Nimeanza ujenzi, kaa hapa tujenge pamoja

Nimeanza ujenzi, kaa hapa tujenge pamoja

650 ila kuna eneo reserved kwa kazi maalumu
25*25 mbona eneo kubwa sana mkuu ukaliminya hivi, unasema kuna eneoe umelibakiza ni la nini? Umepabana sana mkuu ulikua una eneo zaidi
 
25*25 mbona eneo kubwa sana mkuu ukaliminya hivi, unasema kuna eneoe umelibakiza ni la nini? Umepabana sana mkuu ulikua una eneo zaidi
Kwa plan zangu hicho kinatosha kabisaaa eneo lingine lina kazi yake maalumu ya muda mrefu hapo kwa nilichitaji kinatosha kabisa mkuuu..... Tuombe MUNGU atupe uzima labda yajayo yatafurahisha zaidi
 
Kwa plan zangu hicho kinatosha kabisaaa eneo lingine lina kazi yake maalumu ya muda mrefu hapo kwa nilichitaji kinatosha kabisa mkuuu..... Tuombe MUNGU atupe uzima labda yajayo yatafurahisha zaidi
Okey mkuu
 
Kwa plan zangu hicho kinatosha kabisaaa eneo lingine lina kazi yake maalumu ya muda mrefu hapo kwa nilichitaji kinatosha kabisa mkuuu..... Tuombe MUNGU atupe uzima labda yajayo yatafurahisha zaidi
Kila kitu kinawezekana mkuu muombe Mungu akukamilishie ndoto zako kila la heri
 
hongera ni hatua..'
nimejengea tofali za kuchoma ni ngumu na nzuri na imara zina gharama kwenye finishing kuliko za cement sasa jitahidi kwa vyovyote usikutane na mvua za msimu hasa ikiwa umejengea udongo na hasa kama ujafunga lenta..pia kuongeza uimara kwenye angle usitumie udongo pia huko ujenzi rahisi mchanga 60000 huku ni 150000
 
Hii ni nyumba au choo?
Mawazo ya kimaskini na kishamba,huwa hamkosekani nyie yani kumiliki tecno na kuwa na access ya ku-comment JF unajikuta na wewe Star kuwavunja moyo wale wanaojaribu ku-face reality huku ukiwa juu ya mkeka kwenye chumba chako kimoja cha giza ulichopanga.

Hapo ulipo ukiulizwa bei ya mfuko mmoja wa cement hujui hata kama imepanda au imeshuka!hovyo kabisa.
 
Achana nae tufanye ye ashamaliza kiala kitu
Mawazo ya kimaskini na kishamba,huwa hamkosekani nyie yani kumiliki tecno na kuwa na access ya ku-comment JF unajikuta na wewe Star kuwavunja moyo wale wanaojaribu ku-face reality huku ukiwa juu ya mkeka kwenye chumba chako kimoja cha giza ulichopanga.

Hapo ulipo ukiulizwa bei ya mfuko mmoja wa cement hujui hata kama imepanda au imeshuka!hovyo kabisa.
 
Miezi kadhaa nyuma niliomba ushari kuhusu ujenzi. Leo narudi tena kwenu. Wazoefu na wajuzi mnisaidie.

Nitatumia tofali za kuchoma na ntajengea tope mpaka lenta ambapo ntamalizia kwa cement (ushauri wa fundi ni kwamba wakati wa upauaji tope halitahimili gonga gonga)

Nimeanza na msingi na kesho nategemea utakamilika ntaleta mrejesho hapa na gharama zake siku zijazo.

Ushauri wenu nauhitaji hapa.

Ukweli ni kwamba sitakua na uwezo wa kujenga hadi kupaua kwa mara moja nilipenda niende kwa steps.

Je, nitunze pesa mpaka zitakapo timia mpaka upauaji?? Au nijenge tu then stage ya upauaji isubiri kwa miezi mnne mpaka mitano?
Ramani niliyopewa ina roof plan ambayo sijaipenda sana je mafundi wa upauaji wanaweza kuja roof plan nzuri baada ya ujenzi kukamilika?

( Uzi huu utakua endelevu nataka uwe motivation kwa vijana wenzangu)

Gharama za MSINGI.

Wakati nanunua kiwanja kulikua na msingi mfupi wa ramani ya vumba viwili so ilinibidi nibomoe
So...

Mawe gari mbili @70,000 = 140000 hapa endapo usingekuepo mzingi ingenilazimu kununua trip 5

Mchanga gari mbili @60,000 = 120000 (huu utatumika mpaka lenta)

Maji (vinatumika visima) kusomba day 8000*3 =24000

Cement 6 20000 = 120000 zimetumika kucover nje na juu ya mawe msingi nimeyumia tope)

Fundi = 250000 (hapa fundi alitoa punguzo kutoka 350000) ametaget ujenzi wa boma apewe kazi (kulinda ofisi)/

Kamba na mambo = 15000 ( hapa fundi aliomba tu na nkampa kutoka na punguzo lake mana hua wanavyo hivi)

Usafi visiki na kubomoa msingi =20000

Kifusi = 50000 ( kipo kwa jirani yangu so nimetumia mahusiano tu) hapa kupunguza gharama ntaanza na shimo (chamber) udongo utatumika kama kifusi pia.

JUMLA 739,000 (KAMA NIKIWEKA NA GHARAMA NDOGO KAMA MAFUTA NK NI 750,000/-

Awamu ya kwanza imeishia hapa tutaendelea awamu yapi

Subscribe tujenge wote.

View attachment 1674483

Huyu fundi wako anapatikana mkoa gani boss?
 
Back
Top Bottom