Kilimo cha kiangazi kinaweza kisikulipe au kikakulipa sana. Unahitaji ujuzi flani. Lakini kama unataka upate faida, unahitaji yafuatayo
1. Eneo utakalolima lisiwe chini ya ekari tano, ili uweze kuwa na mimea ya mahindi 120,000 kwa uchache. kila hindi ukiliuza kwa sh 150, utakuwa na tsh 18,000,000. Hii ni bei ya shambani
2. Maji.. ili uweze kuotesha na kustawisha mahindi 120,000, utahitaji maji ya kina kisichopungua mm 600, maana yake utahitaji takriban lita za ujazo 15,000,000. Ikiwa kila lita utaipata kwa cent 25 hadi 30, utatumia kati ya 4.5 - 7.5m.
3. Mbolea - hapa utahitajimbolea aina ya DAP au CAN mifuko kama minne, mfuko mmoja na nusu utaweka siku 14 baada ya kupanda na 2.5 iliyosalia utaweka siku 45 baada ya kupanda.
4. Ulinzi na udhibiti wa wadudu na visumbufu vya mazao... andaa 200,000/-
5. Mengineyo- hapa nimedhania ardhi ni yako na si ya kukodi. Sijaweka gharama za kuandaa shamba kwani itategemea njia rahisi iliyopo eneo lako kati ya tractor au vibarua wa kawaida..
kuhusu eneo kuwa kubwa, ni kwamba ekari tano ndio utapata faida, ukilima pungufu ya hapo utapata hasara. Haitalipa kwa sababu gharama zitakuwa juu. kingine cha muhimu ni kuwa soko la uhakika linatakiwa kwani kuanzia siku 60 baada ya kupandwa, mahindi kwa ajili ya kuchoma yanakuwa tayari na siku ya 75, siku 15 baadaye, mahindi huanza kuwa magumu na yanakoma kuwa ya kuchoma na kuwa ya ugali. angalizo hapa ni kuwa lazima uwe na soko la haraka kuweza kumaliza bidhaa ndani ya muda huu mfupi.
aina ya mbegu ya mahindi utakayotumia itategemea mahali ulipo, ikiwa ni ukanda wa joto au baridi. Aina ya STUKA au TAN256 zawezafaa. kama vipi uni pm upate ushauri kuhusu hili
Mimi ni public consultant na nimebobea katka kilimo hiki cha mahindi. usisite kuuliza swali lolote uwapo na tatizo.