko kijijin, spend your full time there kuanzia mwanzo wa kilimo had mwisho wa mavuno. Wallah naapa kazini wewe hurudi tena maana ndani ya huo mwaka mmoja utashika hela ambayo hukuwah kushika toka umeanza kazi.
 
Naomba kuuliza pia Kilimo cha viungo kama Tangawizi, Vitunguu na vitunguu swaumu ni wapi vinastawi? maana jamani vuitunguu vimepanda sana bei. Tulikuwa tunanunua kilo sh 700 sasa hivi eti inafika 1500.
Kwa mkulima mpya nisingekushauri uanze na succulent plants kama vitunguu maana ndio target kubwa ya vimelea vya magonjwa. Unaweza kukiona kilimo kibaya kumbe ni wewe mwenyewe ndo umefanya wrong choice ya nini uanze nacho. Kupambana na hivi vijidudu ni very costful kuliko kutumia muda wako kusimamia palizi katika mahindi na mpunga au katika kunnua mbolea za kuweka kwenye shamba la mahindi or mpunga. Nashauri mkulima mgeni aanzia kwenye mahind ili akuze kwanza mtaji wake.

Kuhusu kukodi shamba au kunnua, nadhan inategemea sana na how beautifully the farm is located. Kama shamba la kukodi lipo karibu na mto kiasi kwamba litapermit kilimo cha umwagiliaji pale mvua zitapogoma, then you better hire it. Kama unauziwa shamba pembeni ya mto unaoflow permanently, dont waste time buy it, thats Jewelry.

Pia nimeona post moja unasema ulipoona hii thread ulihamasika ukaenda vamia pori na kuanza mchakato wa kilimo kwa kupunguza visiki ila mwisho EL alipochemsha na wewe uvunjika moyo. Well, ni sahihi kutake actions immediately, ila nadhan ulitakiwa kufikiria kwa kina, then ucreate belief kuwa hii project inatoa na mwisho ndo utake actions, maana kama hujapita hatua hizo, unaweza ukawa unainvest resources huku unasita. Ikishakuwa hivyo kaka hutoboi. Ni lazma kabla hujainvest uwe umeshafanya uchunguzi wa kina. Na ni lazma ujihaminishe kuwa kutoka ni PIE.

Usiinvest kwa mentality ya kujaribu, hutoboi. Usiinvest kwa kuwa flan kainvest huko, wewe create cultivate interest, develop strong belief then take actions kwa kufwata ushauri wa kitaalam, uliza role models huko na pata elimu juu ya kilimo husika in a nutshell, google offers an excellent material and plenty of lessons in every agricultural crops you wish to cultivate. Utabuild your capacity na utaweza kufanya rational decisions.

Kuhusu kutegemea au kutotegemea mvua hili linategemea sana na mkoa unaolima. Mikoa kama Mbeya, Rukwa, Ruvuma, Kigoma kwa kweli huko bado suala la mvua sio issue.Kama mkulima unayeanza unaweza ukaitumia mvua hii hii na ikakutoa had ukapata mtaji wa kunnua pump na hata Tractor. Ila km utataka kulima mkoa wa Pwani, kwa kweli usicheze mbali na mto na ufikirie zaid kilimo cha umwangiliaji.
 
Hivi nikisema najitolea kwenda kuishi kijijini kwa makubaliano kwamba nitakuwa MTIIFU kufanya kazi zote za usimamizi wa shamba kuanzia kuandaa
shamba mpaka kuvuna kwa makubaliano ya mimi kutumia nguvu,busara na hekima niliyopewa na Mungu na mtu mwingine ajitolee fedha,
ili kufanikisha hilo zoezi naweza kupata mtu wa kupiga naye kazi?

Makubaliano yanafanyika baada ya kila mmoja kiridhika na mwingine kwa kufahamu nyumbani na wazazi wa mwenziwe kama wapo, kisha sheria na taratibu nyingine kufuatwa.

Hili swala linawezekana?


Ila siyo kilimo cha hekari kumi au ishirini(isiwe chini ya hekari 50), hapa nazungumzia shamba la ukweli maana hiyo ndiyo itakuwa ajira yangu.
Yaana kifupi naachana kabisa na mambao ya mwisho wa mwezi.

Huyo mtu yupo?
Tiger hao watu wapo ila makesure naye anacommit resourcekwenye hiyo venture, malipo yenu yawe in terms of shares. Mtu wa kumuajiri hatokuwa anabehave tofauti na waajiriwa wengine. Ni tendency ya waajiriwa kumuibia muajiri not necessarily fedha bali hata kutokuperform to his/her full potential.

So as you want someone to share with make sure naye anacontribute significantly kwenye hiyo deal either in kind or financially. Kwa mfano unaweza share na mtu mbaye tayari ana ardhi kwa ajili ya hicho kilimo so wewe hutalazimika kutumia mtaji ulionao kwenye kukodi au kunnua ardhi.

Mimi pia natafuta mtu aliye kuwa committed kwenye kufanya business katika kilimo. Naamini sana kwenye kilimo kama njia nzuri na rahisi ya kututoa kwenye umaskini, we only need to have world class strategy kwenye kuapproach kilimo.
 
Nao ni mpango kabambe pia.........swali nikuwa utakimbizana nao hadi utapofikisha miaka 60?
Kwa kweli huyu kijana anatafuta uzee wa mahangaiko. Hawa ndo wazee wanaoishia kurandaranda mijini kwa watoto wao na kubugudhi wakwe zao. Anasahau haya maisha ya kudandadanda yana mwisho wake.

Anataka serikali imuwekee mazingira gani zaidi ya haya ili alidhike? Mbona watu wanatafuta visingizio visivyo na maana???Ukilinganisha na sekta nyingine, kilimo kimependelewa sana na kina fursa nyingi zaid kumtoa mwananchi aliyekuwa makini kwenye kilimo. Fursa kama mikopo ya Tractor na zana zingine, Fursa kama stakabadhi gharani kwa bulk producer, Mbolea za Ruzuku, High demand ya agricultural crops. Kwa kweli ukilaumu, we amua tu kulaumu ila kwa kweli utakuwa tu hujui unachotakiwa kufanya ili kupata fursa hizi.
 
Bro umenichekesha sana, kumbe ulienda kwenye kilimo kujaribu??? Next time ukirud, usijaribu bali nenda kalime, yaani uingie kwenye kilimo full fledged. Hakuna investment yoyote ukaifanya kwa kujaribu then ukatoka. Ukienda kwa lengo la kujaribu hutokuwa committed kama ukenda kwa lengo la kujikita.

Na ndio maana kuwa muajiriwa sehemu na huku unafanya business kuna posibility ndogo sana ya kutoka maana ideally wewe unaamini zaid kwenye ajira yako kuliko kwenye business yako. So hata msimamiz wako pia naye anaamin kuwa wewe (boss) hutegemei sana kitega uchumi chako bali unategemea zaid kazi. So atakuhujumu tu na tegemea kuvuna mabua. Ukitaka umpe shares huyo msimamiz na sio umuajiri na kumlipa kila mwisho wa mwezi.


Ila kama mfanyakazi, upo serious na kilimo kama huyu aliyelima heka 50, omba likizo bila malipo just for one year, nenda kakurupushe pori lako huko kijijin, spend your full time there kuanzia mwanzo wa kilimo had mwisho wa mavuno. Wallah naapa kazini wewe hurudi tena maana ndani ya huo mwaka mmoja utashika hela ambayo hukuwah kushika toka umeanza kazi.

Unavyoongea mkuu utadhani niliwahi kukusimulia maana nilitaka kufanyia kazi hiyo issue niliyo-bold (blue) baadae nikasema hapana nikawa na mshikaji mmoja tumekuwa nae street sasa kidogo mambo hayakuwa mambo hivyo kidume nikatafakari nikasema nikimuajiri sio poa bali ikabidi nifanyie kazi hilo wazo la kumpa share na kweli ikawa hivyo, sasa jamaa sijui aliingiwa na nini matokeo yake ufuatiliaji wake ukawa mdogo nikaja kugundua palizi ya kwanza aliipotezea na ndio maana nikasisitiza sana kuhusu kukomaa kwenye palizi hasa mahindi.

Kimsingi nimeita kujaribu baada ya kunikuta maana mshikaji tulishafanya nae issue kadhaa za fedha na alikuwa serious sasa sijui ikawaje akabadilika, anyway hata hivyo kuna kitu ambacho nilijifunza pindi nikirudi narudi full nikiwa kama mkurugenzi mtendaji na 70% ya kazi yote naifanya mwenyewe (nikiwa na maana kwenye zoezi la kupanda, kuweka mbolea, palizi lazima niwe around nashuhudia)
 
Unavyoongea mkuu utadhani niliwahi kukusimulia maana nilitaka kufanyia kazi hiyo issue niliyo-bold (blue) baadae nikasema hapana nikawa na mshikaji mmoja tumekuwa nae street sasa kidogo mambo hayakuwa mambo hivyo kidume nikatafakari nikasema nikimuajiri sio poa bali ikabidi nifanyie kazi hilo wazo la kumpa share na kweli ikawa hivyo, sasa jamaa sijui aliingiwa na nini matokeo yake ufuatiliaji wake ukawa mdogo nikaja kugundua palizi ya kwanza aliipotezea na ndio maana nikasisitiza sana kuhusu kukomaa kwenye palizi hasa mahindi.

Kimsingi nimeita kujaribu baada ya kunikuta maana mshikaji tulishafanya nae issue kadhaa za fedha na alikuwa serious sasa sijui ikawaje akabadilika, anyway hata hivyo kuna kitu ambacho nilijifunza pindi nikirudi narudi full nikiwa kama mkurugenzi mtendaji na 70% ya kazi yote naifanya mwenyewe (nikiwa na maana kwenye zoezi la kupanda, kuweka mbolea, palizi lazima niwe around nashuhudia)
Yah unajua mtu ambaye hachangii resources kwenye mradi flan ni rahisi sana kukutelekeza, ila kama naye atajua kuwa akizembea hela yake nayo imekwenda, nakwambia naye atakomaa hapo shambani. Mimi nadhan wazungu walishajifunzaga kuwa utaratibu wa kumkabidh mtu/ndugu akusimamie kaz yako co efficient, utaishia kutoa mlio tu.

Mimi pia nilishajaribu kama mwenzangu ulivyojaribu. Niliishia kuzika tu hela aisee. Its very rare one can get a person who is really committed. Ingawa inashauriwa usiwe na negative attitude on people if you want to get rich, nashauri uwe tu makin ktk kuchagua partner na pia wewe mwenyewe uwepo around hapo. Otherwise inakuwa ngumu sana kutoka.
 
Kaka ingawa hii post yako ya kitambo lakini imenivutia.VIpi uliweza kufanikiwa na hiyo proj yako?Nina vision ya kufanya agriculture next year so ningependa kupata mrejesho kutoka upande wako ili unisaidie kwenye planning.Info nyingine kuhusu aina ya mbegu ambazo ni best kwa mahindi,current prices za mashamba rural areas,wadudu umedeal nao vipi,sokoni umeingizaje na kuuzaje bidhaa etc...inshort all important details ambazo waweza nipatia kutokana na exp yako zitanisaidia sana kaka.

Wana JF,i need your assistance on this too



"Right thinking comes when you digest the right things"
 
although itz too long tym passed since u wrote diz post,i must congratulate u 4 such a wise dicision am with u.
 
Back
Top Bottom