Hongera sana kwa kuthubutu kuanzisha mradi wa kuku wa kienyeji. Idadi uliyoanza nayo nadhani ni nzuri ila unahitaji jogoo mwenye uwezo mzuri wa kupanda. Mimi siyo daktari wa mifugo lakini ni mfugaji wa kuku kideli ni rahisi sana kuki kinga kwa chanjo ya kideli and newcastle lakini wakisha anza kusinzia ni nadra kufanya lolote. Nimesoma kitabu fulani cha shirika linaitwa KIMKUMAKA wanashauri kutumia muarobaini kutibu kideli. Jaribu kutwanga muarobaini loweka kwenye maji na chija machicha kisha wapatie wanywe. Kwakuwa ni chungu, siku ya kuwapa muarobaini hakikisha siku hiyo unawapa chakula bila maji na wapatie maji ya muarobaini baada ya kuwa wamepata kiu sana.
Wape wote dawa hata wale ambao hawajaanza kusinzia. Ukijaribu chanjo ya kideli sasa hivi usije shangaa wakafa wote. wakisha pona wapatie chanjo ya kideli walao mara 3 au 4 kwa mwaka, utafurahia mifugo yako. Pia usisahau dawa ya monyoo. Hongera sana na kila la kheri.