Nimeangalia debate ya Trump na Kamala. Hizi ndio takeaways nilizoambulia

Nimeangalia debate ya Trump na Kamala. Hizi ndio takeaways nilizoambulia

Huku gizani kwa watu unakuta wananchi wakimshukuru rais kwa barabara utafikiri ametoa pesa yake mfukoni wakati hawajui kuwa ni kodi zao. Huku kwenye mwanga kwa binadamu ukiwa rais ni lazima utoe huduma za kijamii kama elimu, afya, maji, barabara na hupaswi au hakuna wa kukushukuru
 
Trump anasema atamaliza vita ya Israel na Hamas, sasa ataimalizaje hapa ndio najiuliza,
Atamaliza kwa.kuhakikisha ,huo msikiti wa alaqsa, ni ama unabomolewa au waisrael wanaruhusiwa Rasimi kuabudi hapo.

Ikumbukwe, Trump ni anaamin Israel ni Taifa Teule la Mungu.

Ndiocmaana aliaamisha Balozi za Marekan kuzileta Magharibi ya Jerusalemi
 
TRUMP:
Anamshutumu Kamala kwa mfumuko wa bei uliopanda maradufu.

Anamshutumu Kamala kwa makosa waliofanya kupelekea vifo na uachaji wa silaha za vita kipindi wanaondosha jeshi Afghanistan.

Anamshutumu Kamala kwa sera mbovu ya uhamiaji na kutodhibiti mipaka kupelekea kuingia kwa wahamiaji wengi sana waliosababisha baadhi ya uharifu nchini Marekani.

Anamshutumu Kamala kuwa lack of competitiness yao ndio imepelekea kutokea kwa vita vya Russia dhidi ya Ukraine, Mgogoro wa vita kati ya Israel na Hamas.

Anamshutumu Kamala kuruhusu sana wa-China kuleta bidhaa na viwanda vyao Marekani kupelekea viwanda vya nchini kuwa affected angali wa-Marekani wanabanwa kufanya shughuli za viwanda huko China.

Anamshutumu Kamala kwa kuzuia Fracking.

Anamshutumu Kamala kuwa mkomonisti.

KAMALA:
Anamshutumu Trump kwa kutokuwa mungwana kutokana na historia ya kesi mahakamani, ubaguzi na udhalilishaji.

Anamshutumu Trump kwa kutaka kuwabana wanawake ilo wasipate haki ya kufanya abortion.

Anamshutumu Trump kwa uchumi mmbovu aliowaachia term yake na Biden.

Anamshutumu Trump kwa kusababisha na kichochea fujo zilizopelekea uharibifu katika jengo la Capitol.

Anamshutumu Trump kwa kuwa na urafiki uliopitiliza na wenye mashaka viongozi wa mataifa pinzani na adui.

Anamshutumu Trump kwa kuwa na sera za kulinda tu matajiri.

Anamshutumu kwa kuzuia wabunge wa chama chake wasi support plan yake mpya ya kudhibiti mipaka.

SERA ZA TRUMP:
Kuthibiti mipaka kuzuia uhamiaji holela.

Kufanya mass deportation ya wahamiaji haramu.

Kuzuia abortion za kiholela na kuruhusu ifanywe mapema mimba ikiwepo bado ni changa.

Kustopisha vita vya Russia dhidi ya Ukraine.

Kustopisha mgogoro kati ya Israel na Palestine.

Kupunguza mfumuko wa bei.

SERA ZA KAMALA:
Kuongoza wanawake wafanye abortion wanavyotaka kwa maana ni haki yao maana mwili ni wao.

Kujenga opportunity economy.

Kuimalisha biashara ndogo ndogo.

Kuongeza kodi kwa matajiri.

Soma pia: Marekani: Trump na Kamala watofautiana kuhusu Mdahalo

Ni mengi nimezungumza ila ni haya ninayoyakumbuka kwa sasa
Nashangaa kwamba Kamala hakumshutumu Trump kwa racial segregation!
 
sawa....tushaona debate nyingi za huko marekani
Sasa na sisi tunataka mdahalo wa wagombea wa kwetu sasa 😄

ova
HHaha utasikia anaumwa maara amepata ziara ya kwnda china
 
Huku gizani kwa watu unakuta wananchi wakimshukuru rais kwa barabara utafikiri ametoa pesa yake mfukoni wakati hawajui kuwa ni kodi zao. Huku kwenye mwanga kwa binadamu ukiwa rais ni lazima utoe huduma za kijamii kama elimu, afya, maji, barabara na hupaswi au hakuna wa kukushukuru
Inaumiza sana ndugu
 
Mambo ya kuteka na kuua wapinzani kule hamna!

..hakuna kuua wapinzani.

..ajabu nyingine ni Amiri Jeshi Mkuu na Raisi aliyeko madarakani kushindwa ktk uchaguzi na kulalamika kuibiwa kura.

..yaani ameshindwa kutumia watu wasiojulikana, silaha za nyuklia, na dola, kubaki madarakani.
 
Trump anasema atamaliza vita ya Israel na Hamas, sasa ataimalizaje hapa ndio najiuliza,
Trump sio vuguvugu, ni ama moto ama baridi. Ndio maana haumi maneno yuko too direct haongei kwa utaalamu wa kisiasa (uongo + ulaghai).

Trump akilazimisha vita ya Hamas na Israel iishe anakuwa serious. Anawaita mnakubaliana alafu ole wenu muwe vichwa ngymu. Akiamua vita ya Ukraine iishe inaisha, ni kuzungumza na pande zote wakakubaliana. Urusi ikubali vita iishe au ikatae Ukraine ipewe silaha nyingi kuliko sasa.

Ni kama alivyokubaliana na Kim Jong na akawa sawa na North Korea kwa muda. Au alivyoshindwana na Iran akamuua mkuu wa IRGC Jenerali Soleimani. Au alivyoshinikiza Wachina akaingia trade war.

Kwa Trump unaamua kusuka ama kunyoa. Kwa Biden au Kamala mnajizungusha na kujadiliana sana.
 
..hakuna kuua wapinzani.

..ajabu nyingine ni Amiri Jeshi Mkuu na Raisi aliyeko madarakani kushindwa ktk uchaguzi na kulalamika kuibiwa kura.

..yaani ameshindwa kutumia watu wasiojulikana, silaha za nyuklia, na dola, kubaki madarakani.
Wenzetu walistaarabika kitambo
 
Trump sio vuguvugu, ni ama moto ama baridi. Ndio maana haumi maneno yuko too direct haongei kwa utaalamu wa kisiasa (uongo + ulaghai).

Trump akilazimisha vita ya Hamas na Israel iishe anakuwa serious. Anawaita mnakubaliana alafu ole wenu muwe vichwa ngymu. Akiamua vita ya Ukraine iishe inaisha, ni kuzungumza na pande zote wakakubaliana. Urusi ikubali vita iishe au ikatae Ukraine ipewe silaha nyingi kuliko sasa.

Ni kama alivyokubaliana na Kim Jong na akawa sawa na North Korea kwa muda. Au alivyoshindwana na Iran akamuua mkuu wa IRGC Jenerali Soleimani. Au alivyoshinikiza Wachina akaingia trade war.

Kwa Trump unaamua kusuka ama kunyoa. Kwa Biden au Kamala mnajizungusha na kujadiliana sana.
Sasa kwajinsi anavyomkubali Putin, naiona Ukraine ikishindwa vita mapema ikiwa ataingia madarakani,
 
Back
Top Bottom