Wewe binafsi umeshawahi kulima mahindi,nahisi kama umebobea kwenye ushauri tu.
Mkuu ili swali ni langu au la kwa ndugu Capital?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe binafsi umeshawahi kulima mahindi,nahisi kama umebobea kwenye ushauri tu.
Hapo tatizo ni soko tu!
Maana mahindi mabichi ni kipindi kifupi sana yanaanza kukomaa.
La capital,maana maelezo yake yanatofauti sana na ya wakulima.
Miche kadhaa,mvua kiasi kadhaa nk. It was confusing.
Asante mkuu kwa kunielimisha. hata hivyo ktk context ya ujasiriamali wa kisasa, si rahisi kuwa na uhakika wa 100%. hii inatokana kiwango cha uwekezaji na uzalishaji husika. maana yangu ni kuwa ukiwekeza sh 50 elfu na ukapata mahindi 200, soko siyo tatizo kwani mtu mmoja atayaninuwa mara moja.Mkuu kwa utafiti wangu haba,sijawahi kusikia mkulima wa mahindi mabichi akilalamika kukosa soko kipindi cha mavuno,labda wewe kwa uzoefu wako utusaidie kama kuna changamoto hiyo mkuu
Asante mkuu kwa kunielimisha. hata hivyo ktk context ya ujasiriamali wa kisasa, si rahisi kuwa na uhakika wa 100%. hii inatokana kiwango cha uwekezaji na uzalishaji husika. maana yangu ni kuwa ukiwekeza sh 50 elfu na ukapata mahindi 200, soko siyo tatizo kwani mtu mmoja atayaninuwa mara moja.ila ukiwa na mahidi laki moja na umwekeza milion 5, then kuwa na soko ni kitu cha msingi sana. asante na karibu sana tuendelee kuelimishana.
Mkuu si kua nilijaribu kupinga hoja yako,ila nilichojaribu kukiandika ni kutokana na uzoefu wangu mdogo,kuendana na kile mleta mada anachotaka asaidiwe kupata mwanga!ni wazi mleta mada ameweka wazi kua anataka kulima katika kiwango kidogo,ndio maana mimi nijaribu kumtoa hofu kutokana na uzoefu wangu kua,kwa kiwango iko anachopanga kulima,soko halitakua kikwazo sana!nadhani mchanganuo ulioutoa mkuu huko kisayansi na wenye tija zaidi,ila sasa kwa sisi wenye uwezo mdogo wa kimitaji,na nia yetu tufike mbali hata kufikia huko ulipotolea mchanganuo,tutumie njia gani ili tuweze kuzishinda changamoto na kufikia huko?
Asante. Sina tatizo na unalolisema hata kidogo. Kwa mfano kama mtu anataka kuanza kidogo kidogo, bado anaweza kufanikiwa ikiwa atatumia mbinu za kitaalam. Soko pia linahitaji mbinu, nasita kusema soko siyo tatizo.
Mkuu kwa utafiti wangu haba,sijawahi kusikia mkulima wa mahindi mabichi akilalamika kukosa soko kipindi cha mavuno,labda wewe kwa uzoefu wako utusaidie kama kuna changamoto hiyo mkuu
Nakubaliana na wewe mkuu,mbinu za kitaalamu ni muhimu sana ili kufikia malengo kupitia kilimo!tuendelee kuelimishana kuhusu kilimo mkuu
Karibu sana mkuu.
Mkuu mimi naomba ushauri wako wa kitaalam kidogo!je kitaalamu natakiwa kwa heka moja nipige mashimo mangapi ya mahindi/kuwe na miche mingapi?na je uwiano wa shimo na shimo/spacing inatakiwa iwe ni cm ngapi?na mwisho je ni mbolea gani nzuri kwa kukuzia mahindi,natanguliza shukrani zangu
Ok. Karibu. Hayo yote inategemea mahali shamba lilipo. Kama ni ukanda wa juu au wa chini, mfano mbeya, rukwa, ruvuma au mikoa ya pwani. Pili hutegemea na aina ya njia ya upatikanaji wa maji ikiwa ni ya mvua au unamwagilia. Kama mshauri, nitashindwa kukupa ushauri wa jumula kwani hautakusaidia. Ni vyema ueleze vema mahali shamba lilipo. Karibu tena
Ahsante sana ndugu yangu!shamba ninalotarajia kulima lipo katika mkoa wa Morogoro,wilaya ya Mvomero!ni shamba lililo kwenye mabonde yenye unyevu ambao wengine upandaga mpunga kipindi cha mvua,na natarajia kulima kuanzia mwezi july!pia ni ukanda wa maji maji,kwa hiyo iwapo ukame utakua mkubwa nina uwezo wa kumuagilia!nataraji maelezo yangu yamejitosheleza mkuu,nasubiri kwa hamu ushauri wako wa kitaalamu!asante sana
Ok. Nimekupata.
Kwanza mwezi july ni mbele mno, jitahidi by june 15 upande ili upate advantage ya unyevu nyevu uliopo sasa ambao unaishilia. Ukipanda july, mahindi yako yatakumbana na joto kali la mwezi wa tisa, kipindi ambapo mahindi yatakuwa yanachanua. Hili joto kali hufanya chavua (mbegu za kiume za mahindi) kushindwa kuota hivyo kufanya hindi kuwa na mapengo mapengo ndani. yaani hindi halijai. Hata kama umetia maji mengi namna gani.
Pili ni kuwa kwa maeneo ya Mvomero, yaweza kuwa Dakawa, Mbigiri au Mateteni au Msowero, hata maeneo ya Mkindo na Mtibwa, mbegu ya mahindi inayofaa ni STUKA (M1). Hii mbegu inapatikana maduka mengi ya pembejeo.
Namna ya Kupanda
mstari hadi mstari sentimita 75. Hindi hadi hindi (ndani ya mstari) sentimeta 30.
Panda mbegu mbili au zaidi na siku 10 baada ya kupanda (au siku 5 baada ya kuota) ng'olea na bakiza hindi moja kila shimo.
Baada ya Siku 14 baada ya kupanda, tia mbolea aina ya Diammonium Phosphate (DAP) kwa kiasi ya mfuko mmoja kwa ekari (50 kg DAP).
Baada ya siku 45 (muda ambao jani la mwisho linatokeza) tia mbolea aina ya UREA (mifuko 1.5 - 2) kwa ekari.
Hakikisha magugu unayadhibiti sawsawa. Wadudu huwa wengi kipindi cha kiangazi. Sumu aina ya KARATE inatakiwa hapa, ml 10-25 kwa lita 20 za maji kulingana na wingi wa wadudu na utapiga katika interval ya wiki mbili hadi jani la mwisho likitokeza (kati ya siku 45-50).
Umwagiliaji - saa 24 kabla kabla ya kupanda hakikisha unamwagilia maji ya kutosha, kisha panda na acha hadi mahindi yaote (siku 5-7). kisha endelea kumwagilia maji ya wastani lakini ardhi ilowane kwa muda wa wiki mbili. hapo utamwagilia kila baada ya siku tatu. kuanzia wiki mbili hadi tano, utaongeza kiasi cha maji kiasi. Wiki tano hadi nane (siku 35-56) utaweka maji mengi (ya kutosha lakini siyo mafuriko) kila baada ya siku nne au tano. Pia utaangalia mwenyewe hali ya shamba na kufanya maamuzi stahiki. Kuanzia siku ya 56 na kuendelea, unaweza kupunguza kiasi cha maji kwani kama ni mahindi ya kuuza yakiwa mabichi, huu ndio muda wa kuanza kukomaa. unaweza kumwagilia maji mara moja katika siku tano.
Natumaini maswali yako mengi yamejibiwa ila usisite kuuliza ikiwa una swali specific.
Karibu sana
Nashukuru sana ndugu yangu,ukweli ni kua maelezo yako yamenipa mwanga wa kutosha sana tu!labda niweke mambo sawa ili kupata msaada wa kiutaalam zaidi,eneo ninalotaka kulima linaitwa MLALI ni kama 25 Km kutoka Morogoro mjini,eneo ili ni bonde la mpunga,na mara utakapovunwa ndio nataraji kuweka mahindi!je kwa maelezo haya kuna la ziada kunishauri ndugu yangu?
Wewe binafsi umeshawahi kulima mahindi,nahisi kama umebobea kwenye ushauri tu.
Yep. unamaanisha Mlali njia iendayo Mgeta, ukipita Mzumbe Univ.? Huko ni pazuri. ila kuna joto kali sana muda mwingi katika mwaka, kwa hiyo jitahidi upate maji kabla ya kitu chochote. Maji yatakayokuwa ardhini wakati ukipanda hayatatosha, huenda mimea ikadumaa kama hutapata maji ya kutosha ndani ya siku 30 baada ya kupanda.