Nimeanza ujenzi, kaa hapa tujenge pamoja

Mkuu msingi umetumia 750,000🤔
 
Ni kubwa sanaaa au ndogo sanaaa
inategemea na eneo ila kwangu ni kubwa.

kuna sehemu nilipata (wilaya mpya) nikaona nijenge tu maana nyumba za kupanga ni chache nilijenga kama ww anzia msingi kwa simenti boma nikapandisha kwa udongo,nikafunga lenta juu nimemaliza kwa simenti

Ni nyumba viwili,mziki ni kupaua maana bati ziko juu ila kenchi mteremko maana nachanisha huku huku mbao 170 haifiki laki 3
pambana mkuu mambo yatakuwa poa
 
Ahsante mkuu ngoja tupambane
 
Vitatu kimoja master, public toilet, jiko, sebule ( nadhani ni picha ila pia sio bangaroo)

Mkuu vipi gharama ya kutengenezea shimo la choo Mpk likamilike namm nataka nijue
 
USHAURI WA MDAU NTAUFANYIA KAZI....

sasa kama utaweza nilikuwa nakushauri msingi upandishe kidogo halafu ufunge na mkanda kwa uimara zaidi
nyumba ikipanda itaonekana ya kisasa zaidi bora upoteze gharama kubwa zaidi wakati wa msingi lakini uwe na nyumba nzuri na iliyopanda kwa miaka zaidi ya 30 halafu utakapopandisha kuta hakikisha inapanda tena.
hii itakusaidia kuongeza thamani na ushindani pale unapoamua kuipangisha au kuchukulia mkopo kwa biashara na fursa zijazo baadaye.
MWENYEZI MUNGU aliyekupa kibali cha kujenga afungue njia za kipato kwako.
binafsi nimefaidika watu waliniambia nahitaji trip 18 za mawe kwa nyumba ambayo kwa kiasi kikubwa inafanana kama yako au yangu ndogo kidogo hivyo umenitia nguvu ya kuendelea nafikiri mwezi ujao naweza weka trip angalau moja ya mawe kwetu huku ni 120,000/-
 
Hongera sana,sasa kama tofali za tope ukiziacha bila kuuezeka si boma litaharibika? Kwanini usipaue na kupiga plasta nje ndio ukapumzika?
 
Safi
 
Mkuu mrejesho..
Umefikia wapi
Je ulifanyaje kurekebisha msingi?
 
PIGA PICHA NIKUPE USHAURI,TOFALI PIA NIPETENDA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…