Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

usikirupuke ndugu utatumia umwahiliaji au annual rain? ukinijib hapo nitakushaur kitu tuko pamoja pia mtaji umekopa au vp
 

UTANGULIZI
  • Mahindi ni zao muhimu linalo limwa katika maeneo ya kitropiki.
  • Udongo wenye uchachu pH 6-6.5
  • Hustawi zaidi kwenye maeneo yenye mwinuko wa 2500
KANUNI YA KWANZA; KUTAYARISHA SHAMBA
  • Tayarisha shamba la mahindi mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita.
  • Mahindi hustawi sehemu yenye udongo wenye rutuba na usiosimamisha maji.
  • Moto usitumike wakati wa kuandaa shamba.
FAIDA ZA KUANDAA SHAMBA MAPEMA
  • Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi kwa kutumia jembe lolote.
  • Masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.
  • Hupunguza magugu.
  • Hupunguza wadudu waharibifu
KANUNI YA PILI WAKATI WA KUPANDA
Wakati wa kupanda hutatanisha kwani mvua haitabiriki,Kama mvua hunyesha nyakati na majira yale yale ya mwaka basi kalenda ifuatayo inaonyesha tahere za kupanda zao la mahindi katika eneo lako.
  1. Mbeya na maeneo ya jirani, mwanzoni mwa mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni.
  2. Morogoro na maeneo ya jirani, Mwezi Januari katikati hadi Februari katikati
  3. Iringa na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni
  4. Songea na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Januari mwanzoni.
Kupanda mahindi mapema ni muhimu kwani uwezekano wa kuvuna mazao mengi ni mkubwa. Kwa mashamba makubwa sana wakati wa kupanda uwe wiki moja kabla ya mvua kuanza kunyesha na isizidi wiki mbili kabla ya mvua. Isiwe mapema zaidi kwani mbegu zitaharibiwa na joto kati ya udongoni wadudu,panya,ndege na wanyama wengineo.

FAIDA ZA KUPANDA MAPEMA
  1. Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.
  2. Magonjwa kama yale ya ya majani (streak ugonjwa wa milia) hayatatokea au yatakuwa kidogo.
  3. Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi yastawi vizuri.
KANUNI YA TATU KUCHAGUA MBEGU BORA
Mbegu bora ni zile zilizo zalishwa kitaalamu.
  • Ni safi hazijabunguliwa na wadudu.
  • Huzaa mazao mengi.
  • Hustahimili magonjwa.
AINA ZA MBEGU
  1. Mbegu aina ya chotara(hybrid)
  2. Aina ya ndugu moja(synthetic)
  3. Mbegu aina ya composite
Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika misingi ya kilimo zina uwezo wa kuzaa magunia 50-80 au tani 5.5 – 7.5 kwa hekta moja au umi kwa hekari.

MAPENDEKEZO YA MBEGUZA KUPANDA

Kuna mbegu nyingi za kisasa zilizoko kwenye soko mfano wa SIDCO ,PANNAR, CHOTARA, kutoka KENYA n.k

KANUNI YA NNE KUPANDA
Idadi ya mimea katika eneo ni muhimu kwani ikazidi
  • Kuna uwezekano wa mazao hupungua.
  • Mmea huangushwa na upepo
  • Mabua mengi hayazai.
Idadi ya mimea nayo ikipungua kwenya eneo husababishwa mavuno kupungua jambo la kufanya ni kupanda mbegu katika nafasi sahihi zilizoshauriwa na wataalamu.

KIASI CHA KUPANDA
  • Mbegu za mahindi huhifadhiwa kwa dawa kali(sumu)
  • Kiasi cha kilo 20(ishirini) za mbegu kinatosha kupanda hekari moja., (*Hii hutegemea na aina ya mbegu)
Nafasi za kupanda.
  • 75cm x 30cm
  • 75cm x 60cm
  • 90cm x 25cm
  • 90cm x 50cm
KANUNI YA TANO; KUTUMIA MBOLEA
  • Mahindi hustawi na kuzaa vizuri iwapo yatapatiwa mbolea pamoja na matunzo mengine ya kilimo bora.
  • Angalizo: Ukipanda mbegu bora bila kutumia mbolea ni kazi bure.
KUNA AINA MBILI KUU ZA MBOLEA
  1. Mbolea za asili mfano; samadi,mboji na majani mabichi,mbolea hizi hua na virutubisho vya kutosh ambavyo havijulikani vipo kwa kipimo kiasi gani
  2. Mbolea za viwandani, hizi hua na virutubisho vya kutosha na vipimo hujulikana, hii inasaidia kujua ni kiasi gani kitumike kwa kipindi gani.
 
Thanks FristLady1 kwa moyo wako wa kutaka ushirika - kazi ni ngumu kidogo lazima u dedicate at least 4 days kila mwezi kwenda site kufanya physical monitoring. kule ni camp bado kwa hiyo utahitaji kwenda na Maji ya kunywa for those days, safari bed na vitu vingine personal.
Chakula ni Local food, hakuna umeme, maji ya kuoga ni ya kisima (local), rafiki zako kwa those 4 days ni ndege - its real camping life - ni kama vile Maisha plus

Hahahah umenchekesha mno kwa hili angalizo
 
Mwenye macho haambiwi tazama, kilimo au njia mbadala nyingine za kipato kwanza ajira badae.
 
mkuu ELNINO ninaomba feedback,je ulichoplan kimetokea? Je by 2015 ulikua tayari milionea, kama ulishndwa, ni changamoto gan zilikuzuia, kama ulifaulu ni kwa techniques gan? Plz naomba tueleze
 
Wakuu habari.

Vipi kuhusu kilimo cha mahindi maeneo ya msowero- Kilosa kwa kuwa naskia kuwa kuna maeneo makubwa kwa ajili ya kilimo lakini bado hayajachanagamkiwa na watu.

Mwenye taarifa sahii kuhusu upatikanaji wa maeneo na hali ya hewa ya eneo hilo atujuze.
 
Wadau naomba kujua udongo wa mfinyanzi mweusi tiii kama unafaa kwa mazao ya mahindi, maharage, etc na miti kama graveria etc. Naomba kujua kama unafaa kununua!
 
Kuna wataalamu ambao hupima udongo wa shambani ili kujua unafaa kwa kilimo kipi. Kwa uhakika zaidi na ili upate mazao yenye ubora ni bora uwatafute hawa watu. Kwa hapa TZ sijui wanapatikana wapi.
 
In general udongo wa mfinyanzi ni mzur kwa mahindi. Tatizo huu udongo ukikosa maji mahind yanadumaa maana mizizi hushindwa kukua. So kama unataka kulima kwenye mfinyanzi hakikisha maji ypo ya kutusha. Hta ivyo unaweza weka mbolea ya samadi, ngurue au ya kuku ambayo husaidia kuchambua udongo.
 
Niko sambamba na Heradias,
Mfinyanzi ni udongo wenye rutuba kuliko aina zote za udongo.

Lakini unachangamoto kuu mbili
1-Mfinyazi kama kutatokea kukosekana kwa mvua yaani mvua kua uhaba,mfinyanzi unakua mgumu mno kiasi ambacho huathiri mazao.

2-Mfinyanzi kukitokea mvua nyingi nao unatabia yakutokupenyeza manyi kwenda aridhini kwa haraka hivyo kutuamisha maji jambo ambalo mahindi na maharage huathirika.

Hivyo mfinyanzi huhitaji mvua za wastani ili mazao yamee vizur
 
Niko sambamba na Heradias,
Mfinyanzi ni udongo wenye rutuba kuliko aina zote za udongo.
Lakini unachangamoto kuu mbili
1-Mfinyazi kama kutatokea kukosekana kwa mvua yaani mvua kua uhaba,mfinyanzi unakua mgumu mno kiasi ambacho huathiri mazao.
2-Mfinyanzi kukitokea mvua nyingi nao unatabia yakutokupenyeza manyi kwenda aridhini kwa haraka hivyo kutuamisha maji jambo ambalo mahindi na maharage huathirika.
Hivyo mfinyanzi huhitaji mvua za wastani ili mazao yamee vizur

Je Unafaa kupanda miti kama tiki,graveria, please
 
Je Unafaa kupanda miti kama tiki,graveria, please
Hapo siwezi kupasemea kwani panahitaji vipimo lakini labda nitaeleza kwa namna ambavyo nimetizama mitiki mingi nilioiona imepandwa kwenye udongo mfinyanzi kanda ya pwani.

Kimsingi nimeona ikikua kwa shida sana.Ila nafikiri tatizo hapa si udongo ila ni hali ya hewa.Tizama iringa ndio mkoa unaozalisha miti ya mbao kwa wingi.Hali ya hewa ya iringa ni ya baridi sana,hivyo nafikiri hali ya hewa pia ni jambo la msingi sana kwenye umeaji wa miti.

Hivyo nafikiri mfinyanzi si tatizo kwa matiki nahisi huenda hali ya hewa.
Mwisho ningeshaur kama unaweza kufika kwa wataalum wa agriculture kama chuo cha SUA ama pale ambapo papo karibu nawe.
 
Hapo siwezi kupasemea kwani panahitaji vipimo lakini labda nitaeleza kwa namna ambavyo nimetizama mitiki mingi nilioiona imepandwa kwenye udongo mfinyanzi kanda ya pwani.
Kimsingi nimeona ikikua kwa shida sana.Ila nafikiri tatizo hapa si udongo ila ni hali ya hewa.Tizama iringa ndio mkoa unaozalisha miti ya mbao kwa wingi.Hali ya hewa ya iringa ni ya baridi sana,hivyo nafikiri hali ya hewa pia ni jambo la msingi sana kwenye umeaji wa miti.
Hivyo nafikiri mfinyanzi si tatizo kwa matiki nahisi huenda hali ya hewa.
Mwisho ningeshaur kama unaweza kufika kwa wataalum wa agriculture kama chuo cha SUA ama pale ambapo papo karibu nawe.
Asante sana. Na kweli pwani mitiki inakua kwa shida. Tanga hapa ni vile vile haina afya. Nashukuru sana. Ubarikiwe
 
Back
Top Bottom