Nimeathiriwa na muziki wa kwenye radio msaada please 🙏.

Nimeathiriwa na muziki wa kwenye radio msaada please 🙏.

By the way ni addiction tuu mkuu Mimi Kusikiliza radio ama TV naenda kutimiza mwaka wa 2 sasa sifurahishwi navyo kabisaa
Huenda na mimi nitazoea hali ya kusikiliza muziki kupitia vyanzo vingine tofauti na radio.
 
Asalamaleku nyote!

Wakuu muziki wa kwenye redio (direct from the radio station) umeniathiri sana kiasi kwamba muziki ninaoupiga mwenyewe kupitia simu au kifaa kingine tofauti na ule wa kwenye radio siufurahii.

Kwa mfano ninaweza kuwa na wimbo wa Ngwair kwenye simu yangu lakini nikiupiga siufurahii lakini wimbo huo huo ukipigwa nikiwa nasikiliza radio naufurahia sana.

Hii hali inanishangaza na kunikasirisha maana miaka ya hii sisikilizi radio kama zamani hivyo hamu ya kusikiliza muziki sina.

Hebu naombeni mnipe ushauri juu ya la kufanya ili niondokane na hali hii, maana mimi ni mpenda muziki sana lakini sasa hivi Sina ashiki nao.

Cc Monetary doctor KENZY Chaliifrancisco and 100 others Dr am 4 real PhD.
Itakuwa una akili mnemba!
 
Mimi zamani nilikuwa sipendi kusikia mtu anasikiliza wimbo ambao ninao (cassette) nilikuwa naona kama kaiba wimbo wangu
 
Radio station zinatoa mziki wenye ubora wa juu ndio maana nimekupa app ambayo huwa haipotezi ubora wa mziki ukipakua ngoma
Hujamuelewa mtoa mada aisee, We unadhani kuna Platform zina sound Quality nzuri kama Spotify au Boomplay?
Sema tena vizuri anacho adresss
 
Back
Top Bottom