Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Kwa mtizamo tu ni miundo mbinu ya gharama kiasi gani ukitaka kumwagilia shamba la ekari 45...........hii ikiwa ni pamoja na kuchimba kisima.........nahitaji vifaa gani na natakiwa kuwa na akiba ya maji kiasi gani kujihakiishia uzalishaji wa mwaka mzima?

Kuna katabia toka maliasili,kameanza kufanya kazi vijijini.

Ukichepusha maji kwa mfereji toka mtoni, wanatoza kodi, halafu zile nyanya/vitunguu/mahindi utakayovuna kutokana na umwagiliaji huo ukipeleka sokoni wanatoza kodi. Hata ukichimba kisima, wanatoza kodi.

Sijui mkulima mdogo kama atatoka kwa mtindo huu.
 
Kwa mtizamo tu ni miundo mbinu ya gharama kiasi gani ukitaka kumwagilia shamba la ekari 45...........hii ikiwa ni pamoja na kuchimba kisima.........nahitaji vifaa gani na natakiwa kuwa na akiba ya maji kiasi gani kujihakiishia uzalishaji wa mwaka mzima?

Utahitaji kuchimba kisima kirefu (kadiria 5m), iwapo kuna mto karibu unaweza kuokoa gharama katika hili vilevile mashine (pampu) na mabomba ya plastic (low grade) kusambazia, inakuwa rahisi ukiwa na tanki sehemu ya mwinuko ili maji yaende kwa gravity (kadiria 3m - 5m), ukimpata fundi mchundo aliyekaribu na shamba lako anaweza kushauri vizuri kwa kutembelea eneo husika (ulizia Idara ya Maji wilayani utawapata).

Kumbuka lengo hapa ni kuziba pengo la kipindi kifupi ambapo mvua zinachelewa au kukatika katikati ya msimu, hivyo basi mtandao wa mabomba shambani si wa kudumu bali katika hali ambayo unaweza kuweka na kuhamisha.

Kumbuka gharama za uendeshaji; umeme au diesel/petrol, hapa nilipo serikali yao inaweka ruzuku kwenye diesel ya mashambani.
 
Utahitaji kuchimba kisima kirefu (kadiria 5m), iwapo kuna mto karibu unaweza kuokoa gharama katika hili vilevile mashine (pampu) na mabomba ya plastic (low grade) kusambazia, inakuwa rahisi ukiwa na tanki sehemu ya mwinuko ili maji yaende kwa gravity (kadiria 3m - 5m), ukimpata fundi mchundo aliyekaribu na shamba lako anaweza kushauri vizuri kwa kutembelea eneo husika (ulizia Idara ya Maji wilayani utawapata).
Kumbuka lengo hapa ni kuziba pengo la kipindi kifupi ambapo mvua zinachelewa au kukatika katikati ya msimu, hivyo basi mtandao wa mabomba shambani si wa kudumu bali katika hali ambayo unaweza kuweka na kuhamisha. Kumbuka gharama za uendeshaji; umeme au diesel/petrol, hapa nilipo serikali yao inaweka ruzuku kwenye diesel ya mashambani.

Asante sana Kalende,

Eneo langu lina maji kwani yari kuna kisima kidogo cha kuchimbwa na jembe na nia yangu ilikuwa kuendesha kilimo cha kiangazi; cjha kumawagilia muda wote na nisizitegemee mvua kabisa isipokuwa kwa mazao machache ya msimu........hivyo nahitaji miundombinu ya kudumu unaweza kuni rough idea.........pia kuna mwinuko kiasi kwnye kingo moja wapo ya shamba ambayo ukipima mpaka pembe nyingine ni karibu m1 na nusu
 
Jamani nikitaka shamba la kukodisha napata wapi wanabodi? sehemu yenye rutuba ya kutosha na miundo mbinu, na je inagharimu kiasi gani kwa hekari moja?
 
Jamani nikitaka shamba la kukodisha napata wapi wanabodi? sehemu yenye rutuba ya kutosha na miundo mbinu, na je inagharimu kiasi gani kwa hekari moja?

Kwa mkoa wa Dodoma rates za kukodi ni kuanzia elfu 15 mpaka 25 kwa ekari,

Mbeya eneo la mbarali naambiwa inafika hadi laki 2 kwa ekari

baadhi ya sehemu za mvomero ni elfu 45 kwa ekari...............wadau wengine watakupa bei kwa maeneo yao lakini hujasema unataka kulima nini
 
Jamani nikitaka shamba la kukodisha napata wapi wanabodi? sehemu yenye rutuba ya kutosha na miundo mbinu, na je inagharimu kiasi gani kwa hekari moja?
Ungeweka wazi vitu vifuatavyo:
1.Unatarajia kulima mazao gani?
2.Shamba liwe mkoa gani?
3.Unatarajia kulima ekari ngapi?
 
Ni wazo zuri sana lakini kwa ushauri wangu, Mahindi si zao la kuanza nalo kwa Taznania kama zao la biashara, kwani lina siasa nyingi unaweza kukata tamaa mapema.

Mf. unaweza ukaamua uuze mahindi mabiji serikali waksema NO, ukasema uuze mfano kwa mnunuzi anayetaka kupeleka Kenya wakasema NO, kuna upungufu wa chakula nchini, hivyo kama hayo mahesabu yako yanaangalia soko la ndani sawa, lakini kumbuka kwa sasa gunia la kilo 100 la mahindi ni Tsh. 35,000- 40,000.
Hivyo ushauri wangu ungeanza na mazao kama ya viungo, mf. Tangawizi ambayo soko liko njenje ndani na nje ya nchi na halina siasa humo ndani.
 
Ungeweka wazi vitu vifuatavyo:
1.Unatarajia kulima mazao gani?
2.Shamba liwe mkoa gani?
3.Unatarajia kulima ekari ngapi?

Mkuu,

Mimi sijali sana mazao gani ningependa tu isiwe mbali sana na Dsm maana siku yangu ya mapumziko Jumapili tu na jumamosi nipo mzigoni.Lakini nafikiria kati ya mpunga au mahindi lakini naomba mnishauri mazao gani yanalipa zaidi kwa maana hayahitaji usimamizi saana. Naona Morogoro itakuwa karibu au kati ya Moro na Dodoma au kati ya Chalinze na Kabuku.

Yaani sehemu ambayo nitaweza kwenda na kurudi.
 
Kwa mkoa wa Dodoma rates za kukodi ni kuanzia elfu 15 mpaka 25 kwa ekari,

Mbeya eneo la mbarali naambiwa inafika hadi laki 2 kwa ekari

baadhi ya sehemu za mvomero ni elfu 45 kwa ekari...............wadau wengine watakupa bei kwa maeneo yao lakini hujasema unataka kulima nini

Masikini_jeuri,

Hapo Mvomero ni mazao gani yanastawi? Mpunga unakubali? Mahindi je? Je mpunga wa kumwagilia kuna system za umwagiliaji? au mvua ya kutegemea kudra za mungu?
 
Currently nina heka 100 maeneo ya malolo ila Tuliani nimepatarget mda mrefu mkuu ebu nipm contacts zako ili tujikwamue na huu ubepari wa kuajiliwa na kunyanyasika maofisini mshahara wenyewe na 2mil haufiki na kazi mpaka 6pm.

Watoto home unaonana nao kwa kubeep as if uko safarini kisa kazi
Big up mkuu tuwasiliane ingawa pia natega mingo kilosa unajua wengine ata kusoma ela zilitokana na jembe so iko kwa damu
 
Hivyo ushauri wangu ungeanza na mazao kama ya viungo, mf. Tangawizi ambayo soko liko njenje ndani na nje ya nchi na halina siasa humo ndani.


Asante sana Mkuu;
Nimeshauri kule kwa mdau wa vitunguu kuwa we need to set these records strait mfano mazaoa kama haya wapi yanastawi na kuna hitajika nini hadi yanafika sokoni na masoko yaliko...........shime tuungane kutengeneza hii database.

Maundumula: mvomero kuna stawi vyote mahindi na Mpunga kwa baadhi ya maeneo; na nilikofika mimi wanategemea mvua za msimu na hasa ka mpunga lakini kw amahindi kuna maeneo amabayo walima mara 2 kwa mwaka na wanategemea pia kilimo cha umwagiliaji maji.

Nitaendelea kutafiti
 
Masikini_Jeuri,

Naomba uendelee kutuhabarisha. Halafu ningependa kujua kwa mtu anayeanza vizuri ni kununua eneo au kulima kwenye eneo la kukodi?
 
Naomba kuuliza pia Kilimo cha viungo kama Tangawizi, Vitunguu na vitunguu swaumu ni wapi vinastawi? maana jamani vuitunguu vimepanda sana bei. Tulikuwa tunanunua kilo sh 700 sasa hivi eti inafika 1500.
 
wadau nauliza kuhusu kilimo cha maharage ya soya kwa hapa kwetu tz ni wapi yanalimwa (yanastawi)?
 
Jamani mimi naomba kupata soko la njugu mawe. Nimelima kama heka tano. Nategemea kuvuna mwezi mei. Nipo namtumbo songeaJamani mimi naomba kupata soko la njugu mawe. Nimelima kama heka tano.

Nategemea kuvuna mwezi mei. Nipo namtumbo songea
 
Hongera kwa jitihada kaka, lakini hakikisha unatumia mbolea ili kuhakikisha mavuno hayo, pia spacing shambani ni jambo la msingi sana kwani mahindi unapaswa kuwa na mahindi 17000 kwa ekari.

Bei ya mahindi msimu huu haijafika 50000 hapa tuliani hiyo pia isikufanye uchanganyikiwe. Tuwasiliane ukitaka ushauri wa kitaalamu zaidi
JF

Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.

Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.

Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.

Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.

Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m by July this year.

Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.

Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh

By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe. by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. Sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.

This is a challenge to you JF - hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.

Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.
 
Naona umeamua kuwa tajiri, lkn hii ndo safi kwa sbb si kila mtu ataletewa sahani ya ubwabwa mezani na serikali.

Wazo langu kwako ni kuongeza thamani ya mazao yako, badala ya kuyauza yt kama mahindi, mengine uza kama unga, na hapo ndo utapata hy bei ya 600, otherwise utaishia kuuza gunia 30000 na hesabu zk zitaharibika af utatafuta mchawi, kumbuka hp kila mtu kavuna mahindi sooo usitegemee bei kuwa kubwa km unavyopigia mahesabu
 
Mkuu shukrani kwa kutupa uzoefu wako mimi bado naamini kilimo kinakomboa. Huwezi jua umetufunua wengi tena kwa mtaji mdogo tu hivyo mtu unaweza kufanya investment ya maana.
 
Habari za kazi na pilika za maisha wana Forum. Ninatafuta mashamba ya kukodi, ninahitaji heka 20 , ninaishi Mbeya kama kuna mtu mwenye taarifa za upatikanaji wa mashamba nitashukuru kama atanisaidia,asanteni.
 
Back
Top Bottom