kusema ukweli kilimo ni kizuri na watu wanatajirika kwa kilimo sema uvivu wetu na kutaka utajiri kirahisi ndio unatuponza ila ukitia nguvu kwenye kilimo hakika mshahara utausahau kabisa, ila kilimo ni bora ulime sehemu ambapo unaweza ukavuta maji na kumwagilia mvua zikigoma pia kilimo kinakatisha tamaa sana kwenye masoko, kilimo kinahitaji mtaji wa kutosha, mvua zikigoma unalima tena lkn kama mtaji mdogo mvua zikigoma msimu huo hulimi tena.
Soko la mazao kuna kipindi mavuno yanakuwa mengi kila mkulima anabarikiwa mazao yanakua mengi utauza kwa hasara, pia sera ya serikali kuzuia kuuza mazao nje nalo ni tatizo,wakati unalima huku ukihangaika na vibarua wapo kimya hawakusaidii chochote ukisha vuna tu wanakupangia bei na mahali pa kuuza, angalia wakulima wa kahawa wanalima kwa gharama kubwa wakisha vuna tu wanaambiwa wauze kwenye vyama vya ushirika kwa bei watakayo wao ushirika na tena ni kwa mkopo hata kama bei itapanda kwenye soko la dunia bado mkulima watamlipa ile ile aliyouzia.
Wanafaidi wafanyakazi wa ushirika, serikali inatakiwa uwaruhusu wakulima wauze kokote watakako pata soko, pia serikali itulinde wakulima ipige marufuku juice toka dubai wakati matunda yanaoza mashambani tanga, juice zitengenezwe hapa hapa, ipige marufuku nyanya toka nje kuokoa za wakulima wa iringa zinazo oza kwa kukosa soko, ipige marufuku apples toka africa kusini ili zile zinazozalishwa njombe kule uwemba zipate soko.
Ipige marufuku shahiri ya kutengenezea pombe ili wanaolima wapate soko, kama wakullima wazalisha kwa kiwango cha chini hao wanunuzi watoe mbegu na elimu kwa wakulima ila wazalishe wanavyo taka wao,wakati kiwanda cha ivory kinaanza kukamua mafuta ya alizeti walienda kwenye vijiji zinakolimwa alizeti kwa wingi na kutoa mbegu ya alizeti wanazotaka wao,wakulima wakalima na wao wakaja kununa kwa wingi hayo ndio yanatakiwa kufanyika hapa nchini kwetu na sisi vijana tutahamasika kulima maana soko litakuwepo,hv kule manyara shahiri na ngano si inakubari kule?kwann serikali haiwalizimisha hawa watengeneza bia kulima hapa hapa nchini?
kama wanavyo fanya viwanda vya sukari?miwa imekuwa mkombozi kwenye baadhi ya maeneo,wakulima wanalima kwakua soko lipo,nenda wilaya missenyi mkoan kagera ukaone watu walivyo hamasika na kilimo cha mua.
Hongera sana EL kwa uamuzi wa busara. Ila nadhani hapo kwenye bold kwangu mm ni pazuri mno kuwa kweli (too good to be true) please please naomba upadefend.