Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna rafiki yangu huwa ananiazima gari kwenda kwenye shughuli zake.
Lakini kama mwezi umepita gari ilikuwa haifungi boneti, nikamwambia hawezi kutembeza kwani boneti haifungi. Akaniambia haina tatizo atatengeza tu kwani tatizo dogo. Sasa jana karudi bneti imefunguka akiwa anaendesha ikagonga kioo cha mbele na show yake ya mbele kwenye boneti imetoka na haijulikani ipo wapi. Nilimuuliza kama alitengeneza akasema alikuwa bado hajatengeneza. Hapo nilikasirika sana gari ipo nyang'a nyang'a. Alichoniambia ni kuwa yaani unajali gari kuliko uzima wangu? Na hapo hana hela ya kutengeneza., sijamjibu kitu na mpaka sasa sitaki hata kumwona.
mmmmh, hiyo gari ulipewa au ulinunua??
Kuazimana magari??? Never!
Pole lakini!
sasa utkuwa umejifunza kutoazima gari yako hovyo hovyo. wakati mwengine inaweza kuwa ni ya kwenda kuchukua kwa brekidawni kabisa
Kongosho kuazima au kuazimwa gari mi sioni kama ni tatizo. Binafsi nimewaazima watu gari mara kadhaa na mimi pia nimeshawahi kuazima ya rafiki zangu zaidi ya mara moja. Kikubwa ni kuwa na ustaarabu kinapotokea kitu kama hiki. Niliwahi kumuazima rafiki yangu siku moja akaligonga gari. Hata hivyo, yeye alikuwa mstaarabu maana alinipigia simu na kwenda kulinyoosha.Ajali ni bahati mbaya, na gari ni kitu cha kupita tu .....! Msaidie mtu pale inapobidi.
Mambo mengine ni umri tu nadhani.Kuazimana magari kwa vijana labdaNa utu uzima huu?? Siwezi kwa kweli.
una akili sana wewe.
hata kama wote mnamiliki pia hakuna sababu ya kuazimana. Au ndio mambo ya kutokeleza!!!
same here....mimi hata baiskeli yangu mtu haendeshi........
tabia ya kuazimana vitu (sio gari pekee) ni tabia mbaya sana.....lazima mgombane......hasa pesa.....