Nimeamua Kustaafu Rasmi JF, Utangazaji na Uandishi wa Habari Baada ya Kuhudumu Miaka 30. Niko Free Kujiunga Siasa, Nimejiunga CCM na Nitagombea Ubunge

Poa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
jamani mnisaidie sasa wakuu, mbona mimi nimemuelewa tofauti kabisa bwana pascal tofauti na wenzangu!!?
pascal ameishia kuinanga ccm kisanii, tu na mwishoni amehitimisha alichomaanisha.
 
Wait! WooooWooooWhat?!
Kwani kuwa mbunge kunakuzuia nini kuendelea na Uandishi Uporojo na mengineyo!
All the Best Mkuu!
 
Hata hivyo Covid 19 ishapata dawa rasmi na magonjwa wote wameshaanza kutumia na nusu wameshapona kabisa.
Duh..!. Kumbe Corona imeishapata tiba rasmi na watu nusu wameisha pona!. Hii ni taarifa nzuri hivyo basi sasa naendelea kumtafuta Polepole taratibu huku humu jf nikiwa bado nipo nipo tuu.
P
 
Nahisi saikoloji yako ni ndogo sana ulichokiandika sawa na mtoto darasa LA nne LA zamani. Sasa sielewi kama umesomea vyuo vya kata kama vipo, au hujasoma kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Magashashi, mimi sio nimesomea vyuo vya kata, bali sijasoma kabisa, niliishia darasa la 7 tuu la enzi za UPE, hivyo uko vey right, saikoloji yangu ni ndogo sana sawa na mtoto darasa LA nne LA zamani.

Watu humu tunatofautiana viwango na uwezo wa uelewa, kama mimi nimeishia la 7 tuu, halafu wewe kiwango chako cha uelewa ni kiwango cha darasa la 4 la zamani, ukisoma andiko hata la professor wa Ph.D, kite utakachoweza kukielewa ni kile tuu cha kiwango chako cha uelewa. Hivyo hata hii mada yangu ya darasa la 7, mtu wa kiwango cha uelewa cha darasa la nne, ataelewa kwa kiwango chake. Asante kwa kunielewa kwa kiwango hicho. Mambo ya viwango haya ni kila mtu na kiwango chake, cha muhimu ni uwezo wa kusoma na kuelewa, ukiwa ni mtu wa kiwango cha uelewa wa darasa la nne la zamani, ukakutana na mada ya kiwango cha uelewa cha darasa la saba kama hii, lazima utatoka kapa.
Pole.
P
 
Jana yote nilikuwa busy kiasi sijuweza kuingia JF na kuiona thread hii ya mzee mwenzangu Pascal Mayalla.
Hakika imeandikwa kwa ufundi mno na mjadala wake ulipaswa uishie Jana SAA 4 asubuhi au uchukue sura mpya sio hii ya sasa.
Hapa hakuna cha ubunge wala nini, hapa ni Polepole na ccm wamegongwa za USO mchana kweupe na huyu waliye msababishia "NJAA".
Na kwa wale wanao mhukumu Pasco kwa kuuliza swali mkidhani ni statement msije mkafanya hivyo kwenye hilo swali na 11, " jee kujiunga ccm ni ujinga?"
Ujumbe wa thread hii ni mkubwa sana kuliko wengi wafikiviavyo, nitarudi baadae kuujadili.
Muda huu naona mama Yeyoo kama vile kuna jambo anahitaji naweka simu pembeni kwanza. Naweza kuchelewa hapa hata mazoezi ya SAA 12! [emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu huwa wanapata shida sana kumuelewa huyu jamaa..nashkuru huwa namwelewa sana na kila mada anayoianzisha humu ukiisoma kwa kutafakari mstari kwa mstari unaweza ukajikuta unacheka maana huwa anafikisha ujumbe kwa style ambayo si rahisi akili ndogo kumwelewa!
Bandiko la Paskal hata kama ni la utani lakn ndani yake kuna kuwa na ujumbe mzito sana! Hata bible ukiisoma utaelewa maandishi yanasomekaje lakn ni ngumu kuelewa kilichokusudiwa! Hongera sana mkuu kwa hakika haya mabandiko yako yanadhihirisha ubobevu wako na unguli kwenye sanaa hii ya uandishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Nzwangendaba
  1. Msingi wa uandishi wa habari ni truthfulness, objectivity, impartiality na balancing. Ili mwandishi kuyatimiza hayo hupaswi kuwa member, mfuasi au mshabiki wa chama chochote na hivyo ndivyo mimi nilivyokuwa kipindi chote cha miaka 30 niliyohudumu kwenye sekta ya habari. Ukiisha jiunga na chama chochote cha siasa, lazima sasa uta take sides, mfano hakuna mwana CCM CCM yoyote anaweza kukubali kusema ukweli kuwa CCM ndio chanzo cha umasikini wa taifa hili uliosababishwa na sera mbovu zilizochochea rushwa, uhujumu na ufisadi karibu wote. Lazima niitetee CCM kwa kutousema ukweli kama huo. Huwezi kuwa objective wakati wewe ni sehemu ya tatizo, huwezi kuwa impartial wakati tayari ume take side, huwezi ku balance haki bin haki, lazima utaegemea upande wako. Lakini kufuatia dalili za kauli na matendo ya CCM ya Magufuli na Dr. Bashiru Ally Kakurwa, wanaonyesha kuirudisha ile CCM ya Nyerere ya tujisahihishe hivyo hii CCM ninayo azimia kujiunga nayo ni CCM mpya.
  2. Sijajihakikishia 100% ndio maana ninafanya maandalizi kwa phrases. Phase 1 inahitaji just TZS 15M za maandalizi. Jimbo ninalolimendea ni jimbo very lucrative hivyo ushindani wa jimbo hilo ndani ya CCM ni mkubwa. Wataibuka vigogo wa CCM wenye vipochi vinene. Kwa vile mimi najijua uwezo wangu wa kujenga hoja ni mkubwa ila uwezo wangu wa kiuchumi ni limited, kupitishwa kutategemea tunashindana na wakina nani na wana uwezo gani kujenga hoja na nguvu gani ya Kiuchumi, hivyo hapa karata kubwa ni ya kumtumia home boy wangu aliyeniita njaa na kunisababishia njaa itambidi anibebe kunifidia njaa alionisababishia. Nikipitishwa ndio nakuja phase 2 ya kuuza nyumba to secure TZS 500m za kampeni. Kwa political dynamics za siasa za Tanzania kwa sasa, mgombea wa CCM ndiye mshindi kila kona isipokua jimbo moja huku bara, majimbo mawili Zanzibar na majimbo yote Pemba. Ndio maana niliwahi kueleza haya Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums
  3. Kuwa Mbunge sio haramu kuwa jf . Kwenye andishi langu nimesema kuwa Mbunge ni kuwatumikia wananchi, lakini kwa Profile yangu, nitamsaidia sana Magufuli, kiukweli kabisa katika sekta yangu timu ya Magufuli iliyopo wanajitahidi sana lakini bado. Ni katika muktadha huo ndio nitasita kuchangia jf kama watangulizi wangu. Nitolee mfano wana jf watatu hawa niliowazungumzia hapa Baraza Jipya: Pongezi kwa JamiiForums, WanaJF watatu(VERIFIED) waukwaa uwaziri - JamiiForums hawa jamaa walikuwa wachangia wazuri humu, baada ya kuukwaa uliwaona tena humu?. Juzi kati baada ya ndio nilimuona mmoja wao akirejea kujibu hoja ili tuu kujiokoa na kuti kavu kule jimboni kwake, na tulipombana kwa maswali magumu bila kuacha loose ends alikimbia jumla!. Hivyo na mimi nafauata tuu nyanyo. Angalia kina Juliana Shonza, walikuwa very active members baada tuu ya kuukwaa.. kimya. Mbunge pekee aliyesemama na jf ni Zitto, hivyo sijui kama hawa wa CCM wanakatazwa au laa, nikaamua niage mapema tuu.
  4. Utoaji elimu kwa umma utaendelea lakini sasa sio kupitia mitandao ya kijamii bali sasa ni kupitia mainstream media na vyombo rasmi kama mule Bungeni. Baada ya uelimishaji umma kwa miaka 30 kupitia media, sasa muelimishaji umma anakuwa ameingia jikoni kwenye vyombo vya maamuzi na utekelezaji, hivyo sasa nakuwa ni mpishi kabisa wa elimu kwa umma.
  5. Hili la jf kunipa jina ni kweli, kuna wengi wanaitumia jf kama ngazi tuu ya kuikanyaga na kupandia juu, wakishafika huko juu, hawana tena time na ngazi, kama lilivyo dekio, . Siku wakianguka ndipo huikumbuka ngazi, na siku kukitokea ajali ya kunwagika soda mbele ya wageni ndipo dekio hukumbukwa. Kwa upande wangu, kwa muda mrefu kwa muda mrefu nililazimika kuishi double life, kwa vile mimi huwa ninafanya Radio, TV Programs na public appearances, I had to live double life ya Pasco wa JF ambaye ni very critical na Pascal Mayalla ambaye ni verified member, bringing the two together into one was a challenge. Hivyo kwenye Programs zangu nikipata fursa huwa naichomekea jf, nikimpata Max namwalika, nikipata fursa ya kuipaisha jf, naipaisha. Kwa vile mimi siko ndani ya CCM kujua ni nini kinachowafanya members wana CCM kuitumia jf kama ngazi tuu ya kupandio kule juu lakini wakiisha fika, jf hugeuzwa dekio, sijui kama wana katazwa, hivyo naitumia formula ya "when in Rome, do as the Romans does", ndio maana bado naomba support ya wana jf kunisupport kujiunga CCM, kunipigania niingie Bungeni, you never know usikute hao waliopo ni uoga wao tuu kutoendelea kuitumia jf baada ya kuula, lakini mimi nitakapoingia, tukajikuta naibeba jf na kuiingiza kwenye hansard and you never know tukajikuta tunaipandisha jf to unimaginable heights kwa kuingiza jf hadi ndani kabisa kule kunako. Just pray for support me in joining CCM and persue ubunge
P
 
Haaa Mayalla bwana,umesema una sababu kuu 7 sasa umeweka zaidi ya 7 au zingine ni ni kuu saidizi?
Ila sababu yako ya tano imejitosheleza .bilashaka bado hujampata polepole hivyo bado hujastafu rasmiiiiiiiiii
 
jamani viongozi wa JF hakikisheni pascal anakaa mbali kabisa na JF servers, siku pascal akipata access ya server za JF wengi wetu tutakwisha, wasiojulikana watatumaliza…………………ukisikia mtu anatamani kuhamia CCM kaa ukijua huyo siyo mwezio tena, tena mtenge kabisaa
 
Kaka unajua kuandika yaani makala zako huwa nazisoma sichoki,yaani navutiwa kusoma zaidi,unanikumbusha makala za miaka ya 2000 mwanzoni za Ndemacha na kaka yake kama sijakosea majina wakiandika tokea UK
 
Brother Pascal Mayalla nimesoma badiko, kuna wakati nikajikuta nacheka kwa nguvu, sijui kwa nini.Ila kwakweli wewe ni bonge la Bonge la muandishi, ninashukuru kubahatika kusoma maandiko yako.

Tatizo umeandika vitu vingi sana vya ukweli kutoka moyoni kwako, umesahau kuwa vitu vingine vya ukweli utakiwi kuvitoa moyoni inabidi wakati mwingine vibaki tu moyoni ikibidi tu ufe navyo.

Mchanganua wa ile M500 ya nyumba utakayo uza ndio umeniacha hoi kabisa.

umetumia falsafa ya juu sana kwenye huu uzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…