Nimeamua Kustaafu Rasmi JF, Utangazaji na Uandishi wa Habari Baada ya Kuhudumu Miaka 30. Niko Free Kujiunga Siasa, Nimejiunga CCM na Nitagombea Ubunge

pale uliposema pango la kibanda chako ni kama mshahara wa DC ndo nikastuka unatuchota akili
 
Haiwezekani Polepole akakosekana kwenye issue kama hii, hata akiwa mbinguni atawaaga malaika na kushuka kuja kupokea njuka wa CCM na makamera
 
Nenda kalambe miguu baada ya kutokuteuliwa kwa mda mrefu pamoja na masifa kwa serikali yako katili
Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😃😝😝😝😝😝😝😌



 
Paskali
Hii saa nne ndio imeniacha mdomo wazi, maana najua mizaha ya siku ya wajinga, mwisho wake ni saa nne. Je ni coincidence?
Kila la heri katika safari yako, kokote uendako.
 
All the best kwa kustaafu uandishi na JF kwa ID ya Pascal Mayalla. ila hatuwezi kukumiss kwa ile ID yako nyingine
 
Inashangaza kama sio kustaajabisha kuona wengi wetu huku hatusomi mada bali tunakimbilia kureply.wengine wanamshambulia mleta mada bila kujali hoja alizoweka kwenye Uzi

Unawezaje kusema Uzi umeandikwa kwa sababu ya fools day kama umesoma Uzi line baada ya line .hakika huwezi kuwa na mtazamo huo labda iwe huwezi kufikiri nje ya boksi.Au uwezo wako mdogo kumuelewa mleta mada mambo yote aliyoyabainisha

Fools day imetumika kama mwavuli wa kujifichia wakati akiwararua wanasiasa na vyama vyao.mtoa mada amegusa pande zote mbili.upande wa pinzani ameulezea vizuri bila kupepesa macho ni ukweli unaouma kuhusiana na alichokieleza .hakuna upinzani madhubuti wenye kuonyesha kuitoa ccm madarakani na kushika dola..namalizia hapo nisizidi kutia chumvi kidonda ambacho bado kibichi hata Mimi linanigusa kwa upande wangu

Katika sababu kumi alizowasilisha mtoa mada nyingi zimelenga kuonyesha ubaradhuli wa ccm na serikali ya awamu ya tano. Rejea sababu ya kwanza kwanini anajiunga ccm "eti ni kwa sababu ni chama chenye hati miliki ya kutawala hii nchi milele"teh teh teh huu sio utani jamani hilo dongo kwa wenye chama chao ..Yaani ccm kutawala nchi ni Sawa na vitabu vitakatifu havibadilika kamwe.ndio akili zao zinavyowatuma sijui inawezekanaje?

Kuna mahali anasema yeye anajua hataongoza kwenye kura za maoni hivyo anajua atateuliwa kuwa mgombea wa jimbo kwa sababu ya ukabila .kwamba yeye na mwenyekiti wa ccm wametoka mkoa mmoja hii inatuonyesha ukabila unavyofanya kazi kwenye ccm bila kujali haki za wanachama wake..ukabila kwanza mengine yatafuata

Rejea baada ya kuuliza swali ikulu nini kilifuata kwa mtoa mada.tenda zake zote mirija ilikatwa na kuachwa mtupu. Hivyo akaamua kupunguza wafanyakazi kutoka ishirini mpaka watano na kurudi news room akiandika makala katika magazeti.unadhani huko news room ndio alikuwa salama huko pakampeleka mpaka ofisi ya bunge kuhojiwa..kuanzia hapo habari ya news room ikaishia dodoma kwenye ofisi ya bunge sasa amekuwa ni mtu wa kuunga unga kutokana na madhila aliyofanyiwa na serikali ya wanyonge..kiufupi huyu mwamba wamemnyoosha na pasi ya mkaa mpaka mtaani wanamwita pasko Manjaa

Mtoa mada ameandika mengi sana siwezi kusummarize yote ila tusipuuzie hili andiko kuna jumbe nyingi zimefikishwa kwa njia ya fasihi.kwa wale wapenzi wa forex wanaelewa forex is not for everyone.sio lazima kila mtu lazima atatrade wengine itawashinda tu..mabandiko ya paskall sio kila mtu anaweza kuyaelewa kuna watu wake anaowalenga na ujumbe unawafikia barabara...pole sana mtoa mada kwa unayoyapitia japo kuna joking ndani yake



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku ya wajinga duniani

Naona wajinga wote wanasherehekea sikukuu yao ikiwemo wew mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…