Wakuu baada ya mwaka jana mwezi wa tano kuamua kufanya biashara ya mchele na namshukuru Mungu inanilipa vizuri mpaka sasa.
Kipindi naanza biashara nilikuwa nipo mwaka wa pili chuo flani,na sasa nipo mwaka watatu nategemea kumaliza mwakani nihitimishe masomo yangu.
Lakini baada ya mwaka kumalizika nimefanya tathmini nikaona heli nifungue kibiashara kingine,ingawa katika hali yakawaida nikipiga mahesabu kwenye karatasi inanionyesha nitapata hasara lakini dhamira iliyopo moyoni inaniambia nitapata faida nisiogope kufanya.
Biashara yenyewe nikuwa nimefungua "Kibanda umiza,cha kuangalia mpira."
Baada yakuona watu wanaenda mbali kuangalia mpira halafu huduma wanayoipata wanalalamika mbovu na kila mechi wanalipia 1000.Ila mimi nimeamua kuliweka center flani hivi na nitaonyeshea kwa sh 700.
Je kwa wale wenye ufahamu na biashara hii wanaona ntatoboa kweli japo kupata ela ya kula na kulipa kodi ya chumba tu?.[/Mkuu hongera kwa kuthubutu, binafsi ningekushauri kwanza ustick kwenye biashara 1(mchele) ujiimarishe na kuitanua vzr ndipo ufikirie kudivesify. Pongezi sn mkuu. By the way nikuombe unipe abc za biashara ya mchele maana najiandaa kuingia huko ila bado cjapata mtu wa kunidadavulia zaidi. Ubarikiwe.