Nimeanza kuogea chumvi ya mawe kuondoa mikosi mwilini mwangu

Nimeanza kuogea chumvi ya mawe kuondoa mikosi mwilini mwangu

Hii kali, Acheni ujinga nyie.
20250529_075443.jpg
 
Nakupa Siri. Acha kuogea chumvi ya mawe haitikusaidia

Ukiwa nje, vua viatu, simama ardhini. Fungal macho wqza fikiri jinsi umekuwa mti imara, mkuwa.

Katika akili yako wasa mizizi, hii miziz, iko chini ya nyayo zako. Ona jinsi mizizi hii ikiota na kuingia ardhini, vuta picha mizizi hii inashikilia maisha yako na kukuweka imara.

☺️matatizo yako yataisha. Keep doing it
Unaonaje akishaogea chumvi akafanya na hii? 😂😂😂
Aahh dunia ina mengi hiiii!!!!!!
 
Wakuu mko salama humu?.

Baada ya kupitia changamoto nyingi za kimaisha,nikaamua kwenda kwa mganga kusafisha nyota.mganga hakua na mengi ya kunifanyia ,zaidi alinipa tu chumvi ya mawe akaniambia kila nikioga basi niiweke kwenye maji na kunuwia mahitaji yangu,mganga akaniambia nisisahau pia kulitaja jina la Mungu.
Ndo nimeanza jana rasmi kuogea hiyo chumvi.
Itakusaidia sana
 
Nikuongezee na vingine kaka
Ni bure kabisa..
Tafuta

Malumba lumba
Muosha Fedha

Chemsha kwa pamoja vichemke sana kisha ipua weka chumvi ya mawe

Vua nguo zote jifukize sana ukiwa uchi umejifunika na shuka

Ukimaliza Nenda kaogee nje huko ukinuizia changamoto zako..

Kisha Tafuta mgagani kiboko ya kuua kesi, ntakufundisha nini cha kuufanyia.

Hivi vyote ni BURE
 
Nliwahi kutana na Muuza chumvi ya mawe sokoni akilalamika biashara yake haifanyi vizuri, Nkajiuliza ina maana hii chumvi inafanya kazi kwa wanunuzi tuu au?
 
Wakuu mko salama humu?.

Baada ya kupitia changamoto nyingi za kimaisha,nikaamua kwenda kwa mganga kusafisha nyota.mganga hakua na mengi ya kunifanyia ,zaidi alinipa tu chumvi ya mawe akaniambia kila nikioga basi niiweke kwenye maji na kunuwia mahitaji yangu,mganga akaniambia nisisahau pia kulitaja jina la Mungu.
Ndo nimeanza jana rasmi kuogea hiyo chumvi.
Chumvi ya mawe ni tiba nzuri sana.
 
Hapo akimaliza anaambiwa haya lala Chali tuingize dawa.
Kuna dada mmoja anakaa mbezi alikuja kuomba ushauri eti alikua ana bwana akaachwa ghafla,Sasa waganga hawajui akakakumbuka Kuna boda alipanda yule boda akamwambia ye mganga pia,wakavadili namba za simu siku akipata tatizo amtafute.
Dada akampigia yule boda shida yake,boda akamwambia njoo kesho ijumaa akamuelekeza alipo.kufika ndoa anazuga kupandisha maruhani sijui kuomba kavaa kaniki jekundu.ikafika dada akaamabiwa vua nguo zote,lala chini,boda akapaka madubwasha kwenye naniliu yake.kilichofuataa....
Dada anasema alikua anaambiwa "sema utamu utamu utamu mara tatu.

Eti dawa itanfanya awe mtamu bwanake akirudi asimwache.


Ila sisi wanawake akili zetu!
Chai
 
Rudia madaftari yako ya 4m 3. Chumvi ni kemikali inayotokana na tukio la kikemikali (Na + CL).
Msipotoshwe, Jielimisheni.
 
Nliwahi kutana na Muuza chumvi ya mawe sokoni akilalamika biashara yake haifanyi vizuri, Nkajiuliza ina maana hii chumvi inafanya kazi kwa wanunuzi tuu au?
Good mindset.
 
Wakuu mko salama humu?.

Baada ya kupitia changamoto nyingi za kimaisha,nikaamua kwenda kwa mganga kusafisha nyota.mganga hakua na mengi ya kunifanyia ,zaidi alinipa tu chumvi ya mawe akaniambia kila nikioga basi niiweke kwenye maji na kunuwia mahitaji yangu,mganga akaniambia nisisahau pia kulitaja jina la Mungu.
Ndo nimeanza jana rasmi kuogea hiyo chumvi.
Tupe mrejesho.
 
Ungefanya hivo bila hata kwenda kwa mganga.

Chumvi ina nguvu ya asili toka kwa Mungu nguvu ya uponyaji nguvu ya wokovu nguvu ya kutibu ni nguvu ya kipekee sana .

Itakusaidia


Cc Smart911
 
Back
Top Bottom