Mwanzo nilikuwa simuelewi elewi huyu mama, lakini mpaka sasa nimemkubali ni zaidi ya kiongozi!
Haya ni mambo ambayo yanathibitisha kuwa uongozi ni hekima Wala sio mihemuko
1: Ni mpenda haki/ anapenda haki
2: Ni msema kweli na muwazi
3: Sio mtu wa kuchukulia Jambo kwa haraka (sio mtu wa kufanyia kazi umbea)
4: Watu wote kwake ni sawa haijalishi upo chama gani (hapa ametuheshimisha kimataifa)
5: Nchi imetulia maana ilikuwa inayumba kipindi kile Cha giza
6: Sio mtu wa kupenda misifa ya kijinga
7: Kupitia teuzi hizi za wakuu wa wilaya nimemuelewa
Analinda umoja wa kitaifa kutowafukuza nassari, msando, machali, mtatiro, mashinji, kalist lazaro, nimemuona hana ubaguzi wa vyama na by the way wakuu wa wilaya waliokea upinzani wanaperform vizuri sana kuliko kawaida na kazi zao zinaonekana.