Nimeanza kupoteza nguvu ya Macho

Muda mdogo mambo mengi.... Jihadhari sana na matumizi ya ziada ya simu na hiyo iPad mwanga wake una mionzi yenye madhara kwa macho

Jr[emoji769]
 
Nilikuwa na uwezo kujibu swali lako kwasababu nimekaa darasani miaka 10 kusoma jicho ila kwa bahati mbaya huhitaji majibu ya hospitali ok all the best katika safari yako ya kufunga na kusafisha macho na mkojo[emoji23]
Yeye anataka jibu la tatizo, alichokataa ni kwenda hospital kupima!

Kama ulikuwa na jibu kwa nini usimjibu tu? Maana bado ungekuwa ndani ya vigezo vyake!

Imenisikitisha tu, miaka 10 umekaa darasani, halafu unakuja na ngonjera kwa mgonjwa ambaye ungeweza kuonesha umahiri wako kwake

Kama kweli wewe ni msomi basi tuna msiba mkubwa kwenye elimu yetu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa na uwezo kujibu swali lako kwasababu nimekaa darasani miaka 10 kusoma jicho ila kwa bahati mbaya huhitaji majibu ya hospitali ok all the best katika safari yako ya kufunga na kusafisha macho na mkojo[emoji23]
Hapana sio sahihi unaweza kujibu kwa manufaa ya wengine lakini pia huwezi jua kapotoshwa kiasi gani kuhusu hospital hivyo jibu lako lingeweza kumuelimisha pakubwa na pengine kubadili mtazamo wake

Jr[emoji769]
 
Ushauri mzuri
 
Hapana sio sahihi unaweza kujibu kwa manufaa ya wengine lakini pia huwezi jua kapotoshwa kiasi gani kuhusu hospital hivyo jibu lako lingeweza kumuelimisha pakubwa na pengine kubadili mtazamo wake

Jr[emoji769]
Shida ya mleta mada inaitwa Presbyopia kwa kitaalamu, ni kwamba binadamu tuna lensi ndani ya jicho ambayo kazi yake ni kufocus image ya kitu katika umbali tofauti sasa jinsi umri unavyokwenda lensi hupoteza uwezo wake kwasababu inakakamaa na hvyo mtu hushindwa kufocus image za karibu hasa fine details kama maandishi na Mara nyingi tatizo huanza at 40's ,the only way anaweza saidika ni kwenda hospital akapime macho na atapewa way foward ya matibabu ni nini.
 
Kunywa juisi ya ubuyu

Source[emoji117] [emoji117] [emoji117] Afya leo: Ubuyu na faida zake - JamiiForums


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sababu gani hutaki kwenda hospitali ? Una Zaidi ya miaka 40 matatizo mengi huwa yanaanza siyo macho tuu, ni lazima uanze utaratibu wa kucheki your Blood Pressure mara kwa mara, Blood sugar, Ufanyaji kazi wa figo zako, uwezo wa kuona nk . Katika umri wako hayo hayaepukiki , hata hivyo jitahidi uwe unakula walao karoti moja yenye gram kama 200 hivi kila siku, na viazi vitamu ama tumia vitamin A suppliments
 
Mkuu kwanza pole sana kwa hilo tatizo. Pili nipende kukushuhudia kua mm pia ninatatizo kama hilo lilianza taratibu nikachukulia Poa ila Kadri siku zilivyoenda niliona mabadiliko hasa nikiendesha gari.

Niliamua kwenda hospitali nikaambiwa nimepoteza 0.5 ya uwezo wa kuona na nikapewa miwani nikaambiwa niitumie tu kwa miezi Sita then nitakua sawa.

Zoezi la dozi ya miwani likaanza toka november 2017. November 2018 nikarudi tena hospital nikamuambia doctor vip mbona sioni kama kuna kupona? Alichonijibu ndo nilimaind mbaya sana.

Doctor Ananiambia kungekua na dawa watu matajiri kama wabunge na maraisi wangekua wakwanza kupona. Hivyo miwani ndo silaha pekee ya kupambana na hali hiyo[emoji12]

Hivyo mm hua navaa miwani nikidrive tu au kukiwa na jua kali otherwise hua naiacha hasa nikiwa home tu.
 
Ndugu zanguni naomba Kama Kuna mtu ana mawasiliano ya Aghakan mwanza ama Kuna mtu anahusika maeneo Yale nashida kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…