Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Naomba report ya kazi yako kama kuna mafanikio katika kile ambacho ulipanga? nataka kufanya kazi kama hiyo pia, ila uoga ndio unanikaba..
 
naomba report ya kazi yako kama kuna mafanikio katika kile ambacho ulipanga?
nataka kufanya kazi kama hiyo pia, ila uoga ndio unanikaba..

Ni wazo zuri kupata mawazo toka kwake,tatizo anaweza akakupa uzoefu wa kilimo cha mahindi kanda ya Dodoma, na uzoefu huo usikusaidie kama uko nyanda za juu kusini.

Mfano; Njombe mahindi yanapandwa november/desemba na yanavunwa july/august mwaka unaofuata na morogoro mahindi yakipandwa march na june yanavunwa, na mazao mengine pia. Ukiweza sema unataka kulima zao fulani na mahali/zone fulani ili wazoefu wa kanda hiyo au kituo cha kilimo kilicho karibu nawe kinaweza kukusaidia.
 
i do the same lakini kidogo kidogo, i mean seed money inaweza toka popote but then ukishapanua endelea kuexpandi but kwa kutumia faida itokanayo na kilimo, that may take several years to be a commercial farmer, wish you el nino all tha best of luck!
 
UPDATE KWA WANA JAMII

Msimu wa kilimo 2010

Kwanza kheri za xmas. Niliamua kulima heka 50 za kuanza ambapo nilinunua heka moja kwa Tshs. 50,000 kufanya jumla yote kuwa Tshs. 2.5m. Kilimo kilianza msimu wa kilimo 2010 ambapo heka zote zililimwa kwa Trekta kwa Tshs 30,000/- Kila hekari. Tulipanda mvua za mwanzo kwa mikoa ya morogoro ambapo ni Mid January.

Mahindi hayakuota kwa uhakika hivyo ilibidi turudie tena kupanda wakati wa kupalilia. Baada ya marudio tathmini ilionyesha Mahindi yameota vizuri sana hivyo ikanipa moyo wa kupata mafanikio.

Uangalizi ulikuwa mzuri kwani tuliweka kambi kule kule shambani, mimi pamoja na majukumu mengine ya kiofisi (muajiriwa) nilipata nafasi mara moja kwa mwezi atleast kutembelea na kuona jinsi kazi inavyokwenda.

Wakati wa mahindi kubeba watoto Mvua huko Tuliani ilipotea kwa muda, hapo tukawa na wasiwasi sana, ilivyorudi mahindi yakawa yamedhoofu, hata hivyo jambo hili halikunifanya niwe na mawazo mengi kwani bado wakulima wenyeji walinipatia moyo kwamba mavuno yatakuwa mazuri.

Kipindi cha mavuno nilikuwa shambani, kazi ilianza vizuri, tulivuna na kupigapiga mahindi yetu na kupaki kwenye magunia, hapa sasa ndiyo ilikuwa kuona matokeo ya kazi yetu yote tuliyoifanya tangu kununua shamba, kulima, kupalilia, kuvuna na parking.

Ndgu zangu kwa ufupi hali ilikuwa mbaya sana, malengo yangu hayakutimia hata nusu yake, tulipata magunia 60 tu kwa hekari zote 50. niliishiwa nguvu na niliamua mahindi hayo yabakie huko huko shambani kwa muda wakati natafakari wapi tumekwama na je option B ni ipi.

Labda niwape tu gharama kwa ufupi:
Ununuzi wa shamba 2.5m; Kulima kwa heka ni Tsh. 30,000; kupalilia kwa heka 15;000 hii ni pamoja na kurudia kurudia kupanda sehemu ambazo hazikuota; kuvuna tuliingiza nguvu kazi wenyewe plus additional ya Tshs. 50,000.

Jumla ya gharama zote bila Man Power yangu ya ndugu yangu ambaye ni Project Manager inakuwa Tshs. 4.8m. mapato tukapata gunia 60 @56,000 = 3,360,000/=

Msimu wa kilimo 2011:

Kumbukeni nilianza na magunia yangu 60 niliyopata hasara toka msimu uliopita (sikuyauza); baada ya kufanya tathmini kwa kina nikaona ni vigumu sana kutoka kwa kutumia hiki kilimo cha kizamani hasa ukizingatia sina mtaji wa kutosha, hivyo nikaamua kubadilisha plan nzima. Kwa sasa tukaamua msimu huu hatutafanya kilimo badala yake tutanunua mazao toka kwa wenzetu na kuuza wakati yatakapopanda bei, ingawa bado kwa wakati huo nilifikiria sana kufanya food processing yaani uchumi wa kilimo. (agro -economics)

Mwezi wa tatu mwaka huu, tulianza kuwapa advance wakulima wenzetu - Mahindi na pesa ili mavuno yakifika basi warudishe mkopo kwa mahindi. hapa ni hesabu zilifanyika sababu ukipata gunia moja basi utarudisha mawili na ukipata Tshs mia basi utarudisha mia mbili.

Hatukuwa na wasiwasi sababu hawa tuliowakopesha ni wakulima wenzetu na majirani - wakuu mwezi wa tano tulianza kupokea mafao, tulikusanya mahindi gunia mia 300. Gunia hizi hatukuziweka tu, nilianza muda huo huo mwezi wa tano kusafirisha dar kwa ajiri ya processing.

Animals food processing:
Moja kwa moja nilijiingiza kwenye processing ya vyakula vya mifugo kazi ambayo naifanya mpaka sasa, na bado tunanunua mahindi kwani hayo gunia 300 hayatoshi ya yaliisha mapema tu. Nimeshafungua kampuni ya inafanya kazi mpaka sasa ingawa mwanzo huwa mgumu ila tunafanya vizuri kwani sasa kampuni ina miezi sita na mapato yanaonekana.

Je nitaendelea na Kilimo au nitanunua mazao na kufanya food processing tu?
Wakuu kilimo si lelemama, lazima mtu ujipange kweli kweli, kwa sasa nasitisha kilimo kwa muda lakini nitaendelea na kufanya processing ya vyakula vya mifugo; ila bado nitakuwa vijijini kwani nahitaji haya mazao kwa kazi yangu hii.

Bado nina muda kama nilivyowaahidi kwamba kufikia 2015 basi niwe nimetokana na huu umaskini - kwa sasa mungu akibariki nitakuwa naachana na ajira mwezi tarehe kama ya leo mwakani kwani kazi za kampuni yangu zimeanza kuzidi na zinahitaji uwepo wangu.

Kwa wale mnaotaka kulima siwakatishi tamaa ila muwe waangalifu sana kwani katika kilimo unaweza kuingiza Tshs 10m then ukapata 2m tu, mimi nimebadilisha upepo kwa muda, nikirudi kwenye kilimo basi nitarudi kivingine si hivi.

Mwisho Xmas njema na Kheri ya mwaka mpya.

Elnin0:
 
Ni experience nzuri uliyoipata na ninaamini imewasaidia wengi. Nimekuwa encouraged sana na flexibility yako na hasa pale ulipoamua hata kutouza mazao ili kupata muda wa kufikiri nini kifanyike! Hongera!

Naomba kama utaweza tusaidie mchanganuo wa hii ya food processing ... gharama tangu mwanzo mpaka umeziingiza sokoni. Je kuna mashine unapaswa kununua? Ni tsh ngapi? Soko lako liko wapi? (I mean wateja wako wakubwa) na je soko hilo ni reliable?

Natanguliza shukurani!
 
Mkuu EL asante,

Nikupongeze kwa ujasiri wa kusema ukweli wa hali halisi iliyokutokea.Nikupe shukrani pia kwa kutoacha kilimo na kuingia ktk usindikaji wa mazao ya kilimo. Hii ndio picha halisi ya kilimo cha kutegemea mvua.

Je hilo shamba unalifanyia nini kwa sasa? Je una mpango wa kuliuza? 2013 mimi nitaingia ktk kilimo cha mahindi rasmi huko Iringa,hopeful nitakuwa mteja wako ktk kiwanda chako.
 
Kilimo kweli kigumu, lakini to be fair unapowalangua wakulima nako nikuwatia umaskini na kuondoa uezekano wa wao kuondokana na umaskini.
ni kweli lakini mazingira yanafanya hata nionekane nawasaidia, mtu ana heka 4 shambani lakini mwanae anahitaji kwenda shule, uniform pamoja na matumizi mengine, hakuna benki wala kitu cha kuweka rehani shamba lake apate pesa.

Ananifuata mimi, namwezesha kutatua matatizo yake lakini na mimi at the end of the season nipate faida, ni kweli lakini ukiingia kwenye biashara utaelewa zaidi what i mean.

Kiukweli wakulima wadogo wadogo wana matatatizo mengi sana na nawaambia hata siku moja hawataondokana na umaskini wao kama kweli mipango ya serikali itabakia huwa hii hii. kungekuwa na mfumo wa mikopo na magulio kma ilivyokuwa miaka ya nyuma kipindi cha mwalimu nafikiri ingesaidia lakini bila hivyo walanguzi wanapokewa kama wafalme kwani wanatatua matatizo ya hawa wakulima hasa kipindi cha kilimo wakati ukata unakuwa umezitawala familia hizi.

Ukiishi kule kwa mwezi mmoja mashambani utaona hii nchi wanafaidi ni 10% tu, wengine 90% ni mateso matupu, na hawa ndiyo wako huko vijijini.

Kwa hiyo mkuu usinilaumu mimi Elnino kununua hivi vimahindi gunia 300, mimi niite mganga njaa tu; kuna waarabu wananunua mahindi na mpunga maelfu kwa maelfu ya tani huko huko. nafikiri mfumo hamsaidii mkulima wa chini kabisa - wapi akope na wapi auze mazao yake baada ya mavuno. sasa hiyo ni topic nyingine na pana sana.

Mkulima anaumia na ataendelea kuumia mpaka mfumo wa kilimo ubadilishwe.
 
Mkuu Elnino.
Nimefurahishwa sana na uzoefu wako ktk mapambano na natumaini utatimiza ndoto zako maana kupata mkondo wa pesa si kazi lelemama.

Mi mwenyewe nipo ktk kilimo cha mpunga ifakara msimu wa tatu sasa lakini mambo sio mazur ila sababu ni kilimo chakutegemea mvua.

Ushauri wangu wakati unaendelea na agro processing angalia ni jinsi gani utaboresha kilimo cha mahindi.

Nakutakia kila la kheri
 
Mkuu EL asante,

Nikupongeze kwa ujasiri wa kusema ukweli wa hali halisi iliyokutokea.Nikupe shukrani pia kwa kutoacha kilimo na kuingia ktk usindikaji wa mazao ya kilimo. Hii ndio picha halisi ya kilimo cha kutegemea mvua.

Je hilo shamba unalifanyia nini kwa sasa? Je una mpango wa kuliuza? 2013 mimi nitaingia ktk kilimo cha mahindi rasmi huko Iringa,hopeful nitakuwa mteja wako ktk kiwanda chako.
Mkuu Malila.
Wakati unaendelea nakujiandaa na kilimo cha mahindi 2013 inabidi niwe karibu nawewe maana namimi nampango huo huo maana kwa miaka mitatu nimekuwa nalima mpunga ifakara bila mafanikio yakuridhisha ivo nataka niugawe mtaji wangu mara mbili ktk mahindi na mpunga maana nimeshafanikiwa kupata nyenzo kidogo za kulimia.
 
Brother El Nino nimekuelewa. Siamini serikali yaweza kufanya chochote manake vituko vilivyopo huko kwa wakuu wenyewe unaweza kujua nini cha ku-expect.

Nothing!!. Rai yangu tu kwamba tujitahidi hata kwenye huo unyonyaji tujaribu kurejesha japo kidogo kwenye hiyo community tuliovuna ili walau ianze kujikongoja.
 
Mkuu EL asante,

Nikupongeze kwa ujasiri wa kusema ukweli wa hali halisi iliyokutokea.Nikupe shukrani pia kwa kutoacha kilimo na kuingia ktk usindikaji wa mazao ya kilimo. Hii ndio picha halisi ya kilimo cha kutegemea mvua.

Je hilo shamba unalifanyia nini kwa sasa? Je una mpango wa kuliuza? 2013 mimi nitaingia ktk kilimo cha mahindi rasmi huko Iringa,hopeful nitakuwa mteja wako ktk kiwanda chako.
Malila, kweli sijajua nitalifanya nini hilo shamba, kwani kuna kibanda kidogo na mifugo kiasi - kuna mtu anaishi pale.

Sijajua naweza kuangalia either kupanda miembe au zao lolote la kudumu, kuliuza si option nzuri kwangu. Mzee kama unaingia iringa kulima mahindi tuwasiliane - nafikiri next year naweza kuhitaji tani nyingi zaidi.
 
Elnino, asante kwa habari na kutupa hali halisi ya huko.

Ntakutafuta siku moja nikiwa mitaa ya Morogoro/Dar kwani kuna mambo itakuwa vema kuongea moja kwa moja.

Habari kama hizi kwa kweli ni nzuri sana kwa watu kuja na kusoma ili wajue waanzie wapi na wategemee nini.
 
Ni experience nzuri uliyoipata na ninaamini imewasaidia wengi. Nimekuwa encouraged sana na flexibility yako na hasa pale ulipoamua hata kutouza mazao ili kupata muda wa kufikiri nini kifanyike! Hongera!

Naomba kama utaweza tusaidie mchanganuo wa hii ya food processing ... gharama tangu mwanzo mpaka umeziingiza sokoni. Je kuna mashine unapaswa kununua? Ni tsh ngapi? Soko lako liko wapi? (I mean wateja wako wakubwa) na je soko hilo ni reliable?

Natanguliza shukurani!
Esther, Kwa ufupi hii biashara inahitaji pesa nyingi kiasi - ni vigumu kukupa mchanganuo lakini utahitaji machine ya processing complete approx 30m.
Utahitaji place of installation na connections zote; hapa mafundi mitambo na umeme wa viwandani.
Ujenzi wa stoo;

Utahitaji consultation fee toka kwa bwana mifugo. Lastly utahitaji materials toka mikoani - mahindi, dagaa, mashudu ya alzeti / pamba nk - unahitaji channels toka mikoani wa hili

Nafikiri unaweza kuanza ukiwa na initial capital not less than 80m - 90m to be in safe side. Masoko hamna shida kuna watu wengi sana ni wafugaji wa Nguruwe, Kuku wa kisasa, Ngombe wa maziwa, mbuzi nk. Lakini wafugaji wa kuku wanaweza kuwa wateja wako wakuu na ni wengi sana kwa hili hamna shaka.
 
Elnino, asante kwa habari na kutupa hali halisi ya huko.

Ntakutafuta siku moja nikiwa mitaa ya Morogoro/Dar kwani kuna mambo itakuwa vema kuongea moja kwa moja.

Habari kama hizi kwa kweli ni nzuri sana kwa watu kuja na kusoma ili wajue waanzie wapi na wategemee nini.
mkuu upo? yes kilimo ni kizuri na kinaweza kumlipa mtu, lakini bila kuwa makini ni hatari, unaweza kujikuta unapoteza mtaji wote.

aisee kuna rafiki yangu ananitania ananiambia hivi kwenu sikonge hakuna mashamba mbona kila siku unahangaika kununua huku wakati kwenu unajidai ardhi ya kumwaga? tena bei ni bure? ha ha ha

nataka nimpeleke pori la Ipemba -Pazi akavune asali awe tajiri.
 
Brother El Nino nimekuelewa. Siamini serikali yaweza kufanya chochote manake vituko vilivyopo huko kwa wakuu wenyewe unaweza kujua nini cha ku-expect. Nothing!!. Rai yangu tu kwamba tujitahidi hata kwenye huo unyonyaji tujaribu kurejesha japo kidogo kwenye hiyo community tuliovuna ili walau ianze kujikongoja.
safi mkuu, kwa mfano mimi kijijini ambapo kuna shamba langu nawakilishwa na nakuwa napata updates zote (active member) za mipango ya kijiji chetu- na mapato yetu tunalipa kodi kadri tunavyopangiana wenyewe kwa maendeleo ya kijiji chetu.
 
Mkuu Malila.
Wakati unaendelea nakujiandaa na kilimo cha mahindi 2013 inabidi niwe karibu nawewe maana namimi nampango huo huo maana kwa miaka mitatu nimekuwa nalima mpunga ifakara bila mafanikio yakuridhisha ivo nataka niugawe mtaji wangu mara mbili ktk mahindi na mpunga maana nimeshafanikiwa kupata nyenzo kidogo za kulimia.

Natafuta mashamba mazuri ktk maeneo ambayo mvua si tatizo, pia maeneo ambayo naweza kulima soya/maharage. Nitakupa feedback kila nikipata fursa nzuri ktk kilimo cha mahindi.
 
mimi nipo mtwara. ninampango wa kulima eka 3 za choroko, haka kazao kanalipa vizuri.
 
HI ELNINO
Vipi Project inaendaje? Nataka nami pia niaze. Nimeagiza trakta MF Model 350. NInazo ekari 70. NInaweza kulimia majirani kwa elf 50 kwa ekari na kupiga harrow kwa kiasi hicho hicho. Nipo maeneo ya KImanzichana - kule jirani na akina Adam Malima (just 4kms kutoka nyumbani kwao). NIngependa uni-PM unipe maujanja ya kuendesha maisha pasipo kutegemea mshahara kwa kila kitu!
JF
Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.
Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.

Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.

Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.

Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m by July this year.

Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.

Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh

By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe. by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.

This is a challenge to you JF- hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.

Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.
 
Back
Top Bottom