Hongera mkuu, hata Mimi nilichukua uamuzi huo mgumu miaka miwili iloyopita nikaingia kitaani kujiajiri, sasaivi sitaki hata kuajiriwa tena labda nifilisike, cha msingi jitume kwa nguvu zako zote, kuwa na nidhamu kwa biashara utakayoianzisha hatakama itakuwa ndogo, ukiwaheshimu wateja wanaokuja kununua hiyo biashara utaongeza wengi zaidi, sasa kwa mtaji wa laki tano kama huendekezi usharobaro na kutaka kujionyeshaonyesha kwa mademu anza na genge hasa sehemu ambayo unaona watu wanafuata mahitaji mbali wawekee karibu, ni hayo tu mjomba