Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

09e33ae8f62873cdf7816cc3292eb107.jpg

Inawezekana hiyo hapo mie nafanya mkuu na inalipa

Hongera sana mkuu, unalimia wapi? Na maji unachukulia wapi mbona sijaona source yako ya maji unapochukua?
 
wekeni info za kutosha tuone uhalisia na pia cost zake na challenges
Kuna watu nimekuwa nikiona matangazo yao kuwa wanafunga hizi irrigation system, ila nashangaa hapa siwaoni aiseh.
 
Jaman mwaka huu nimejipanga kulima kiteto lakn bado sina taarifa za kutosha japo mwezi ujao nitaenda kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu lakn kabla sijaenda huko ningepnda kupata taarifa zozote za awali ambazo zinaweza kunisaidia kuandaa bajeti ikae vizuri na kujiandaa kwa lolote.

NINGEPENDA KUJUA YAFUATAYO;

  • Bei ya kukodisha ekari moja
  • Bei ya kulima kwa maana ya kuandaa shamba, kuotesha, kupalilia na kuvuna
  • Kiteto ni kubwa hivyo ningependa kujua maeneo ambayo ni mazri (ardhi haijachoka sana)
  • Aina ya mbegu inayokubali yaani ya mda mfupi mana naambiwa tayr msimu wa mvua ni mmoja tu( hapa ningepata mtaalam wa kilimo itakua vizuri zaidi)
  • makadirio ya mavunokwa ekari moja
  • Ushauir mwingine wowote ambao unaona utanisaidia kufanikisha suala langu pia nikipata contact za afisa kilimo huko kiteto nitashukuru sana.
 
Jaman mwaka huu nimejipanga kulima kiteto lakn bado sina taarifa za kutosha japo mwezi ujao nitaenda kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu lakn kabla sijaenda huko ningepnda kupata taarifa zozote za awali ambazo zinaweza kunisaidia kuandaa bajeti ikae vizuri na kujiandaa kwa lolote.

NINGEPENDA KUJUA YAFUATAYO;

  • Bei ya kukodisha ekari moja = 30,000 au gunia moja baada ya kuvuna
  • Bei ya kulima kwa maana ya kuandaa shamba, kuotesha, kupalilia na kuvuna = kulima 25,000 - 32,000; kupalili 15,000 - 20,000; kuotesha 10,000
  • Kiteto ni kubwa hivyo ningependa kujua maeneo ambayo ni mazri (ardhi haijachoka sana) sina hakika na hili itabidi utafute mwenyeji akusaidie zaidi.
  • Aina ya mbegu inayokubali yaani ya mda mfupi mana naambiwa tayr msimu wa mvua ni mmoja tu( hapa ningepata mtaalam wa kilimo itakua vizuri zaidi)
  • makadirio ya mavunokwa ekari moja = Gunia 10 kwa eka, pia hii inategemea na aina ya mbegu uliopanda na shamba
  • Ushauir mwingine wowote ambao unaona utanisaidia kufanikisha suala langu pia nikipata contact za afisa kilimo huko kiteto nitashukuru sana. Usiende kichwa kichwa huko kama huna mwenyeji, zaidi watakukodishia mashamba yaliyochoka. na kama unapesa ni bora ukanunua pori ukaanza kulisafisha, hapo utakuwa na uhakika wa shamba unalolilima.

Sio kwamba nakukatisha tamaa ila, suala la afisa kilimo sahau maana hawatakusaidia, kwani hata wao hawajui.

Anagalia majibu yangu hapo juu kny rangi ya bluu yatakusaidia.
 
Kaka nashukusuru sana kwa mchango huu hapa ni mwazno mzuri Mungu akusaidie
 
JF

Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.

Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.

Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.

Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.

Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m by July this year.

Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.

Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh

By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe. by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. Sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.

This is a challenge to you JF - hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.

Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.
hey now it's 2016... how abt ur success? wakati huo nilikua form one now nipo chuo nataka kujoin kweny kilimo... is it too late ?????
 
Naomba kujua ivi kipi kinafaida, kuuza mahindi mabichi au kuuza makavu?
 
Mkuu MTOTO YATIMA vipi mpaka sasa umefanikiwa kupata taarifa kiasi gani? Mathalan aina ya mbegu ifaanyo kwa maeneo ya kiteto. Mwezi huu wa 12 ntatia timu huko kiteto kupiga kazi. Tutafutane mkuu
 
JF

Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.

Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.

Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.

Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.

Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m by July this year.

Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.

Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh

By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe. by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. Sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.

This is a challenge to you JF - hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.

Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.
Mkuu hebu tusaidie updates ulipofikia kiongozi
 
chardams nami naulizia kilimo cha umwagiliaji huko kiteto. Tunasubiria majibu. Alafu naona uko vizuri katika ufafanuzi wako. Mungu akuzidishie
 
Mtoto ya Tima hongera sana kilimo kinalipa. Haswa ukikodi hecre nyingi at least kwanzia 50 na kwendelea. Sasa mi shida yangu kiteto yiko kwenye kumwagilia
 
Back
Top Bottom