Nimeboreka mpaka basi

Pole sana kwa kukereka!
Lakini inaonekana umemzoesha kumuazima!
 

Unajua kuna vitu vya kuazimana kama binadamu. Kitu kama gari na vinginevyo ambavyo vinawezaleta uhasama, ni vizuri ukawa muwazi kuliko kuwa mnafiki unamwazima mtu halafu anaharibu.Ni vizuri mtu akutie majina yote ya ubaya ila kitu chako kiwe salama.
 
sasa utkuwa umejifunza kutoazima gari yako hovyo hovyo. wakati mwengine inaweza kuwa ni ya kwenda kuchukua kwa brekidawni kabisa
 
mmmmh, hiyo gari ulipewa au ulinunua??

Kuazimana magari??? Never!

Pole lakini!

Kongosho kuazima au kuazimwa gari mi sioni kama ni tatizo. Binafsi nimewaazima watu gari mara kadhaa na mimi pia nimeshawahi kuazima ya rafiki zangu zaidi ya mara moja. Kikubwa ni kuwa na ustaarabu kinapotokea kitu kama hiki. Niliwahi kumuazima rafiki yangu siku moja akaligonga gari. Hata hivyo, yeye alikuwa mstaarabu maana alinipigia simu na kwenda kulinyoosha.
Ajali ni bahati mbaya, na gari ni kitu cha kupita tu .....! Msaidie mtu pale inapobidi.
 
Mbona siku hizi usafiri wa Daladala upo saafi tu? Acheni kupenda makuu...! Wewe huna uwezo wa kutengeneza "boneti" ya gari ni kwanini unamiliki gari? Na huyo mwenzio anakwenda kwenye shughuli gani ambazo anahitaji gari wakati hata kuendesha gari hajui? SoB...!
 
Mambo mengine ni umri tu nadhani.Kuazimana magari kwa vijana labdaNa utu uzima huu?? Siwezi kwa kweli.
 
kuazima = tamaa! mtu haridhiki na chake, au kama huna na unakipenda struggle upate lako/ chako! inakera sanaaaaaaaa!
 
Mambo ya kuazima kitu chochote kwangu mwiko...................
 
Mambo mengine ni umri tu nadhani.Kuazimana magari kwa vijana labdaNa utu uzima huu?? Siwezi kwa kweli.

Kongosho una mambo!, Umri hautaki kusaidiana? Anyway nafahamu pia jambo hili vile vile ni jinsi ambavyo mtu mwenyewe analitafsiri pamoja na ukaribu na hao watu waliomzunguka. Nafikiri ni vyema kila mtu aamue jinsi ambavyo anaona yeye mwenyewe kuwa ni sawa ndani ya nafsi yake, kuazimana au kutokuazimana! Yaani hapa tu ninapoandika kaja jamaa kuniazima gari anaenda bank mara moja, kisa? parking kuna mto kam-block kwa nyuma hivyo kashindwa kutoa gari yake, lol! Kazi kweli kweli ila nimempa ....
 
hata kama wote mnamiliki pia hakuna sababu ya kuazimana. Au ndio mambo ya kutokeleza!!!

Gari ni mashine, wakati mwiningine lazima liende matengenezo, watu wengine ktk shughuli zao gari ni lazima.
 
same here....mimi hata baiskeli yangu mtu haendeshi........
tabia ya kuazimana vitu (sio gari pekee) ni tabia mbaya sana.....lazima mgombane......hasa pesa.....

We utakuwa mangi wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…