Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Kama umeajiriwa achana na ajira ingia kwenye kilimo au achana na kilimo kabisa.

Ni kweli mkuu, haya mambo hayataki vuguvugu, hautapata matokeo ya kuridhisha. Ni lazime uwe moto au baridi.
 
Kilimo si cha kuchezea waeza filisika ukawa Omba omba pembezoni mwa Barabara, and also kuna kitu huwa kinanishangaza akili hupungua kwa kiasi kikubwa.

Kama Unalima Bora ulime kilimo cha Umwagiliaji. Nyie Mnao amini Mungu ufanye madhambi yako weeeee ulime ardhi eti ikupe utajili gademed.
 
vipi msimu huu kwa wakulima wa nanasi kuanzia dec na hii january?matokeo yakoje mwanalumango upande wa bei sokoni?ni kipindi gani bei ziko juu?ushauri wako na mtizamo wako kwa sasa vipi ni uleule?
 
Hongera. Kaza buti
 
Pole ndugu yangu nimechelewa kukujibu lakini nimeona bora nikujibu.

Mwezi Dec na Jan ni kipindi cha msimu wa mananai na soko la mananasi kama masoko ya mazao mengine yanatawaliwa na theory ya demand and supply na hisi unafahamu, nikiwa na maana kwamba kama uzalishaji ni mkubwa na kwa wakati mmoja soko lazima litafurika na matokeo yake bei itashuka. Ila kwa kipindi chote hiki mananasi kwa bei ya jumla ninakolimia mimi huko Kiwangwa haijashuka chini ya Tshs 600 kwa nanasi moja toka shambani.

Chamsingi ni kuhakikisha mananasi yako yanatunzwa vizuri na kuwa na ubora unaotakiwa, bei hiyo ni kwa mananasi makubwa yaliyotunzwa vizuri. Hadi leo bei imeshapanda kwenye Tsh 800 kwa aina ya nanasi ninalozungumzia ya aina yanayotoka shambani kwangu.

Sasa mimi kwa bahati mbaya nafanyakazi nje ya nchi sina muda sana wa kutafuta masoko mwenyewe ila kwa kipindi hiki ninachozungumzia nilkuwa nyumbani na nimeshuhudia haya ninayoyasema.

Nilichofanya nimeamua kutumia economiv theory ya "economics of scale" kwa maana ya kwamba nafanya uzalishaji mkubwa sana wa mananasi mengi hata kwa bei hiyo na hata kama nitapata faida kidogo kwa kila nanasi lakini kwakuwa yako mengi faida bado inaonekana.

Nipo very serious kwenye kilimo kwakuwa nimeona kitanifanya si kujitoa tu hapa nilipo bali kuwa minionea. Nimepanda mananasi 500, 000 mwaka jana ambayo nitaanza kuvuna desemba hii na ninatarajia kuwa likizo mwezi wa March ambapo nitakuwa TZ natarajia nipande mananasi mengine 200,000 kisha nisimame nianze kuyahudumia mashamba haya kwa ufanisi zaidi ili niweze kwendana na ubora na matakwa ya soko.

Kwahiyo nikiwa na mananasi 700, 000 hata kama nikiuza 400,000 tu kwa mwaka kwa bei ndogo ya Tshs 600 bado ninatarajia si chini ya Tshs 200 milion kwa mwaka.

Si hadithi ni kweli kwakuwa sasa hivi ninavuna toka kwenye shamba langu la hekari 5 la pilot study na matokea ndio yaliyonisukuma kuwekeza zaidi, naona naweza pata pesa nyingi sana kutoka kwenye mananasi zaidi ya hizi ninazopata huku ninakofanyakazi na hii itaweza kunisaidia kurudi nyumbani mapema isivyotarajiwa.

Ukitaka kujifunza na kutiwa moyo tuwasiliane ili December nikupele ukatembee na kujifunza shambani kwangu. Karibu ndugu yangu na ninakutakia kila la kheri, mimi in the long run nimeamua kuwa mkulima na sasa ninajandaa wakati bado nipo kazini na nina nguvu kama kijana.

vipi msimu huu kwa wakulima wa nanasi kuanzia dec na hii january? matokeo yakoje mwanalumango upande wa bei sokoni? ni kipindi gani bei ziko juu?ushauri wako na mtizamo wako kwa sasa vipi ni uleule?
 
Nawashaurini wanajf,limeni zao la alzeti, ni zao zuri saaana kibiashara pamoja na gharama kiduchu za kuendeshea kuhudumia shamba, tofauti na gharama zingine palizi yake ni moja tu, na mazao yanaiva vizuri
 
Nawashaurini wanajf,limeni zao la alzeti ,ni zao zuri saaana kibiashara pamoja na gharama kiduchu za kuendeshea kuhudumia shamba,tofauti na gharama zingine palizi yake ni moja tu,na mazao yanaiva vizuri
hebu tuambie wanalima wapi na na masoko yake yakoje mkuu
 

Mkubwa Mbegu moja ya nanasi ni kihasi gani? Maana Mbegu 500,000 si mchezo....Naona kwa haraka haraka umeinvest si chini ya 50m.
 
Mkubwa Mbegu moja ya nanasi ni kihasi gani? Maana Mbegu 500,000 si mchezo....Naona kwa haraka haraka umeinvest si chini ya 50m.

Muheshimiwa, mbegu moja inagharimu Tshs 115 (bei ya kununulia, kusafirisha na kupanda) inategemea na umbali unakonunua mbegu, kwahiyo mbegu 100,000 zinagharimu 11,500,000 na mambomengine inagharimu wastani wa Tshs 12,000,000 na hivyo mbegu 500,000 zinagharimu takribani Tshs 60,000,000.

Hapo ni kupanda tu, sasa gharama zingine itategemea na hali ya shamba lako, mimi shamba langu lilikuwa ni msitu wenye miti mikubwa kwahiyo kulikuwa na gharama za kufyeka, kuchimba visiki (gharama kubwa hii), kulima na kupiga halo.

Project yangu inakwenda over Tshs. 100,000,000 lakini hii isikutishe utafanya kidogokidogo kulingana na hali yako. Nakutakia kila la kheri, kama nilivokuambia nitakuwa TZ kuanzia 15 March na nitakaa kwa mwezi mmoja kabla sijarudi kazini, kama wataka kujifunza nakuona ninachofanya utaniambia ili wiki endi moja tutembelee uone.
 
Bro Mwanalumango unajitambua sana, ni wabongo wachache walioko ughaibuni wenye wana akili ya kutumia fursa za bongo. Na ukweli ninaoujua mm ni rahisi sana kuwekeza bongo na kupata faida kubwa kuliko kuwekeza huko ughaibuni. Karibu tuijenge Tanzania yetu.
 

Asante kaka. Nimezaliwa Tanzania, nimekulia na nimesoma bure kabisa kwa kodi za Watanzania, nitakufia popote pale lakini nitazikiwa Tanzania inshallah. Tupo pamoja sana.
 
Mwanalumango bwana tarehe hozo ntakutafuta nitembelee project yako mkuu wangu.najua nitajifunza vitu vingi kitoka kwako kaka.
 
Mkuu samahani kama swali hili limeshajibiwa, naomba details kuhusu muda wa kuanza kuandaa shamba la nanasi na kupanda ni lini kwa maeneo ya pwani hasa mkuranga na huko bagamoyo, pia hizo mbegu ni maalumu au mbegu za kawaida tu wanazouza bara barani? nitashukuru kwa majibu yako mkuu
 
Habari wana jf

Hebu niulize jambo, nimeona wengi wenu mlioshiriki kuweka comments kwenye hii thread mtakuwa mna uzoefu mzuri katika eneo hili la kilimo cha mahindi kama ndugu elinino na wengine, naomba kujuzwa yafuatayo:

Ni njia gani ama kifaa gani ama dawa gani bora hutumiwa kuhifadhia mahindi kwa muda mrefu pasipo kuharibika na pia niwekeni na bei kabisa kama ni magunia na dawa ama ni dram?

Na je ni wakati gani bei ya mahindi huwa juu?

Na je ardhi yenye mbolea ya kutosha maana wakati nina lianda shamba nilisambaza mbolea ya samadi shamba zima na pia wakat wakupanda pia niliweka mbolea kidogo kwenye mashimo wakati wa upandaji, swali langu ni je kuna haja tena ya kuweka mbolea ya kukuzia baadae either DAP ama UREA? maana ardhi ina mbolea ya kutosha ya samadi,

Natanguliza shukrani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…