Nimeamua Kustaafu Rasmi JF, Utangazaji na Uandishi wa Habari Baada ya Kuhudumu Miaka 30. Niko Free Kujiunga Siasa, Nimejiunga CCM na Nitagombea Ubunge

Mkuu umeamua kuonesha rangi yako halisi baada ya muda mrefu wa kuishi kwa mashaka na kuficha ficha ili usionekane wa kijani.
wajanja tulimng'amua toka kitambo sana kupitia nyuzi zake. angalau sasa amekiri japo jina lake mmh. haya kila la kheri kwake!

kumbe kugombea ubungr yataka pesa sio chenji!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna cha leo ni siku ya wajinga au wajanja, anayo sema pascal ni maneno toka moyoni mwake kabisa,,,...., yule kamanda alituambia kuwa pascal ni gamba lilikomaaa kabisa, ona sasa...
 
"Sababu ya 5 na ya mwisho ni lisemwalo, lipo kama halipo linakuja. Japo mimi ni Msukuma, na jina langu la ubini ni Mayalla, siku zote nimekuwa nikielezwa na Wasukuma wa Ukweli maana ya jina Mayalla kwa Kisukuma ni ukame, drought unaosababisha famine, baa la njaa, lakini siku hizi kuna Wasukuma wa aina nyingi nyingi wengine ni wakuja tuu hivyo hata maana ya jina la Mayalla linabadilika badilika kutegemeana na Msukuma wa wapi. Toka siku ile nilipouliza lile swali Ikulu nikajibiwa kuwa Mayalla kwa Kisukuma ni Njaa, kiukweli kauli nyingine huumba, tangu nilipoitwa Njaa, kauli ile ikaniumbia njaa ya ukweli, hadi jina langu humu na mitaani ninaitwa Pasco Manjaa!. Baada tuu ya swali lile, contracts zangu zote za kampuni yangu ya PPR za serikalini zilisitishwa hivyo njaa ikaanza kunitembelea, tenda za maonyesho ya Saba Saba zikafutwa, tenda za kuandaa kipindi vya elimu kwa umma zikafutwa, ile ofisi yangu jengo la NHC pale Mtaa Mkepu niliokuwa nalipia pango sawa mshahara wa DC nikafunga, nilikuwa na wafanyakazi 20, nikawapunguza 15, tukabaki 5 na kuhamia kwenye kaji chumba jengo la Posta House. Kwa kwa vile mimi ni mwandishi wa habari, baada ya kufungiwa huko kote nikaamua kurejea newsroom kuandika makala za magazeti nako ndio vile tena nikaitwa Dodoma kuhojiwa na Kamati ya Bunge. Kila ninachogusa hakiendi. Sasa limeingia hili janga la Corona, ndio kabisa, hakuna kazi kabisa, ofisi nimefunga niko home sina hili wala lile ndipo likanijia hili wazo la kujiunga CCM na kugombea ubunge ili sasa nikawatumikie watu. Mtaji wa ubunge nimeamua kuuza kila kitu changu, kuanzia nyumba, na kila kitu kilichomo, magari, na container lililosheni mali za thamani kubwa. Kwa kuanzia nahitaji just 15M za hizo items. Nikipitishwa naiuza hiyo nyumba Thamani yake TZS 900. Mila mimi nitauza kwa TZS 500.M. Hii ndio fedha ya kampeni, Msimamizi wa Uchanguzi nimemtengea, 100M kuwapiga pingamizi wagombea wengine wote, 100M ya michango mbalimbali, 100M nakichangia Chama, 100M ya logistics na 100M ya akiba. Politics is science, political science na politics is business, you invest na zinarudi na ku multiply three fold."
Mr P nadhani hii namba 5 ndio bandiko lako la leo, nimepanda jinsi ulivyolijaradia na issues nyingine ili kupoteza maboya au wasiojulikana kubisha hodi kwenye hekalu lako la TSH 1b...nice art work..30 years experience imejionesha
 
Nilikuwa nimeamini ulichoandika, ila nilipofika pale unaeleza mgao utakaotoa kwa watu mbalimbali, nikaona hii ni Aprili mosi. Lakini kwa vyovyote vile, kuna ukweli mwingi sana umeieleza, pamoja na mengi yakuhuzunisha.

Kwamba lile swali la ikulu limekugharimu kiasi hicho. Pole sana mkuu. Sasa leo nimekuelewa vizuri. Mara nyingi nimekukosoa sana. Wewe unajitambulisha ni nani. Sisi tumejificha. Ndio maana wewe kwa kile unachoandika, unawajibika, na unaweza kuitwa na kamati ya bunge au mamlaka zingine. Wewe ni shujaa wa kweli. Na unapata mateso kwa ushujaa wako. Hongera sana.
 
Pia Mr P anasema kuna wasukuma halisi na wakuja, ambao bila Shaka ndio waliotoa tafsiri ya Mayalla njaa...bandiko lake ni kama kurusha jiwe gizani.
 
Nimegundua kumbe wajinga ni wengi sana nilisubili nione utapata wajinga wangapi mpaka kufikia muda huu ushapata wajinga wengi sana hongera kaka Pascal Mayalla
 
Huo ni uamuzi wako wewe familia yako hasa hasa mkeo, Kwetu sisi si muhimu kujua mambo yako..!!
Tuna mambo muhimu ya kitaifa ya kufanya na si kujua who has gone where politically.... so what?

Hata hivyo Covid 19 ishapata dawa rasmi na magonjwa wote wameshaanza kutumia na nusu wameshapona kabisa.
 
It was written clearly in your contributions and postings in this forum. You prepared well bro bravo and good luck
 
Tangu asubuhi naogopa kuchangia lolote maana nilikuwa naona kama hoja imenizidi nguvu na nakosa lakufanya.

Sasa wewe umenisaidia sana. Amaa kweli @pascalmayala ni fundi kwenye tasnia ya habar

Sent using Jamii Forums mobile app[/USER]
Ndugu yangu hata Kama ni Mimi naamua tu kuwa timu home boy, kibinyo kisikie kwa wengine sio kwako. Nimeumia kuona hili suala la pascal mh alilichukulia uzito kias kile wakati ndg yetu alikuwa katika kutimiza majukumu yake😥
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…