Nimeanza kutumia PEP saa ya 38 tangu kujichoma sindano ya mtu aliyeathirika na VVU

Nimeanza kutumia PEP saa ya 38 tangu kujichoma sindano ya mtu aliyeathirika na VVU

mrisho5

Member
Joined
Dec 25, 2021
Posts
14
Reaction score
5
Habari wakuu

Katika kujipima kutumia bioline nimejikuta nimejichoma sindano niliyokuwa nimemchoma mtu mwenye HIV

Sasa nilikuwa mbali kidogo na eneo la kituo cha afya kwahiyo kesho yake ikanibidi niende kituo cha afya mida ya saa nane nikawaelezea wakanipa dawa ya pep imeandikwa LTD m nikaambiwa nianze kunywa usiku ambapo nilikunywa saa nne usiku ikiwa masaa 38 yametimia tangu kujichoma.

Je, kwa masaa hayo yaliyopita hadi nilipoanza kumeza dawa nitakuwa salama kuzuia virusi maana nilikuwa ndani ya saa 72?
 
Pole sana mkuu ila uko ndani ya mda.
Fuata ushauri wa wataalam.
 
Ondoa Hofu, uko poa...visa vya ivo vipo vingi huku mahosp .


Siku nyingine ujikamue kwanza hiyo sehem ulojichoma damu ikutoke, kisha nawa kwa maji tiririka.



Kwasasa Meza PEP Sawa sawa na ushauri ulopewa na umwombe Mungu.


Nakutia nguvu, wakati tupo Internship, Rafiki wangu mwanaaa ,amewah jichoma Mara Tano , kwahiyo amekunywa PEP Mara tano, saizi yuko poaaa.


Siku moja Ma Nurse wanazalisha, yule mama alipata mchaniko mdogo mahali ikalazimika ashonwe, Nurse mmoja wakat anashona akajichoma, wazo la kumpima upya Mzazi likaja, walivyopima wakamkuta Positive..... Nurse akaanza PEP.....yuko poaa mpaka Leo.




ALAFU UNAKUTA MTANZANIA MMOJA, KANYWA UJI, ANAKAA KUSHAMBULIA WATUMISHI WA AFYA.... [emoji23][emoji23]

Hizo Dawa maudhi yake sasa, utafurahi na roho... Zinamaaudhi balaaa, usishangae kuchoka Sana, kula Sana,Tumbo kuuma,kuharisha, kuota unapaaa, kua kama unaona maluweluwe, Mara unahisi unaitwa, miguuu kufa ganzi, kuwaka moto n.k


KULA MISOSI, YAAN ULE FOOD MARA KWA MARA ,FOOD INASAWAZISHA MAUDHI YA DAWA.


USIACHE PEP, USIISHIE NJIANI, MALIZA DOZI YAKO.
 
Fuatisha muda wa matumizi ya PEP, baada ya kumaliza utapima na utapima tena...

Bila shaka kabla hujapewa mbaazi ulipimwa...
 
Back
Top Bottom