Nimeanza ujenzi, kaa hapa tujenge pamoja

Nimeanza ujenzi, kaa hapa tujenge pamoja

Miezi kadhaa nyuma niliomba ushari kuhusu ujenzi. Leo narudi tena kwenu. Wazoefu na wajuzi mnisaidie.

Nitatumia tofali za kuchoma na ntajengea tope mpaka lenta ambapo ntamalizia kwa cement (ushauri wa fundi ni kwamba wakati wa upauaji tope halitahimili gonga gonga)

Nimeanza na msingi na kesho nategemea utakamilika ntaleta mrejesho hapa na gharama zake siku zijazo.

Ushauri wenu nauhitaji hapa.

Ukweli ni kwamba sitakua na uwezo wa kujenga hadi kupaua kwa mara moja nilipenda niende kwa steps.

Je, nitunze pesa mpaka zitakapo timia mpaka upauaji?? Au nijenge tu then stage ya upauaji isubiri kwa miezi mnne mpaka mitano?
Ramani niliyopewa ina roof plan ambayo sijaipenda sana je mafundi wa upauaji wanaweza kuja roof plan nzuri baada ya ujenzi kukamilika?

( Uzi huu utakua endelevu nataka uwe motivation kwa vijana wenzangu)

Gharama za MSINGI.

Wakati nanunua kiwanja kulikua na msingi mfupi wa ramani ya vumba viwili so ilinibidi nibomoe
So...

Mawe gari mbili @70,000 = 140000 hapa endapo usingekuepo mzingi ingenilazimu kununua trip 5

Mchanga gari mbili @60,000 = 120000 (huu utatumika mpaka lenta)

Maji (vinatumika visima) kusomba day 8000*3 =24000

Cement 6 20000 = 120000 zimetumika kucover nje na juu ya mawe msingi nimeyumia tope)

Fundi = 250000 (hapa fundi alitoa punguzo kutoka 350000) ametaget ujenzi wa boma apewe kazi (kulinda ofisi)/

Kamba na mambo = 15000 ( hapa fundi aliomba tu na nkampa kutoka na punguzo lake mana hua wanavyo hivi)

Usafi visiki na kubomoa msingi =20000

Kifusi = 50000 ( kipo kwa jirani yangu so nimetumia mahusiano tu) hapa kupunguza gharama ntaanza na shimo (chamber) udongo utatumika kama kifusi pia.

JUMLA 739,000 (KAMA NIKIWEKA NA GHARAMA NDOGO KAMA MAFUTA NK NI 750,000/-

Awamu ya kwanza imeishia hapa tutaendelea awamu yapi

UPDATES:
Baada ya kujenga msingi likaja swala la kujaza kifusi ambapo nilifikiria sana kuja ingehitaji gari 5 mpaka 6 kwa kila gari TSH 65,000/=

So ikanilazimu kuchumba shimo (chamber ya chooo) udongo utakaotolewa utumike kama kifusi.

Gharama ni kama ifuatavyo.
Kuchimba shimo Ft 14 (5*5) =195,000
Tofali 200 =210,000
Cement 4 =80,000
Fundi = 100,000
Wiremesh 1 + nondo mm12(1) +nondo mm 10 (5) + misumari ½ + mabanzi (7) + mbao 14 (za kukodi) + binding wire +maji + nk
GHARAMA ZA SHIMO MPAKA KUFUNIKA 736,000/=

KIFUSI KILIJAZA NA IKABAKI SEHEMU NDOGO SANAAA

NOTE.
KAZI YA KUJAZA KIFUSI NILIIFANYA MWENYEWE .

.............
MAPAKA SASA nimekwama kwenye msingi baada ya kugundua
1.mawe mengi yamesimamishwa badala ya kulazwa
2. Kina kifupi cha msingi japo ardhi ni ngumu ila kinanipa.mashaka.

Baadhi ya mafundi wanashauri niweke bim katika msingi, wengine wanasema hautaleta shida niendelee tu, mmoja alinambia atalaza nondo sehem zenye nyufa hata ndogoo tu itazuia, mwingine akasema nitafute angles muhimu niweke nguzo zitakazo kuja kuungana na bim ya msingi. mpaka sasa nimekwama cha kufanya

Ushauri wenu ni muhimu.... je nianze ujenzi au niimairishe msingi na nitumie mbinu gani kuuimarisha?
Salaaam.

UPDATES 29/10/2021

nitaenda fasta sana....

niliamua kuweka mkanda katika msingi ili kuuimarisha ambapo kila kitu kiligharimu 763,500 hivyo kufanya gharama za msingi kuwa 1,382,500.

nilianza kunyanyua boma mwezi may 2021 kwa awamu mbili....

awamu ya kwanza ilikua kufikia level ya madirisha kozi 4 na mkanda iligharimu TSH 1,705,000/= NA ILIKAMILIKA JUNE 2021

Awamu ya pili ilianza July,2021 ambapo nililenga kukamilisha boma na nilijenga kozi 9 kufikia lenta, then lenta na kumalizia kozi 3 za juu ikinigharimu TSH 3,250,000/=

Mpaka kufika hapo nilitumia tofali 1800+ ivi na nilinunua 2000

kumbuka..... gharama ninazotaja ni jumuishi ya ufundi, mbao kukodi na baadhi kununua, maji, kumwagilia nk.

awamu ya pili ilienda sambamba na kumwaga jamvi na lili gharimu TSH 430,000/=


MPAKA KUFIKIA August, 2021 boma lilikua limekamilika ka jumla ya TSH 7,519,500
inaweza kuwa kuna gharama sikuziweka kama gharama za muda, mafuta ya usafiri nk..... ila hizo ni gharama halisi

Subscribe tujenge wote.

View attachment 1991164

Muendelezo wa nimeanza Ujenzi sehemu ya pili
Ujenzi kazi sana
 
Tunauza mbao kwa bei ya jumla na rejareja :-
2*2 fut12=2500
2*3 fut 12=3500
2*2 fut12(treated) ya dawa=2800
2*2 fut18(treated) ya dawa=5000
2*4 fut12 treated(ya dawa)=5000
2*4 fut12 isiyo ya dawa=4500
1*6 fut12=4500
1*8 fut12=8500
1*8fut12 ya fisher board(treated)=9500
1*10 fut12=14000
1*10fut 12 fisher board( treated)=15000
2*4 fut18(treated)=10000
2*6 fut12=8000
1*4 fut12=2800
2*6 fut 18=19000
Tunapatikana muda wote kwa namba za simu zifuatazo:-
----0759630751
----0654830416

vile vile kuna huduma ya kuchana,kuranda na kusize mbao inapatikana ofisini kwetu pia Tunafanya delivery kwa wakazi wa Dar es salaam
Ofisi zetu zipo Tegeta-Bagamoyo road
Treated ya aina ipi unatumia, ile ya kuchemsha moja kwa moja kwenye mbao (Kama wanavyofanya Saohill) au ile ya kupakwa kama juu ya mbao kama rangi ya kucha

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
hongera mkuu, kwa sababu umesema tofali ni za udongo na unajengea udongo sikushauri kujenga boma na ukaliacha kwa muda mrefu bila kupaua maana mvua itakuharibia tofali zako na kuta kwa ujumla, ingekuwa tofali za cement kawaida ningekushauri ujenge boma na kufunga linta kisha uvute pumzi kadri utakavyo alafu upaue hata baadae sana.

Kwa hiyo sasa mimi binafsi nakushauri ujipange kwa hatua zote kwa pamoja, yani ukishapandisha boma basi ulifunike moja kwa moja alafu finishing baadae taratibu.


BTW Kila la kheri
Ushauri huo ni chanya maana akijenga kwa awamu kwa aina hiyo ya ujenzi nisawa na kazi bure maana atapata hasara
Ujenzi huo unatakiwa uwe vizuri kibajeti na ujenge msimu wa kiangazi
 
January 2023 na mm naanza aise kwa kufuata mwongozo wako huu Mkuu, Salute sana. Halafu mwendelezo wake tuweke Boss
Kupitia Mwongozo wako albab nimefika hapa, tuletea mwendelezo bac tupate madini mapya
IMG_20230404_083059.jpg
 
Mkuu hayo ni madirisha ama sehemu za kupigia chabo majirani?,anyway hongera kujenga sio lelemama
Kama siyo mtaalam huwezi kuelewa hapo nimeamua kuwa tofauti dirisha mlilozoea nimeligawa mara 2 nannimtindo wa kisasa kama utembei mtandaoni sana huwezi kuelewa
 
Back
Top Bottom