Nimeanza kulipwa laki 3 kwa mwezi nianzishe biashara gani?

Hivi nyie mnawezajewezaje, yani mshahara wa 300K unataka uanzishe biashara hapohapo kwenye 300k kwa mwezi?, nauli, chakula, mavazi, other expenses cjui bili ya maji, umeme, bdo mbususu haijaenda saloon. Hapo hujaenda kupanda juu meza kitambaa cheupe. Kha!
 
Sio rahisi nilijinyima tu nikakamilisha lengo mean kwa mahahara wa 300K ninakufanyia Savingi ya zaidi ya 100K kila mwezi na nyumbani nasaidia vilevile
Mkuu ebu toa maelezo yote Kwa kujitambulisha .then utuambie ulianzaje maisha Kwa iyo 200k,
1.kodi,
2.chakula,
3.mavazi
4.matumizi Kwa siku.
5.nauli
6.
7.
 
10k ndo ulikua unakula mwezi mzima? Ji mwaka gani uo?
Nikkweka details zote za lifestyle hapa itakuwa rahisi kujulioana ila simple sehemu napofanya kazi ni sehemu ghari Sana kwa TZ mzima chakula wali tu hupati chini ya 2500 mlo mmoja bila kinywaji ila naweza ku-manage kula mlo mmoja kwa 500 Tzs tu ambayo sawa na 10,000 Tzs kwa Mwezi mzima
 
Mkuu ebu toa maelezo yote Kwa kujitambulisha .then utuambie ulianzaje maisha Kwa iyo 200k,
1.kodi,
2.chakula,
3.mavazi
4.matumizi Kwa siku.
5.nauli
6.
7.
Hapo nimetoa mfano mfano Mimi ndio Nina 300K kwa Mwezi ninaweza save Hivyo ila naweza kukupa hesabau pia ukitaka hio 200K natumiaje ona umeandika mavazi 😂😂
 
Hivi Mkuu hujui tatizo la Ajira na Mitaji lilivyo Dunia ya sasa mpaka unaandika hivyo mtu unakaa huna ajira miaka 7 unaishi kwa kuungaunga ukipata 300K unasemaje huwezi hizo zitakuwa nyodo kwasabu hakuna njia nyengine ujue
 
Weka akiba angalau 30k Kila mwezi,usijinyime sana ukapata magonjwa ya afya ya akili.
Ni kweli angalau hio 30 maana mambo n mengi tena kama yupo dsm aisee n hatari usafiri kodi chakula.
 
Usikimbilie kujitegemea
Epuka kutoa misaada kwa ndugu utavyojiingiz kuwasaidia watajenga utegemez
Weka akiba
Kuwa mchapakaz
Tuliza akili angalia mazingra yako anzisha jambo na hakikisha unauwezo wa kulisimamia ata 35% (kila siku ufike kwenye jambo lako la biashara )


Nakutakia kila la Heri
 
Vibiashara vya hapa na pale mkuu.
Tafuta kijana unae muamini mpe mtaji wa biashara ya kuzunguka nayo. Maji,karanga,juice,soda ice cream. Halafu weka nae makubaliano ya 50% ya mauzo baada ya kurejesha hela ya mtaji.
Mfano:- mtaji 50,000 mauzo mwisho wa siku 70,000 unatoa hela ya mtaji 50,000 halafu inabakia 20,000 hii mnagawa 50%. Ndani ya wiki mbili unaongeza kijana mwengine na mwengine. Miezi 3 una vijana 10 kila kijana akikupa 50%(10,000) kwa siku una 100,000. Kabla hujafanya hili fanya utafiti wako mwenyewe zaidi.
 
30K saving kilamwezi sio saving ni kupoteza muda yaani ni sawa na 300K kwa mwaka mzima nonsense

Mshahara wa 200K Mimi niliweza save hio 300K kwa miezi miwili tu
Ulikuwa unakula sh ngapi?

Kodi sh ngapi?.
 
Tuliza kichwa pitia idea zako zote za biashara ulizokuwa nazo kabla ya kupata hio kazi, kama umezipoteza au hukuwahi kuziandika basi tuliza kichwa usikurupuke kukimbilia wazo utakalo pata

zingatia kufanya saving ,usilizike na mshahara wako majukumu yakianza utaona mdogo sana huo.
 
Nilishajitegemea kabla sijapata hii ajira
 
siwezi kujinyima kisa nisave for tomorrow!, ntafanya matumizi yangu yote kwanza, kama kutakua na surplus ndio nitasave, kama hakuna surplus, saving cant be my priority.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…