Nimeanza kulipwa laki 3 kwa mwezi nianzishe biashara gani?

Nimeanza kulipwa laki 3 kwa mwezi nianzishe biashara gani?

Tafuta kijana unae muamini mpe mtaji wa biashara ya kuzunguka nayo. Maji,karanga,juice,soda ice cream. Halafu weka nae makubaliano ya 50% ya mauzo baada ya kurejesha hela ya mtaji.
Mfano:- mtaji 50,000 mauzo mwisho wa siku 70,000 unatoa hela ya mtaji 50,000 halafu inabakia 20,000 hii mnagawa 50%. Ndani ya wiki mbili unaongeza kijana mwengine na mwengine. Miezi 3 una vijana 10 kila kijana akikupa 50%(10,000) kwa siku una 100,000. Kabla hujafanya hili fanya utafiti wako mwenyewe zaidi.
Nashukuru mkuu!
 
Ulikuwa unakula sh ngapi?

Kodi sh ngapi?.
Kodi 25K sawa na around 700 Tzs/Day na kula 1000/Day usiku lunch ni 500 Tzs ambayo nimeweka Bill mwezi mzima

Nauri job kuna pesa fulani mfano unatakiwa kutoka kariakoo mpaka Posta kufikisha documents nauri 1000 sipandi bajaji natembea kesho itatumika hio Kama nauri....
 
Jitahidi kuweka akiba, ikifika mil 3 njoo tusaidiane kumwagilia moyo hapa duniani wapitaji tu
 
siwezi kujinyima kisa nisave for tomorrow!, ntafanya matumizi yangu yote kwanza, kama kutakua na surplus ndio nitasave, kama hakuna surplus, saving cant be my priority.
Then 300K ndio itakuwa kipato chako mpaka unazeeka utataabika kihasi gani.
 
Kwanza utuambie unaishi kijiji gani?

Usikute mshahara lkn 3 misheni town 2m. Hapo mkuu unaacha mshahara wote km akiba
 
30K saving kilamwezi sio saving ni kupoteza muda yaani ni sawa na 300K kwa mwaka mzima nonsense

Mshahara wa 200K Mimi niliweza save hio 300K kwa miezi miwili tu
Hapo kwenye 300k , mtu mwenye u serious hata 200k kwa kila mwez ana save
Hapo unaachana na matumizi yote yasiyo ya lazima, mademu nao unawaweka pembeni
 
Hivi nyie mnawezajewezaje, yani mshahara wa 300K unataka uanzishe biashara hapohapo kwenye 300k kwa mwezi?, nauli, chakula, mavazi, other expenses cjui bili ya maji, umeme, bdo mbususu haijaenda saloon. Hapo hujaenda kupanda juu meza kitambaa cheupe. Kha!
Mkuu ww ndo huwez ili wenye usongo wa maisha wanaweza
 
Hapo kwenye 300k , mtu mwenye u serious hata 200k kwa kila mwez ana save
Hapo unaachana na matumizi yote yasiyo ya lazima, mademu nao unawaweka pembeni
Yes Hio 100K nimeweka kwasababu ya nitasaidiasaidia familia zetu za kimaskini sisi tushakuwa baba ila Mimi alone nakusevia 200K hapo kwa mwezi
 
Mimi nimeajiriwa private company, sitataja mshahara wangu ila kwa mwezi bajeti yangu ni 200k

Iko hivi

10k umeme
10k maji
23k Dstv
1k sms mwezi
6k internet mwezi

Inabaki 150k

Kila siku natumia 5k × 30 days = 150k

Note: Siishi nje ya hii bajeti
 
Hiyo take home, akifungiwa kamba hata ndege mdogo (kitorondo) ama hata shorwe bwenzi...anaruka nao bab!
 
Back
Top Bottom