Nimeanza Mwaka kwa Mazoezi

Nimeanza Mwaka kwa Mazoezi

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
55,727
Reaction score
123,094
Mwaka huu nimejiwekea lengo la kuwa FIT. Nimeanza mwaka kwa mazoezi sasa hivi namaliza mwezi najisikia vizuri sana. Mazoezi sio lazima uende Gym. Hata chumbani au nje ya nyumba yako unaweza kufanya mazoezi.

Kama mimi asubuhi(siku tano kwa wiki) nakimbia(jogging) kwa muda wa nusu saa kila siku kuzunguka eneo dogo tu nje ya nyumba. Jioni napiga push ups 300 siku tano kwa wiki. Hizi push ups napiga 30 mkupuo mmoja, zoezi zima huwa linachukua nusu saa.

Jogging inasaidia kuimarisha misuli ya miguu na kuimarisha moyo wakati push ups zinanisaidia kuimarisha misuli ya mikono na kiwiliwili kwa jumla. Huna haja ya kubeba machuma ili uwe fit. Jogging,sit ups,push ups zinatosha kukufanya uwe fit.
 
Push up na mimi nimechemsha, nahisi umri nao umeenda sasa, mazoezi mengine tuachie vijana
Ha ha ha ha hamna mzee hata wewe unaweza, usipige nyingi kwa mara moja. Anza hata tano halafu unaongeza taratibu. Mimi nikitaka kurudisha mwili shati likae napiga push ups tu mwezi mmoja tu nisharudi. Mimi namshukuru Mungu nikitaka ku-gain wait nafanya mazoezi nisipofanya napoteza kg hadi tano kwasababu hata kula sili sisikii njaa.
 
Mkuu fanya pia mazorzi ya kushinda njaa walau kwa wiki mara 4, uta gain sana
 
Kuruka kamba na kucheza mziki kwa masaa 4 hadi 5 mfululizo bila kupumzika ndo zoezi kubwa ambalo huwa nalifanya bila kujifikiria mara mbili.

Hongera mazoezi ni mazuri kwa afya, ukijipenda huwezi kujiacha uangamie.
 
Kuanza ni rahisi sana mkuu. Wengi tu wameshafanya hivyo. Tatizo ni kuendelea na kuwa consistent. Nidhamu ya kuendelea ndiyo inayosumbua wengi.
Basi mimi ni kinyume. Nikiacha kurudi inakuwa ngumu kidogo ila nikishaanza kuacha napo ni kazi sana.
 
Back
Top Bottom