The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Kama umeajiriwa achana na ajira ingia kwenye kilimo au achana na kilimo kabisa.
Ni kweli mkuu, haya mambo hayataki vuguvugu, hautapata matokeo ya kuridhisha. Ni lazime uwe moto au baridi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama umeajiriwa achana na ajira ingia kwenye kilimo au achana na kilimo kabisa.
Ni kweli mkuu, haya mambo hayataki vuguvugu, hautapata matokeo ya kuridhisha. Ni lazime uwe moto au baridi.
nimeachana na kilimo kabisa nitarejea baada ya miaka miwili.Kama umeajiriwa achana na ajira ingia kwenye kilimo au achana na kilimo kabisa.
nimeachana na kilimo kabisa nitarejea baada ya miaka miwili.
vipi msimu huu kwa wakulima wa nanasi kuanzia dec na hii january?matokeo yakoje mwanalumango upande wa bei sokoni?ni kipindi gani bei ziko juu?ushauri wako na mtizamo wako kwa sasa vipi ni uleule?Ndugu yangu Milungwi angalia hiyo nilishamjibu mtu inaweza kukusaidia na kama bado niambie, kama uko tayari mimi narudi Bongo end of this week, naweza kukupeleka shambani kwangu ukaangalie ili ujifunze, wewe nieleze tu kama uko serious. Mimi ni mtoto wa Mkulima nina asili ya kilimo ingawa kwetu huko Moro tunalima sana mpunga lakini nimeamua nifanye maamuzi ya uangalifu sana kwenye aina ya mazao ya kulima yasiyoleta usumbufu wa maradhi au kuathirika sana na ukame na ndo maana nikachagua kulima miwa Kilombero na mananasi Bagamoyo. Mananasi yanapendwa kipindi chochote cha mwaka hata wakati wa jua kali na hayafi, mvua ikija tu yanachipua, kinachotakiwa ni palizi za nguvu na mbolea ya nguvu. Hekari moja ya muwa unaweza tumia mfuko mmoja wa mbolea lakini kwa mananasi kati ya mifuko 4-5 ya mbolea. Angalia hapa kwa uangalifu na hayo ni mahesabu yaliyo sahihi kabisa hayana shaka ndani yake. Kwa gharama ya hapo chini hata ukiongeza asilimia 20 ya gharama bado unapata super profit.
Usikate tamaa, hata hekari moja ukiitunza vizuri inalipa. Angalia mahesabu ya hekari moja.
Shamba lenye visiki
Gharama za kuondoa visiki = 250,000
Kulima = 70,000
Kupiga hallo = 50,000
gharama za mbegu (16,000 kwa hekari moja) =1,440,000
Gharama za kupanda Tshs 15 x 16,000) =240,000
Kupalilia kama mara tano hivi Tshs 60,000 x 5 = 300,000
Mbolea mara mbili kabla ya kuvuna jumla mifuko 10 = 700,000
Jumla ya wastani wa gharama zote hadi unavuna (Total cost) = 3,050,000
Mauzo kwa bei ya wastani wa Tshs 800 kwa nanasi moja, mimi kwasasa hivi nauzi kwa Tshs 1000 kwa nanasi toka shambani kwangu na hakuna tax, kwa hiyo wewe utapata 16,000 x 800 =12,8000
Faida 12,800,000 - 3,050,000 =9,750,00 super profit.
Sasa mimi niliamua nifanya mass production ili hata kama bei itapungua bado nitapata faida kubwa kwa ajili ya economies of scale.
Anza leo usingoje kesho.
Kila la kheri
Hongera. Kaza butiJF
Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.
Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.
Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.
Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.
Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m by July this year.
Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.
Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh
By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe. by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. Sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.
This is a challenge to you JF - hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.
Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.
vipi msimu huu kwa wakulima wa nanasi kuanzia dec na hii january? matokeo yakoje mwanalumango upande wa bei sokoni? ni kipindi gani bei ziko juu?ushauri wako na mtizamo wako kwa sasa vipi ni uleule?
hebu tuambie wanalima wapi na na masoko yake yakoje mkuuNawashaurini wanajf,limeni zao la alzeti ,ni zao zuri saaana kibiashara pamoja na gharama kiduchu za kuendeshea kuhudumia shamba,tofauti na gharama zingine palizi yake ni moja tu,na mazao yanaiva vizuri
Pole ndugu yangu nimechelewa kukujibu lakini nimeona bora nikujibu. Mwezi Dec na Jan ni kipindi cha msimu wa mananai na soko la mananasi kama masoko ya mazao mengine yanatawaliwa na theory ya demand and supply na hisi unafahamu, nikiwa na maana kwamba kama uzalishaji ni mkubwa na kwa wakati mmoja soko lazima litafurika na matokeo yake bei itashuka. Ila kwa kipindi chote hiki mananasi kwa bei ya jumla ninakolimia mimi huko Kiwangwa haijashuka chini ya Tshs 600 kwa nanasi moja toka shambani. Chamsingi ni kuhakikisha mananasi yako yanatunzwa vizuri na kuwa na ubora unaotakiwa, bei hiyo ni kwa mananasi makubwa yaliyotunzwa vizuri. Hadi leo bei imeshapanda kwenye Tsh 800 kwa aina ya nanasi ninalozungumzia ya aina yanayotoka shambani kwangu. Sasa mimi kwa bahati mbaya nafanyakazi nje ya nchi sina muda sana wa kutafuta masoko mwenyewe ila kwa kipindi hiki ninachozungumzia nilkuwa nyumbani na nimeshuhudia haya ninayoyasema. Nilichofanya nimeamua kutumia economiv theory ya "economics of scale" kwa maana ya kwamba nafanya uzalishaji mkubwa sana wa mananasi mengi hata kwa bei hiyo na hata kama nitapata faida kidogo kwa kila nanasi lakini kwakuwa yako mengi faida bado inaonekana. Nipo very serious kwenye kilimo kwakuwa nimeona kitanifanya si kujitoa tu hapa nilipo bali kuwa minionea. Nimepanda mananasi 500, 000 mwaka jana ambayo nitaanza kuvuna desemba hii na ninatarajia kuwa likizo mwezi wa March ambapo nitakuwa TZ natarajia nipande mananasi mengine 200,000 kisha nisimame nianze kuyahudumia mashamba haya kwa ufanisi zaidi ili niweze kwendana na ubora na matakwa ya soko. Kwahiyo nikiwa na mananasi 700, 000 hata kama nikiuza 400,000 tu kwa mwaka kwa bei ndogo ya Tshs 600 bado ninatarajia si chini ya Tshs 200 milion kwa mwaka. Si hadithi ni kweli kwakuwa sasa hivi ninavuna toka kwenye shamba langu la hekari 5 la pilot study na matokea ndio yaliyonisukuma kuwekeza zaidi, naona naweza pata pesa nyingi sana kutoka kwenye mananasi zaidi ya hizi ninazopata huku ninakofanyakazi na hii itaweza kunisaidia kurudi nyumbani mapema isivyotarajiwa. Ukitaka kujifunza na kutiwa moyo tuwasiliane ili December nikupele ukatembee na kujifunza shambani kwangu. Karibu ndugu yangu na ninakutakia kila la kheri, mimi in the long run nimeamua kuwa mkulima na sasa ninajandaa wakati bado nipo kazini na nina nguvu kama kijana.
Mkubwa Mbegu moja ya nanasi ni kihasi gani? Maana Mbegu 500,000 si mchezo....Naona kwa haraka haraka umeinvest si chini ya 50m.
Bro Mwanalumango unajitambua sana, ni wabongo wachache walioko ughaibuni wenye wana akili ya kutumia fursa za bongo. Na ukweli ninaoujua mm ni rahisi sana kuwekeza bongo na kupata faida kubwa kuliko kuwekeza huko ughaibuni. Karibu tuijenge Tanzania yetu.