Nimeamua Kustaafu Rasmi JF, Utangazaji na Uandishi wa Habari Baada ya Kuhudumu Miaka 30. Niko Free Kujiunga Siasa, Nimejiunga CCM na Nitagombea Ubunge

mkuu, kooote ulikoandika ni sikukuu ya wajinga isipokuwa hii sehemu ya wewe kuwa na njaa kali..... huu ni ukweli halisia kwani njaa imekuwa ni common denominator kwetu wote isipokuwa Wakolomije & co!
 
Yote haya ni sababu ya woga. Na sio tatizo lako, tatizo ni Katiba yetu mbovu
 
Leo ni siku ya CCM yaani siku ya wajinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla Yaani siku ya wajinga ndo umeandika insha yote hii?Nimesoma kichwa cha habari pekee. Sijasoma habari yote maana mimi si mjinga. Ila why unapoteza time yako kuandika insha ndefu only to fool people ?
 
FOOLS DAY. Pascal bwana! Kawapata wengi!!
 
Kila la kheri kwa matarajio yako mapya; kumbuka LUMUMBA siyo tawi, uanachama hutolewa kwenye tawi na pili kabla ya kuchukua fomu ya kuomba uteuzi si vibaya ukawasiliana na Alfred Masako naye akupe uzoefu wake kwenye huo mchakato.

Narudia tena kila la kheri kwa matarajio yako mapya; tunakukosa sana humu JF hasa bashiri zako za mambo ya kisiasa
 
Bravo Pascal Mayala - leo ni siku ya wajinga na umewapata kweli! Wanafikiri ni kweli!
 
Leo siku ya waongo duniani, mjihadhari na baadhi ya hizi kauli, Pascal Mayalla mbona unawababaisha Watanzania wenzako, uache JF kisa unafuata ubunge? Mimi Mkenya hapa huwa napenda sana kusoma makala yako, acha hizo, kama kweli sio zuga la April fools day, basi hata ukiingia kwenye siasa usiache JF, endelea kumwaga nondo.
 
Pamoja na waliochangia wenzangu nililoliona ni moja lenye upungufu, pale ulipoandika nanukuu " Leo hii hii majira ya saa 10:00 asubuhi......"mwisho wa kunukuu.

Ulipaswa kuandika " Leo hii hii majira ya saa 09:59:59 asubuhi ......" kwasababu siku ya wajinga inaisha saa 09:59 :59 asubuhi, ikifika saa 10:00 asubuhi wote wana akili timamu.

Ikifika saa 10:00 asubuhi wasipo kuona watakushangaa, ila kama watakuuliza "mbona tumekusubiri hadi saa 09:59:59 asubuhi haujatokea?" Basi hao ndio wenye siku yao.
 
Du kwa mara ya kwanza kusikia mtu anaachana na proffesion yake. Nilizoea kujuwa kwamba ni kaburi tu humtenganisha mtu na utaalamu wake. Kila la kheri.
Hiyo siyo kweli,mbona bashiru kaacha kufundisha chuo kikuu?
Sema kuwa mayalla ameshindwa kujielewa kuwa hata kazi aliyokuwa anafanya jf na penginepo kupitia taaluma yake alikuwa akiitumikia nchi na wananchi

Tatizo la waafrika hasa watz %kubwa NI wanafiki na wanazandiki sana
mtanzania yeyote ishi nae kwa mashaka Sana na tahadhari kubwa Kama swala anavyoishi na Simba mwituni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…