Nimeanza Biashara ya Kukopesha, naomba ushauri

Baada ya kusafisha kiwanja cha mchongo..
Muonekano wake na size unahitaji milioni 10 na zaidi kujenga nyumba ya kueleweka😒

 
Hii biashara ina changamoto sana usipokuwa makini unatapeliwa vizuri sana ukidhani unafaidika.

Huyu mtu ameniletea hati ya kiwanja isiyo yake akiwa anataka mkopo wa Tsh laki 5.

kama si uchunguzi na upelelezi ningeumia vibaya sana.

 
Dunia tambara bovu. Muwe makini mnaokopesha kama mimi
.....
huyu jamaa aliweka pikipiki bondi ambazo sio zake (za mkataba, yeye ni boda boda)

binafsi.mimi namdai 428,000
mwenzangu anamdai 1,050,000

kesi iko polisi na kwa mwenyekiti wa mtaa, tumeandikishana malipo mwisho tarehe 8.7.2022

vitu vyake vya ndani viko chini ya ulinzi na vinaelekea kuuzwa vyote

amedhaminiwa na mtu mmoja
 
Unakabidhi mtaji wako kwa watu, subiri muda kidogo utajua hujui. Bora ufungue genge ufanye biashara za kawaida. Sikia kukopesha, Mkopaji anaweza akaingia mkatabata wowote unaomnyonya ili mradi tu aipate hiyo ela, akishaipata utasubiri.
Mkuu usidhani hela zinaondoka kirahisi rahisi kwamba tunatapeliwa huku hatujajipanga.

kuna watu ni makonki hapa town kabla hujawaza.kumla kichwa yeye keshakuwahi.
 
Bodaboda ni wasenge wasenge sana
 
Hii biashara watu walitajirika sana enzi ya JK.
Ila kwa sasa hii biashara ukiifanya jiandae na maumivu.
Kwa sasa hali ya watanzania ni ngumu sana hali ya maisha imebadilika.
So ukifanya hii biashara utakuwa unagombana na watu kila siku,mtu haoni shida kuja kukudanganya ili umkopeshe hela ili mradi tu apate pesa ya kujikimu bila kujua hiyo pesa atailipa kwa njia gani.
Kwa hiyo fikiria mara 2 kabla hujaingia mkenge
 
Hela haitolewi kama mkojo mkuu.
Hebu fuatilia mtiririko wa T&C utaona kuna mikataba inafanyika
 
Hela haitolewi kama mkojo mkuu.
Hebu fuatilia mtiririko wa T&C utaona kuna mikataba inafanyika
Mkuu mtu mwenye shida huwa hajali hiyo mikataba,yuko tayari kuanguka saini yaani potelea mbali atajua mbele kwa mbele huko sasa usumbufu unabaki kwako mkopeshaji.
 
Mkuu mtu mwenye shida huwa hajali hiyo mikataba,yuko tayari kuanguka saini yaani potelea mbali atajua mbele kwa mbele huko sasa usumbufu unabaki kwako mkopeshaji.
Rejea nyuma kwamba ninashika vitu bondi vyenye thamani mara 2 mpaka 3 ya mkopo.

usumbufu nautoa wapi wakati mkataba ukiisha sioni malipo napiga bei mali ya mdaiwa😅😅😅
 
Ushauri wangu ni bora uji dalalie tu mkuu!
Yaani ununue bidhaa kama ardhi kisha ifanyie udalali Itakulipa sana kuliko kufanya biashara ya mikopo tena na akina mama mtaji utakata mkuu
 
Rejea nyuma kwamba ninashika vitu bondi vyenye thamani mara 2 mpaka 3 ya mkopo.

usumbufu nautoa wapi wakati mkataba ukiisha sioni malipo napiga bei mali ya mdaiwa[emoji28][emoji28][emoji28]
Sawa nimekuelewa.
Ila kuwa makini sometimes unaweza kukabidhiwa vitu vya wizi ukaingizwa mkenge.
 
Kaka biashara inaendaje....?
 
Jifunze sheria na kuwa na porojo nyingi wasije kukuzidi kiswahili
 
Baada ya kuacha unauwakika na PEPO?
Asante
 
Kiongozi piga KAZI kanyaga twende.
Eti pepo!! Wakati zambi zingine wanatenda kama kawaida tu.


Kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…